Monday, August 25, 2014

BAADA YA JAJA NAYE COUTINHO AFUNGUA AKAUNTI YA MAGOLI YANGA FC

Mohamed Abdallah, Zanzibar Andrey Coutinho amefanikiwa kupiga bao na kuisaidia Yanga kuifunga Shangani inayoshiriki Ligi Daraja la Pili hapa. Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, moja likiwa limesababishwa na Salum Telela ambaye alipiga krosi safi mabeki wa Shangani wakajifunga. Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa, ilikuwa nzuri nay a kuvutia. Coutinho alionekana kuwa fiti zaidi huku Mbrazili mwenzake, Jaja akibanwa. Yanga ilicheza kwa kuelewana tokea mwanzo, lakini baadaye Shangani nao walijibu mashambulizi na kuifanya mechi kuwa ya ushindani. Chini ya Marcio Maximo, Yanga itacheza mechi nyingine moja ya kirafiki Jumatano kabla ya kurejea jijini Dar.

SIMBA SC YAIJIBU YANGA SC, YAUA 2-1 AMAAN USIKU HUU

Mohamed Abdallah, Zanaibar Kikosi cha Simba kinachoongozwa na Patrick Phiri, kimeishinda Kilimani ya daraja la pili Zanzibar kwa mabo 2-1 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa. Ingawa ina kikosi kinachoundwa na Kilimani wengi kweli, Chipukizi ilionyesha soka safi na la kuvutia. Timu hiyo inasifika kwa soka la kasi na pasi nyingi ikiwa Simba wakati mgumu kwa muda mwingi. Simba ndiyo ilianza kupata bao kupitia Amissi Tambwe kwa mkwaju wa penalti lakini Kilimani wakasawazisha katika dakika ya 78. Simba walifanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 84 kupitia Haruna Chanongo.NA MDADISI BLOG /FESTOSAIMON

MAN UNITED, REAL MADRID ZAMALIZANA KWA DI MARIA, ANATUA LEO ENGLAND

Real Madrid imekubali kumuachia Angelo Di Maria ambaye anatua Man United kw akitita cha pauni milioni 64. Uhamisho wake utavunja rekodi na kuwa ghali zaidi England ukiupita ule wa pauni milioni 50 wakati Fernando Torred alipotua Chelsea akitokea Liverpool. Di Maria raia wa Argentina, anatarajia kutua jijini Manchester leo kwa ajili ya vipimo na kumalizana na wenyeji wake. Kocha Carlo Ancelotti wa Madrid amethibitisha kwamba mkali huyo alikwenda kuwaaga mazoezini kwamba anaondoka. Man United imekuwa ikifanya juhudi kujiimarisha baada ya kusuasua kwa msimu mzima na pia kuanza vibaya msimu mpya kwa kipigo na sare dhidi ya Swansea na Sunderland. NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON

Sunday, August 24, 2014

SPURS YAUA 4-0, ADEBAYOR NAYE ATUPIA NYAVUNI

Wazee wa dozi; Mshambuliaji wa Spurs, Emmanuel Adebayor akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao katika ushindi wa 4-0 dhidi ya QPR Uwanja wa White Hart Lane. Mabao mengine ya Tottenham Hotspur yamefungwa na Chadli mawili na moja Eric Dier kikosi cha Mauricio Pochettino kiking'ara leo katika Ligi Kuu ya England

DI MARIA SASA NI MOJA, MBILI, TATU, NNE.....

Muda wa mshambuliaji Angelo Di Maria kuondoa Real Madrid unaanza kuhesabika. Pamoja na kutangaza dau jipya la zaidi ya pauni milioni 70 ili Manchester United impate, lakini inaonekana Madrid imeshindwa kumzuia. Kwani leo asubuhi hakuonekana mazoezini na kitendo cha kocha Carlo Ancelotti kutomjumuisha kwenye mechi za Super Cup ya Hispania, inaonyesha kiasi gani hayuko kwenye hesabu za timu hiyo. Siku nne zilizopita, Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos walizungumza na uongozi na kuutaka ufanye juhudi kumbakiza. Lakini Muargentina huyo anaonekana kuchoshwa na kutopewa heshima yake, hivyo anaweza kuondoka ndani ya leo au kesho. Na mdadisiblog/festosaimon

DIEGO COSTA AKIVUTA MEHELA BAADA YA KUIPIGIA BAO CHELSEA JANA

Piga bao, vita mkwanja; Mshambuliaji mpya wa Chelsea Diego Costa aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 32 kutoka Atletico Madrid akitoa fedha kwa mashine za benki (ATM) muda mfupi baada ya kuifungia Chelsea katika ushindi wa 2-0 jana dhidi ya Leicester katika Ligi Kuu ya Englans. Diego amefunga mechi zote mbili za awali za Chelsea.

Mwanzo mzuri: Costa akishangilia bao lake la jana dhidi ya Leicester Uwanja wa Stamford Bridge dakika ya 62

JOSE MOURINHO AWACHARUKIA DIEGO COSTA NA WENZAKE LICHA YA KUSHINDA 2-0 DHIDI YA LEICESTER

Kibarua kizito: Diego Costa aliifungia Chelsea bao la kuongoza dhidi ya timu ngumu ya Leicester. JOSE Mourinho aliwajia juu wachezaji wake kuwa ni wavivu kufuatia kucheza vibaya kipindi cha kwanza licha ya ushindi wa mabao 2-0 waliopata jana dhidi ya Leicester. Chelsea walibanwa mbavu kipindi cha kwanza na timu mpya iliyopanda daraja ya Leicester kabla ya Mourinho kuwawashia moto wachezaji wake wakati wa mapumziko. Mabao ya Diego Costa na Eden Hazard yalitosha kuwapa ushindi The Blues katika dimba la Stamford Bridge. Vijana kazeni: Jose Mourinho aliwajia juu wachezaji wake baada ya kipindi cha kwanza kumalizika. Mourinho hakafurahishwa na mwanzo wa taratibu. Alisema: “Napenda kufanya mazoezi asubuhi, lakini wiki hii nilifanya mazoezi mchana kwasababu sio hali nzuri ya kucheza mpira, unapata uvivu”. “Kipindi cha kwanza timu ilicheza kivivu na sikupenda kabisa. “Lakini walijiboresha kipindi cha pili na kushinda, hiki ndicho kitu muhimu zaidi” “Wakati wa mapumziko tuliwakalipia kidogo. Niliwaambia kuwa jinsi tunavyocheza haitoshi kushinda mchezo na walikuwa katika hatari”. NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON

Fifa yataka kina Ronaldo wakacheze Morocco (kwenye EBOLA)

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa) limethibitisha kwamba Morocco itakuwa mwenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa Dunia kwa mwaka wa pili mfululizo licha ya kuwapo na wasiwasi wa ugonjwa wa Ebola. Maeneo ya Afrika Magharibi yamekuwa tishio kubwa kutokana na kuibuka kwa virusi hivyo vya ugonjwa wa Ebola na kuibua wasiwasi kama ni mwafaka kwa michuano hiyo kufanyika Morocco Desemba mwaka huu. Hata hivyo, Fifa imetangaza kwamba hakuna haja ya kuwa na wasiwasi na timu zitakuwa kwenye mazingira mazuri. “Afya za wachezaji, maofisa na mashabiki ni kitu kinachozingatiwa zaidi na Fifa kwenye michuano yake,” ilibainisha taarifa ya shirikisho hilo. “Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba hakuna kesi yoyote ya Ebola iliyoripotiwa Morocco, hivyo hakuna sababu ya kuzungumzia kubadili sehemu ya kufanyika kwa michuano hiyo. Kama kutakuwa na mabadiliko tutatoa taarifa.” Miongoni mwa timu zitakazoshiriki ni Real Madrid inayochezewa na masupastaa wa dunia, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, James Rodriguez na Toni Kroos.

Kigogo Simba akwama kumuiba Okwi Jangwani

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Emmanuel Okwi, huenda akaiingiza hasara klabu hiyo na inaweza kulazimika kuvunja mkataba wake kama hatajiunga nayo mpaka usajili utakapofungwa Agosti 27 huku ikielezwa kuwa kuna ujanja ulifanyika wa kughushi barua ya timu iliyoelezwa kuwa ana mpango wa kujiunga nayo. Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinadai kuwa Okwi ni mchezaji anayewasumbua na amechukua fedha nyingi, lakini katika uchunguzi uliofanywa umebainisha kuna mmoja wa wanazi na kiongozi wa Yanga alishirikiana na kigogo wa Simba kutaka kumrubuni Okwi kwa kughushi barua kwamba kuna timu inamtaka. Habari zinasema kwamba viongozi wa Yanga walifuatilia kwa umakini juu ya madai ya kuwapo kwa timu inayomtaka na kubaini kuwa barua iliyotumwa Yanga haikutoka katika klabu hiyo ambayo hata hivyo haitajwi wazi. Yanga ilimsajili Okwi kwa Sh116milioni na inamlipa mshahara wa Sh6milioni kwa mwezi. “Tulibaini kuna ujanja ulifanyika kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Yanga akishirikiana na mtu wa Simba kutengeneza uongo kwani klabu waliyosema inamtaka haina taarifa zozote, walitaka Okwi aachiwe ili ajiunge na Simba, hivyo bado tunaangalia jinsi ya kumchukulia hatua kiongozi huyo,” alidokeza kigogo wa Yanga. “Hapa kuna mawili, Yanga kuingia hasara kwa kuvunja mkataba na Okwi au Okwi kuendelea kuwepo katika timu, ila napo itategemea na kocha atakavyoamua kwani hataki mchezaji ambaye hana utayari wa kucheza, Okwi alisema atarudi ila hatujui ni lini.” Kwa upande wa Simba, ilielezwa kwamba suala la Okwi lilitinga katika vikao vya Kamati ya Usajili na kuleta mtafaruku mkubwa kwani wajumbe walio wengi hawakukubaliana na Okwi kurudi ingawa kigogo mmoja akawa anashinikiza na hakuungwa mkono.Credit mwanaspoti

KWA MZIGO WA PAUNDI MILIONI 60 ANGEL DI MARIA ANATUA OLD TRAFFORD

Fundi: Angel Di Maria aliichezea Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid katika mechi ya Super Cup MANCHESTER United wanakaribia kukamilisha usajili ghali wa Muargentina, Angel Di Maria kwa paundi milioni 60. Uhamisho huo ukikamilika utavunja rekodi ya klabu hiyo katika usajili. United wamekuwa wakifuatilia dili la nyota huyo wa Real Madrid kwa muda mrefu na inafahamika kuwa wametoa ofa ya mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki. kwa sasa inafahamika kuwa Di Maria imewaambia United kuwa atakuja Old Trafford na sasa klabu hiyo ipo katika mazungumzo ya kukubaliana ada ya uhamisho na Real madrid. Kiwango cha juu: Di Maria anatarajia kujiunga na Manchester United kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 60 na mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki. Kifaa cha ukweli: Gary Neville anaamini kuwa Di Maria ndio aina ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa na Manchester United. Na mdadisiblog/festosaimon

Ingia hapa kusoma habari zngine>>>> BONYA HAPA