Muda wa mshambuliaji
Angelo Di Maria
kuondoa Real Madrid
unaanza kuhesabika.
Pamoja na kutangaza
dau jipya la zaidi
ya pauni milioni 70
ili Manchester
United impate,
lakini inaonekana
Madrid imeshindwa
kumzuia.
Kwani leo asubuhi
hakuonekana
mazoezini na kitendo
cha kocha Carlo
Ancelotti
kutomjumuisha kwenye
mechi za Super Cup
ya Hispania,
inaonyesha kiasi
gani hayuko kwenye
hesabu za timu hiyo.
Siku nne zilizopita,
Cristiano Ronaldo na
Sergio Ramos
walizungumza na
uongozi na kuutaka
ufanye juhudi
kumbakiza.
Lakini Muargentina
huyo anaonekana
kuchoshwa na
kutopewa heshima
yake, hivyo anaweza
kuondoka ndani ya
leo au kesho. Na mdadisiblog/festosaimon |
0 comments:
Post a Comment