MSHAMBULIAJI wa Yanga,
Emmanuel Okwi, huenda akaiingiza
hasara klabu hiyo na inaweza
kulazimika kuvunja mkataba wake
kama hatajiunga nayo mpaka
usajili utakapofungwa Agosti 27
huku ikielezwa kuwa kuna ujanja
ulifanyika wa kughushi barua ya
timu iliyoelezwa kuwa ana mpango
wa kujiunga nayo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya
Yanga zinadai kuwa Okwi ni
mchezaji anayewasumbua na
amechukua fedha nyingi, lakini
katika uchunguzi uliofanywa
umebainisha kuna mmoja wa
wanazi na kiongozi wa Yanga
alishirikiana na kigogo wa Simba
kutaka kumrubuni Okwi kwa
kughushi barua kwamba kuna timu
inamtaka.
Habari zinasema kwamba viongozi
wa Yanga walifuatilia kwa umakini
juu ya madai ya kuwapo kwa timu
inayomtaka na kubaini kuwa barua
iliyotumwa Yanga haikutoka katika
klabu hiyo ambayo hata hivyo
haitajwi wazi. Yanga ilimsajili Okwi
kwa Sh116milioni na inamlipa
mshahara wa Sh6milioni kwa
mwezi.
“Tulibaini kuna ujanja ulifanyika
kutoka kwa mmoja wa viongozi wa
Yanga akishirikiana na mtu wa
Simba kutengeneza uongo kwani
klabu waliyosema inamtaka haina
taarifa zozote, walitaka Okwi
aachiwe ili ajiunge na Simba, hivyo
bado tunaangalia jinsi ya
kumchukulia hatua kiongozi huyo,”
alidokeza kigogo wa Yanga.
“Hapa kuna mawili, Yanga kuingia
hasara kwa kuvunja mkataba na
Okwi au Okwi kuendelea kuwepo
katika timu, ila napo itategemea
na kocha atakavyoamua kwani
hataki mchezaji ambaye hana
utayari wa kucheza, Okwi alisema
atarudi ila hatujui ni lini.”
Kwa upande wa Simba, ilielezwa
kwamba suala la Okwi lilitinga
katika vikao vya Kamati ya Usajili
na kuleta mtafaruku mkubwa
kwani wajumbe walio wengi
hawakukubaliana na Okwi kurudi
ingawa kigogo mmoja akawa
anashinikiza na hakuungwa
mkono.Credit mwanaspoti |
0 comments:
Post a Comment