SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa
(Fifa) limethibitisha kwamba
Morocco itakuwa mwenyeji wa
michuano ya Klabu Bingwa Dunia
kwa mwaka wa pili mfululizo licha
ya kuwapo na wasiwasi wa
ugonjwa wa Ebola.
Maeneo ya Afrika Magharibi
yamekuwa tishio kubwa kutokana
na kuibuka kwa virusi hivyo vya
ugonjwa wa Ebola na kuibua
wasiwasi kama ni mwafaka kwa
michuano hiyo kufanyika Morocco
Desemba mwaka huu.
Hata hivyo, Fifa imetangaza
kwamba hakuna haja ya kuwa na
wasiwasi na timu zitakuwa kwenye
mazingira mazuri.
“Afya za wachezaji, maofisa na
mashabiki ni kitu kinachozingatiwa
zaidi na Fifa kwenye michuano
yake,” ilibainisha taarifa ya
shirikisho hilo.
“Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni
kwamba hakuna kesi yoyote ya
Ebola iliyoripotiwa Morocco, hivyo
hakuna sababu ya kuzungumzia
kubadili sehemu ya kufanyika kwa
michuano hiyo. Kama kutakuwa na
mabadiliko tutatoa taarifa.”
Miongoni mwa timu zitakazoshiriki
ni Real Madrid inayochezewa na
masupastaa wa dunia, Cristiano
Ronaldo, Gareth Bale, James
Rodriguez na Toni Kroos. |
0 comments:
Post a Comment