Kibarua kizito:
Diego Costa
aliifungia
Chelsea bao la
kuongoza dhidi
ya timu ngumu
ya Leicester.
JOSE Mourinho
aliwajia juu
wachezaji wake
kuwa ni wavivu
kufuatia
kucheza vibaya
kipindi cha
kwanza licha ya
ushindi wa
mabao 2-0
waliopata jana
dhidi
ya Leicester.
Chelsea
walibanwa
mbavu kipindi
cha kwanza na
timu mpya
iliyopanda
daraja
ya Leicester
kabla ya
Mourinho
kuwawashia
moto wachezaji
wake wakati wa
mapumziko.
Mabao ya Diego
Costa na Eden
Hazard
yalitosha
kuwapa ushindi
The Blues
katika dimba la
Stamford
Bridge.
Vijana kazeni:
Jose Mourinho
aliwajia juu
wachezaji wake
baada ya kipindi
cha kwanza
kumalizika.
Mourinho
hakafurahishwa
na mwanzo wa
taratibu.
Alisema:
“Napenda
kufanya
mazoezi
asubuhi, lakini
wiki hii
nilifanya
mazoezi
mchana
kwasababu sio
hali nzuri ya
kucheza mpira,
unapata uvivu”.
“Kipindi cha
kwanza timu
ilicheza kivivu
na sikupenda
kabisa.
“Lakini
walijiboresha
kipindi cha pili
na kushinda,
hiki ndicho kitu
muhimu zaidi”
“Wakati wa
mapumziko
tuliwakalipia
kidogo.
Niliwaambia
kuwa jinsi
tunavyocheza
haitoshi
kushinda
mchezo na
walikuwa
katika hatari”. NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON |
0 comments:
Post a Comment