Saturday, August 30, 2014

CHEKI BALOTELLI ANAVYOFURAHIA MAISHA LIVERPOOL, UTAFIKIRI MWENYEJIII

BARUA INAYOVUNJA MKATABA WA YANGA NA OKWI HII YAPA

SIKIA HII KALI YA MANJI KUTAKA AWANUNUE WACHEZAJI WA SIMBA, HALAFU WASICHEZE LIGI

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, leo ametoa kali kwenye kikao chake na waandishi wa habari aliposema kwamba ana uwezo wa kuwanuanua wachezaji wa Simba, halafu wasicheze ligi na badala yake wawe wanafanya mazoezi Covo Beach tu. Manji amesema hayo wakati akipinga Simba kutangaza kumsajili mshambuliaji Emmanuel Okwi. Manji amesema suala hilo ni sawa na uhuni kwa kuwa Simba inajua Okwi ana mkataba na Yanga. “Kama itakuwa ni kufanya mambo kwa staili ya kihuni, hata mimi ninaweza kuamua kuwanunua wachezaji wa Simba sijui kina (Amissi) Tambwe na wenzake, halafu wawe wanafanya mazoezi Coco Beach tu, wasicheze ligi. “Lakini busara ni jambo jema, lakini nione kwamba ninachofanya ni kitu gani na hasara zake ni zipi. “Umesikia sisi (Yanga) tumelalamika kuhusiana na usajili wa Domayo au Kavumbagu kwenda Azam FC. Kila kitu kilikwenda kwa utaratibu. “Hata Simba wanaosema kuhusiana na suala la Okwi pia hawajui, sisi hatukuzozana na Simba, utaona Okwi wakati anakuja Yanga tulifuata utaratibu na kumalizana na SC Villa. “Simba hawakuwa na tatizo na Okwi, badala yake Etoile du Sahel ya Tunisia ambayo Yanga hatukufanya nao biashara. Hakukuwa na sehemu ambayo inatugonganisha,” alisema. “Sasa kama kuna lengo la kufanya ili kuikomoa au kuona ni kulipa kisasi, basi ni kujidanganya tu na kutaka kufanya mambo yaende kwa kukomoana ambalo si jambo zuri. “Ndiyo maana tumetoa siku saba tuwaachie TFF washughulikie madai yetu, ikishindikana, Caf, Fifa au Cas bado ni sehemu tunazoweza kwenda,” alisisitiza Manji. “Pia kusema Okwi amevunja mkataba nasi ni kujidanganya. Iko wapi barua aliyonayo yeye kwamba tumevunja naye mkataba. “Hata majina tumetuma sita, tungejua lipi la kulitoa kwa kuwa hadi Septemba 6 ndiyo mwisho wa kusajili wageni. Haraka ya nini

Posted via Blogaway

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA LEO JUMAMOSI ZIPO HAPA

Real Madrid wamekamilisha uhamisho wa pauni milioni 20 wa Radamel Falcao, 28, kutoka Monaco (Calciomercato), Arsenal wana matumaini ya kukamilisha uhamisho wa beki Sorkatis Papastathopoulos, 26, kutoka Borussia Dortmund, lakini wamesema hawatalipa pauni milioni 20 (Daily Mirror), boss wa Aston Villa Paul Lambert ametoa dau la pauni milioni 8 kumtaka kiungo wa Manchester United Tom Cleverly, 25, (Daily Telegraph), lakini Lambert huenda wakapata upinzani mkali kutoka Valencia, ambao nao pia wamepanda dau kwa Cleverly (Sky Sports), Danny Welbeck, 23, anajiandaa kuondoka Old Trafford, na akitajwa kwenda Tottenham kwa mkopo (Daily Star), Chelsea wanakaribia kutoa ruhusa kwa Fernando Torres, 30, kwenda Inter Milan (Times), Manchester United wameongeza bidii kumfuatilia kiungo Martin Odegaard, 15, anayechezea Stromsgodset kutoka Norway (Daily Telegraph), Valencia na Juventus wametoa dau la kutaka kumsajili Javier Hernandez, 26, kutoka Manchester United kwa kiasi cha pauni milioni 15 (Guardian), mshambuliaji Demba Ba, 29, alikaribia kujiunga na Arsenal kabla ya kusaini kwenda Besitkas ya Uturuki kutoka Chelsea kwa pauni milioni 8 (Independent), kiungo anayesakwa na Manchester United Arturo Vidal, 27, amekaririwa akisema hataki kuondoka Juventus (Daily Express), kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song, 26, ana matumaini ya kurejea katika Premier League na Liverpool baada ya Barcelona kuonekana kutomtaka (Daily Mirror), kiungo wa PSG Adrien Rabiot ambaye mkataba wake unaisha msimu ujao anasakwa na Roma na Arsenal (Le Parisien). Zimesalia siku mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. By salim kikeke

Posted via Blogaway

Je Toni Kroos ndio kamkimbiza Alonso Madrid? Xab Alonso ajibu.

Kiungo wa kimataifa wa Spain Xabi Alonso amejiunga na klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani akitokea kwa mabingwa wa ulaya Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 5. Alonso ambaye alijunga na Real Madrid akitokea Liverpool ametambulishwa rasmi leo hii kwenye mkutano waandishi wa habari na kutoa sababu ambayo imemfanya mpaka akaamua kuondoka Santiago Bernabeu. Kiungo huyo ambaye juzi alitangaza kujiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Hispania amesema kwamba kilichomfanya kuhama Madrid sio upinzani wa namba kama inavyodhaniwa na wengi. “Klabu haikutaka niondoke, ulikuwa uamuzi wangu mwenyewe kuondoka. Baada ya kushinda La Decima, nilihisi nahitaji changamoto mpya. Nilihisi muda wa kuondoka umefika,” Alonso aliwaambia waandishi wa habari. “Sikuamua kuondoka kwa sababu ya ujio wa Toni Kroos. Madrid wamefanya usajili mzuri sana na tungecheza wote kwa muda mwingi. Hivyo sikuondoka kwa sababu yake, nilihitaji tu changamoto mpya. “Bayern ndio lilikuwa chaguo sahih kwangu mimi.” – Alonso

Posted via Blogaway

Alichojibu Ronaldo kuhusu Di Maria kujiunga na Man Utd na kupewa jezi namba 7

Siku moja baada ya Angel Di Maria kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa klabu ya Manchester United ya England huku akikabidhiwa jezi yenye historia kubwa ndani ya klabu hiyo (namba 7), mwanasoka bora wa ulaya na mchezaji wa zamani wa United, Cristiano Ronaldo amezungumza juu ya Di Maria kwenda Old Trafford pamoja na kupewa jezi namba 7. Ronaldo ambaye aliondoka Man United mnamo mwaka 2009 kwa ada ya uhamisho ambayo iliweka rekodi ya £80m amesema hana wasiwasi wa Di Maria kufanikiwa ndani ya United. “Uhamisho huu ni kitu kizuri kwake.” Ronaldo aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Monaco. “Manchester [United] ni moja ya klabu kubwa duniani, ni sehemu nzuri kwa Di Maria na namtakia kheri na mafanikio, Di Maria ni mchezaji mzuri sana, anastahili kuichezea United.” Alipoulizwa juu ya Di Maria kupewa jezi namba 7 aliyokuwa akivaa alipokuwa Man United, Ronaldo alisema: “Nilimwambia, ‘jezi No.7 ina maana kubwa ndani ya United, lakini nadhani ataweza kubeba uzito wa jezi kwa sababu ni mchezaji mzuri sana.” Di Maria anaweza kuanza kuichezea Man U kesho kwenye mchezo dhidi ya Burnley.b

Posted via Blogaway

Shinji Kagawa njiani kuondoka Man United – hii ndio klabu anayoenda

Wakati wa utambulisho rasmi wa Angel Di Maria jana, kocha qa man United Louis Van Gaal alithibitishqa kwamba kuna kundi la wachezaji litaondoka mpaka kufikia mwishoni mwa wiki hii. Leo hii zimetoka taarifa kwamba kiungo wa kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa ni mmoja wa wachezaji wanaondoka kwenye klabu hiyo kabla ya kuisha kwa dirisha la usajili. Shinji anatarajiwa kujiunga na klabu yake ya zamani ya Borrusia Dortmund kwa ada ya uhamisho wa £8m. Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Ujerumani leo hii tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha usajili wake Dortmund. Kagawa alijiunga na Man United miaka mitatu iliyopita kwa ada ya uhamisho wa £12m.

Posted via Blogaway

Hiki ndio kinachomfanya Marcos Rojo asianze kuichezea Man United

Imepita zaidi ya wiki moja tangu klabu ya Manchester United ilipokamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Argentina Marcos Rojo kutoka klabu ya Sporting Lisbon – lakini cha ajabu mchezaji huyo amekuwa haonekani kwenye mechi za United. Leo hii imefahamika kwamba mchezaji huyo bado hajapata kibali cha kumuwezesha kufanya kazi nchinin UK – kitu kinachomfanya timu yake ishindwe kupata idhini ya premier league kumchezesha mchezaji huyo. Mwanzoni kulikuwa wasiwasi kwamba utata wa kisheria uliopo kati ya klabu yake ya zamani Sporting dhidi ya kampuni ya Doyen Sports ambayo ilikuwa inamiliki asilimia 75 ya haki zake za usajili. Lakini leo hii kocha wa Man united Louis van gaal amethibitisha mchezaji huyo amekwama kutokana na kibali cha kazi na sasa yupo nchini Hispania ambapo ndio kuna ubalozi wa Argentina akifuatilia kibali hicho. Hata hivyo Van Gaal amesema suala hilo sasa halitachukua muda mrefu, pia akathibitisha kwamba Angel Dimaria anaweza kuanza kesho kwenye mchezo dhidi ya Burnley.

Posted via Blogaway

HATIMAYE TORRES AONDOKA CHELSEA AENDA TIMU HII

HATIMAYE mshambuliaji Fernando Torres amemaliza miaka yake mitatu na nusu migumu Chelsea kwa kukubali kuhamia AC Milan. Mchezaji huyo wa Hispania anakwenda kuziba pengo la Mario Balotelli ambaye Milan imemuuza kwa Pauni Milioni 16 Mtaliano huyo Liverpool. Wakala wa Torres alifanya mazungumzo na Milan Alhamisi asubuhi na mshambuliaji huyo amekubali kujiunga na vigogo hao wa Italia kwa miaka miwili. Amechuja: Licha ya kusajiliwa kwa Pauni Milioni 50 kutoka Liverpool, Torres amemudu kufunga mabao 45 tu katika mechi 172 alizocheza Chelsea Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anahamia San Siro kwa mkopo wa miaka miwili. Torres aliyetua Stamford Bridge kwa dau la Pauni Milioni 50 alikuwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa Pauni 150,000 kwa wiki Stamford Bridge na inaaminika wawakilishi wake walipatana kiasi hicho hicho cha mshahara kabla ya mchezaji huyo kukubali uhamisho huo. Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alikuwa radhi kumuacha Torres kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu ili kupata nafasi ya kusajili mshambuliaji mwingine na Loic Remy sasa yupo kwenye nafasi nzuri ya kutua Magharibi mwa London kutoka Queens Park Rangers.

Posted via Blogaway

Friday, August 29, 2014

DI MARIA AMESEMA CRISTIAN RONALDO ALIMPA TAARIFA ZA NAMBA SABA YA MAN UNITED

Kiungo mshambuliaji mpya wa Man United, Angel Di Maria amesema ana taarifa kuhusiana na jezi namba 7. Di Maria amesema ana taarifa za heshima kubwa ya jezi hiyo kwa kuwa alizungumza na Ronaldo ambaye aalikuwa anakipiga naye Real Madrid. Amesema pamoja na uongozi wa Man United kutaka aivae, hata yeye alikuwa akitaka kuivaa jezi hiyo.

Posted via Blogaway

MANJI ASISITIZA, SIMBA WAMEKURUPUKA KWA OKWI

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema Simba wamekurupuka katika suala la Emmanuel Okwi. Manji ameiambia SALEHJEMBE kwamba Simba wamefanya haraka kumsajili mchezaji ambaye ana mkataba na Yanga. “Okwi bado ni mchezaji wa Yanga, ana mkataba na Yanga lakini ana kesi na Yanga. “Simba wamekiuka sheria za Fifa kwa kumsajili mchezaji ambaye ana mkataba. Sisi tumemfungulia Okwi mashitaka akiwa bado mchezaji wetu na mkataba wetu naye haujaisha. “Sasa walishindwa hata kutuuliza kuliko kukurupuka hivi,” alihoji Manji. “Leo nitazungumza na waandishi, unaweza ukanisikiliza na kupata ninachosema lakini nakuhakikishia Simba wamekurupuka na wamevunja sheria na kanuni za Fifa kumsajili mchezaji mwenye mkataba na mtu mwingine. “Sikuona sababu ya wao kujiingiza matatizoni,” alisema Manji ambaye anazungumza na waandishi leo saa tano asubuhi kuhusiana na suala hilo la Okwi.

Posted via Blogaway

SAKATA LA OKWI; YANGA SC WATAKA SIMBA NA MCHEZAKJI MWENEYWE WOTE WAFUNGIWE, WAIPA TFF SIKU SABA KUCHUKUA HATUA, VINGINEVYO KESI FIFA HADI CAS…WATAKA FIDIA PIA YA SH MILIONI 900

Mambo yanazidi kupamba moto baada ya uongozi wa Yanga kusema ulipeleka jina la mshambuliaji Emmanuel Okwi katika majina yake ya wachezaji.
Yanga imesema ilipeleka jina hilo, hivyo inashangazwa kusikia Simba imemsajili na imeamua kuongeza adhabu ya kutaka afungiwe na ile faini kutoka dola 200,000 iongezeke nyingine ya dola 500,000.

Kama hiyo haitoshi, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar kwamba walituma barua ya kutaka kuvunja mkataba kwa TFF wakieleza nia yao.
“TFF haikuwa bado imejibu, Okwi akatuandikia sisi barua lakini sisi hatukiandika kwake. Ilipaswa naye apelike TFF.
“Simba pia wamefanya kosa, wanajua Okwi bado ana mkataba na Yanga, lakini wamekurupuka na kumsajili ambalo ni kosa kwa mujibu wa Fifa na Caf.
“Yanga tunajua bado suala la wachezaji wa kigeni liko wazi, dirisha halijafungwa. Ndiyo maana tulipeleka jina lake tukijua kama suala la kupunguza mchezaji mmoja litafika, tutalifanyia kazi.
“Simba na Okwi, wote wanapaswa kufungiwa kutokana na kukiuka vipengele hivi. Sisi tuliamini ni watu wa busara ambao wanakuja kuendeleza soka, lakini hizi ni vurugu ambazo hazijengi,” alisema Manji.
“Tunaamini suala letu TFF italishughulikia ndani ya siku saba, ikishindikana tukakwenda Caf, Fifa au Cas (mahakama ya soka).”

HAYA NDIYO INAYASISITIZA YANGA KWA OKWI:
1.   Tokea lakini laki 2 hadi laki 5, Simba pia inawahusu, wasingekubali, wangefuata utaratibu, wamemfuata mchezaji kabla ya kuanza na timu.
2.   Wataiomba TFF, ikiwezekana Okwi afungiwe kucheza moja kwa moja, pia Simba kwa kuwa wamemsajili akiwa bado na mkataba.
3.   Hawajavunja mkataba, barua aliyoiandikia Yanga, ilitakiwa aindikie TFF kwa kuwa yenye haikumuandikia yeye.
4.    Wametoa siku 7 kwa TFF kusikiliza na kutoa majibu ya kesi yao, la sivyo watalipeleka Caf, Fifa au Cas.


Posted via Blogaway

MANJI: TUTASAJILI WA KIGENI SITA OKWI NA JAJA WOTE NDANI

Na Samira Said, DAR ES SALAAM YANGA SC imesema itatuma majina ya wachezaji sita wa kigeni katika usajili wao kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, badala ya watano wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni. Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji amewaambia Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani kwamba, jina la mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Uganda litaongoza orodha hiyo. Mbali na Okwi, wachezaji wengine wa kigeni wa Yanga SC ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima kutoka Rwanda, Mganda Hamisi Kiiza na Wabrazil, Andrey Coutinho na Geilson Santana ‘Jaja’. Lakini Okwi, pia amesajiliwa na Simba SC, maana yake usajili ya Mganda huyo utazua tafrani mbele ya safari. Dirisha la usajili kwa wachezaji wazalendo linatarajiwa kufungwa leo, baada ya Shirikisho la SOka Tanzania (TFF) kuongea siku mbili zaidi tangu juzi. Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa aliimbia BIN ZUBEIRY jana kwamba, sababu za kusogeza mbele ni klabu zote za Ligi Kuu kushindwa kukamilisha usajili juzi. “Nadhani wameshindwa kuutumia huu mfumo wetu mpya wa elektroniki, sasa tumewapa Saa 48 zaidi warekebishe, zikiisha hizo, hapo hakuna nafasi tena, tunasonga mbele,”amesema Mwesigwa jana. Amesema kwamba hadi muda wa kufunga usajili juzi Saa 6:00 usiku, ni timu moja tu, Kimondo FC ya Daraja la Kwanza ndiyo iliyokuwa imefanikiwa kukamilisha usajili wake katika mfumo huo. “Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Kimondo kwa kumudu kuutumia mfumo huu na kuwasilisha usajili wao ndani ya muda,”amesema. Aidha, Mwesigwa amesema kwamba dirisha la usajili kwa wachezaji wa kigeni litafungwa Septemba 6, mwaka huu. “Hili dirisha la wachezaji wa kigeni likifungwa, hakuna nyongeza ya muda tena, kwa kuwa hili lipo katika mfumo wa kimataifa chini ya FIFA, likifungwa, limefungwa dunia nzima, hivyo nawasihi viongozi wa klabu wahakikishe hawafanyi makoasa,”amesema.

Posted via Blogaway

HII NDO SIKU AMBAYO MCHEZAJI DOMAYO ATALUDI RAMSI UWANJANI

DAKTARI wa Azam, Mwanandi Mwankenwa, amethibitisha kuwa kiungo Frank Domayo na Joseph Kimwaga wa Azam watarejea kwenye Ligi Kuu Bara mwanzoni mwa mwaka 2015. Mwankenwa amelieleza Mwanaspoti kuwa Domayo ambaye alisainiwa akitokea Yanga atakuwa fiti kucheza michezo ya ligi kuanzia Januari Mosi wakati Kimwaga atasubiri hadi Machi Mosi. Wachezaji hao wameanza mazoezi ya viungo kwenye hospitali ya ‘Sanitas Mikocheni Clinic’ iliyopo jijini Dar es Salaam. “Kutokana na utaratibu wa matibabu walioelekezwa na madaktari bingwa wa mifupa waliowatibu, Domayo ataruhusiwa rasmi kucheza mpira wa kishindani ifikapo Januari Mosi 2015, kwa upande wa Kimwaga atachukua muda zaidi ya miezi miwili mbele mpaka Machi,”alisema Daktari huyo. Kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu 2014/15, Domayo ataweza kucheza michezo yote ya ligi kuu mzunguko wa pili na hata ile ya mashindano ya kimataifa. Kimwaga naye atarudi uwanjani mwezi machi na kucheza michezo saba ya ligi ambayo ni dhidi ya Coastal, Yanga, Mtibwa, Kagera, Stand United, Simba na Mgambo JKT. Na mdadisiblog/festo saimon 0657035125

Posted via Blogaway

YANGA NI MUZIKI MNENE MSIMU HUU! NI SHEEEDAH

YANGA iliyokuwa kambini Zanzibar inarejea Dar es Salaam leo Alhamisi na inatarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza uwanjani wikiendi hii itakaposhuka kukipiga kwenye mchezo wa kirafiki ambao hata hivyo bado haujjathibitishwa. Vijana hao wa Jangwani hawajacheza mechi yoyote Dar es Salaam tangu kuanza maandalizi ya msimu mpya wala mashabiki mji huo hawajakiona kikosi kipya chini ya Mbrazili Marcio Maximo. Yanga ikiwa Zanzibar ilicheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Chipukizi ya Pemba, Shangani na KMKM za Unguja. Maximo licha ya kusisitiza kwamba hajajua ni timu gani atacheza nayo, alisema anatarajia kupanga kikosi kamili kitakachocheza dakika zote 90 na kama atafanya mabadiliko, yatakuwa madogomadogo ya kawaida na tofauti kabisa na alivyokuwa anafanya kwenye mechi zake za kirafiki alizocheza Zanzibar ambapo kila mchezaji alicheza dakika 45. “Mwanzo ulikuwa mgumu sana kwa wachezaji wangu kwani walikuwa na kazi ya kujifunza staili mpya za namna ninavyotaka wacheze, namna ya kumili mpira ninavyotaka, pasi za kueleweka kuchanganya na siyo kubutua bila mpango, kazi ambayo kwa sasa inakwenda vizuri.” Uchunguzi uliofanywa na Mwanaspoti kulingana na mazoezi yake na mechi za kirafiki ‘First Eleven’ ya Maximo ni hii; Kipa ni Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul beki ya kulia na kushoto ni Oscar Joshua lakini Edward Manyama na Amos Abeil anaocheza nao nafasi moja ni hatari, Maximo anaweza kubadilika kulingana na wapinzani wake na walizonazo wachezaji hao. Joshua anatumia nguvu na haogopi, Manyama anatumia akili, wakati Amos ana kasi.Mabeki wa kati ni Kelvin Yondani ‘Vidic’ na Nadir Haroub ‘Cannavaro’. Kiungo mkabaji ni Mnyarwanda Mbuyu Twite na kiungo mshambuliaji ni Hassan Dilunga. Panga pangua Mbrazili Andrey Coutinho atacheza winga ya kushoto na Mnyarwanda Haruna Niyonzima atacheza winga ya kulia, mastraika wa kati Mrisho Ngassa anayecheza kama kiungo nyuma ya Genilson Santos ‘Jaja’. Simon Msuva anaweza kucheza winga ya kulia kama anataka timu ishambulie kwa kasi, Jerry Tegete, Hamis Kiiza raia wa Uganda, Said Bahanuzi na Hussein Javu nao wanaweza kumpeleka Ngassa pembeni. Maximo atakuwa na mpango wa kucheza mpira wa kutulia. Mashabiki wa Wana Jangwani hao wanaisubiri kwa hamu timu hiyo ili kuona makali ya vifaa vipya. Source mwanaspoti

Posted via Blogaway

YANGA KUVUNJA UKIMYA KUHUSU OKWI LEO HII

Siku moja baada ya kujiunga na Simba huku akiwa bado na mkataba na Yanga, uongozi wa Yanga utatoa ufafanuzi kuhusiana na Emmanuel Okwi. Yanga itatoa ufafanuzi kuhusiana na Okwi kuamua kwenda Simba. Habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza uongozi wa klabu hiyo kongwe utatoa ufafanuzi kuhusiana na uamuzi wa kumsajili Okwi. Okwi ametua Simba ikiwa ni siku chache tu baada ya Yanga kuwasilisha barua TFF ikitaka afungiwe kutokana na kukiuka kanuni. Yanga pia iliomba ilipwe fidia ya dola 200,000 (Sh milioni 330). Kabla ya TFF haijajibu lolote kuhusiana na suala hilo, Okwi ametua Simba



Posted via Blogaway