| Na Samira Said, DAR ES SALAAM
YANGA SC imesema itatuma majina ya
wachezaji sita wa kigeni katika usajili wao kwa
ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
badala ya watano wanaotakiwa kwa mujibu wa
kanuni.
Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji
amewaambia Waandishi wa Habari leo makao
makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga
na Jangwani kwamba, jina la mshambuliaji
Emmanuel Okwi kutoka Uganda litaongoza
orodha hiyo.
Mbali na Okwi, wachezaji wengine wa kigeni
wa Yanga SC ni Mbuyu Twite, Haruna
Niyonzima kutoka Rwanda, Mganda Hamisi
Kiiza na Wabrazil, Andrey Coutinho na Geilson
Santana ‘Jaja’.
Lakini Okwi, pia amesajiliwa na Simba SC,
maana yake usajili ya Mganda huyo utazua
tafrani mbele ya safari.
Dirisha la usajili kwa wachezaji wazalendo
linatarajiwa kufungwa leo, baada ya Shirikisho
la SOka Tanzania (TFF) kuongea siku mbili
zaidi tangu juzi.
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa aliimbia
BIN ZUBEIRY jana kwamba, sababu za
kusogeza mbele ni klabu zote za Ligi Kuu
kushindwa kukamilisha usajili juzi.
“Nadhani wameshindwa kuutumia huu mfumo
wetu mpya wa elektroniki, sasa tumewapa Saa
48 zaidi warekebishe, zikiisha hizo, hapo
hakuna nafasi tena, tunasonga
mbele,”amesema Mwesigwa jana.
Amesema kwamba hadi muda wa kufunga
usajili juzi Saa 6:00 usiku, ni timu moja tu,
Kimondo FC ya Daraja la Kwanza ndiyo
iliyokuwa imefanikiwa kukamilisha usajili wake
katika mfumo huo. “Napenda kuchukua fursa
hii kuwapongeza Kimondo kwa kumudu
kuutumia mfumo huu na kuwasilisha usajili
wao ndani ya muda,”amesema.
Aidha, Mwesigwa amesema kwamba dirisha la
usajili kwa wachezaji wa kigeni litafungwa
Septemba 6, mwaka huu. “Hili dirisha la
wachezaji wa kigeni likifungwa, hakuna
nyongeza ya muda tena, kwa kuwa hili lipo
katika mfumo wa kimataifa chini ya FIFA,
likifungwa, limefungwa dunia nzima, hivyo
nawasihi viongozi wa klabu wahakikishe
hawafanyi makoasa,”amesema. |
0 comments:
Post a Comment