Saturday, August 30, 2014
 |
| Siku moja baada ya Angel Di Maria
kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa klabu
ya Manchester United ya England huku
akikabidhiwa jezi yenye historia kubwa ndani
ya klabu hiyo (namba 7), mwanasoka bora wa
ulaya na mchezaji wa zamani wa United,
Cristiano Ronaldo amezungumza juu ya Di
Maria kwenda Old Trafford pamoja na kupewa
jezi namba 7.
Ronaldo ambaye aliondoka Man United
mnamo mwaka 2009 kwa ada ya uhamisho
ambayo iliweka rekodi ya £80m amesema
hana wasiwasi wa Di Maria kufanikiwa ndani
ya United.
“Uhamisho huu ni kitu kizuri kwake.” Ronaldo
aliwaambia waandishi wa habari jana jijini
Monaco.
“Manchester [United] ni moja ya klabu kubwa
duniani, ni sehemu nzuri kwa Di Maria na
namtakia kheri na mafanikio, Di Maria ni
mchezaji mzuri sana, anastahili kuichezea
United.”
Alipoulizwa juu ya Di Maria kupewa jezi
namba 7 aliyokuwa akivaa alipokuwa Man
United, Ronaldo alisema: “Nilimwambia, ‘jezi
No.7 ina maana kubwa ndani ya United, lakini
nadhani ataweza kubeba uzito wa jezi kwa
sababu ni mchezaji mzuri sana.”
Di Maria anaweza kuanza kuichezea Man U
kesho kwenye mchezo dhidi ya Burnley.b |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment