Saturday, August 30, 2014

Hiki ndio kinachomfanya Marcos Rojo asianze kuichezea Man United

Imepita zaidi ya wiki moja tangu klabu ya Manchester United ilipokamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Argentina Marcos Rojo kutoka klabu ya Sporting Lisbon – lakini cha ajabu mchezaji huyo amekuwa haonekani kwenye mechi za United. Leo hii imefahamika kwamba mchezaji huyo bado hajapata kibali cha kumuwezesha kufanya kazi nchinin UK – kitu kinachomfanya timu yake ishindwe kupata idhini ya premier league kumchezesha mchezaji huyo. Mwanzoni kulikuwa wasiwasi kwamba utata wa kisheria uliopo kati ya klabu yake ya zamani Sporting dhidi ya kampuni ya Doyen Sports ambayo ilikuwa inamiliki asilimia 75 ya haki zake za usajili. Lakini leo hii kocha wa Man united Louis van gaal amethibitisha mchezaji huyo amekwama kutokana na kibali cha kazi na sasa yupo nchini Hispania ambapo ndio kuna ubalozi wa Argentina akifuatilia kibali hicho. Hata hivyo Van Gaal amesema suala hilo sasa halitachukua muda mrefu, pia akathibitisha kwamba Angel Dimaria anaweza kuanza kesho kwenye mchezo dhidi ya Burnley.

Posted via Blogaway

0 comments:

Post a Comment