Saturday, August 30, 2014
 |
| Wakati wa utambulisho rasmi wa Angel Di
Maria jana, kocha qa man United Louis Van
Gaal alithibitishqa kwamba kuna kundi la
wachezaji litaondoka mpaka kufikia mwishoni
mwa wiki hii.
Leo hii zimetoka taarifa kwamba kiungo wa
kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa ni mmoja
wa wachezaji wanaondoka kwenye klabu hiyo
kabla ya kuisha kwa dirisha la usajili.
Shinji anatarajiwa kujiunga na klabu yake ya
zamani ya Borrusia Dortmund kwa ada ya
uhamisho wa £8m.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Ujerumani
leo hii tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya
ili kukamilisha usajili wake Dortmund.
Kagawa alijiunga na Man United miaka mitatu
iliyopita kwa ada ya uhamisho wa £12m. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment