Saturday, August 30, 2014
 |
| Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf
Manji, leo ametoa kali
kwenye kikao chake na
waandishi wa habari
aliposema kwamba ana uwezo
wa kuwanuanua wachezaji wa
Simba, halafu wasicheze
ligi na badala yake wawe
wanafanya mazoezi Covo
Beach tu.
Manji amesema hayo wakati
akipinga Simba kutangaza
kumsajili mshambuliaji
Emmanuel Okwi.
Manji amesema suala hilo ni
sawa na uhuni kwa kuwa
Simba inajua Okwi ana
mkataba na Yanga.
“Kama itakuwa ni kufanya
mambo kwa staili ya kihuni,
hata mimi ninaweza kuamua
kuwanunua wachezaji wa
Simba sijui kina (Amissi)
Tambwe na wenzake, halafu
wawe wanafanya mazoezi Coco
Beach tu, wasicheze ligi.
“Lakini busara ni jambo
jema, lakini nione kwamba
ninachofanya ni kitu gani
na hasara zake ni zipi.
“Umesikia sisi (Yanga)
tumelalamika kuhusiana na
usajili wa Domayo au
Kavumbagu kwenda Azam FC.
Kila kitu kilikwenda kwa
utaratibu.
“Hata Simba wanaosema
kuhusiana na suala la Okwi
pia hawajui, sisi
hatukuzozana na Simba,
utaona Okwi wakati anakuja
Yanga tulifuata utaratibu
na kumalizana na SC Villa.
“Simba hawakuwa na tatizo
na Okwi, badala yake Etoile
du Sahel ya Tunisia ambayo
Yanga hatukufanya nao
biashara. Hakukuwa na
sehemu ambayo
inatugonganisha,” alisema.
“Sasa kama kuna lengo la
kufanya ili kuikomoa au
kuona ni kulipa kisasi,
basi ni kujidanganya tu na
kutaka kufanya mambo yaende
kwa kukomoana ambalo si
jambo zuri.
“Ndiyo maana tumetoa siku
saba tuwaachie TFF
washughulikie madai yetu,
ikishindikana, Caf, Fifa au
Cas bado ni sehemu
tunazoweza kwenda,”
alisisitiza Manji.
“Pia kusema Okwi amevunja
mkataba nasi ni
kujidanganya. Iko wapi
barua aliyonayo yeye kwamba
tumevunja naye mkataba.
“Hata majina tumetuma sita,
tungejua lipi la kulitoa
kwa kuwa hadi Septemba 6
ndiyo mwisho wa kusajili
wageni. Haraka ya nini |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment