| YANGA iliyokuwa kambini Zanzibar inarejea Dar
es Salaam leo Alhamisi na inatarajiwa
kuonekana kwa mara ya kwanza uwanjani
wikiendi hii itakaposhuka kukipiga kwenye
mchezo wa kirafiki ambao hata hivyo bado
haujjathibitishwa.
Vijana hao wa Jangwani hawajacheza mechi
yoyote Dar es Salaam tangu kuanza maandalizi
ya msimu mpya wala mashabiki mji huo
hawajakiona kikosi kipya chini ya Mbrazili
Marcio Maximo.
Yanga ikiwa Zanzibar ilicheza mechi tatu za
kirafiki dhidi ya Chipukizi ya Pemba, Shangani
na KMKM za Unguja.
Maximo licha ya kusisitiza kwamba hajajua ni
timu gani atacheza nayo, alisema anatarajia
kupanga kikosi kamili kitakachocheza dakika
zote 90 na kama atafanya mabadiliko, yatakuwa
madogomadogo ya kawaida na tofauti kabisa
na alivyokuwa anafanya kwenye mechi zake za
kirafiki alizocheza Zanzibar ambapo kila
mchezaji alicheza dakika 45.
“Mwanzo ulikuwa mgumu sana kwa wachezaji
wangu kwani walikuwa na kazi ya kujifunza
staili mpya za namna ninavyotaka wacheze,
namna ya kumili mpira ninavyotaka, pasi za
kueleweka kuchanganya na siyo kubutua bila
mpango, kazi ambayo kwa sasa inakwenda
vizuri.”
Uchunguzi uliofanywa na Mwanaspoti kulingana
na mazoezi yake na mechi za kirafiki ‘First
Eleven’ ya Maximo ni hii; Kipa ni Deogratius
Munishi ‘Dida’, Juma Abdul beki ya kulia na
kushoto ni Oscar Joshua lakini Edward
Manyama na Amos Abeil anaocheza nao nafasi
moja ni hatari, Maximo anaweza kubadilika
kulingana na wapinzani wake na walizonazo
wachezaji hao.
Joshua anatumia nguvu na haogopi, Manyama
anatumia akili, wakati Amos ana kasi.Mabeki wa
kati ni Kelvin Yondani ‘Vidic’ na Nadir Haroub
‘Cannavaro’.
Kiungo mkabaji ni Mnyarwanda Mbuyu Twite
na kiungo mshambuliaji ni Hassan Dilunga.
Panga pangua Mbrazili Andrey Coutinho
atacheza winga ya kushoto na Mnyarwanda
Haruna Niyonzima atacheza winga ya kulia,
mastraika wa kati Mrisho Ngassa anayecheza
kama kiungo nyuma ya Genilson Santos ‘Jaja’.
Simon Msuva anaweza kucheza winga ya kulia
kama anataka timu ishambulie kwa kasi, Jerry
Tegete, Hamis Kiiza raia wa Uganda, Said
Bahanuzi na Hussein Javu nao wanaweza
kumpeleka Ngassa pembeni.
Maximo atakuwa na mpango wa kucheza mpira
wa kutulia.
Mashabiki wa Wana Jangwani hao wanaisubiri
kwa hamu timu hiyo ili kuona makali ya vifaa
vipya. Source mwanaspoti |
0 comments:
Post a Comment