Saturday, August 30, 2014
 |
| Kiungo wa kimataifa wa Spain Xabi Alonso
amejiunga na klabu ya FC Bayern Munich ya
Ujerumani akitokea kwa mabingwa wa ulaya
Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi
millioni 5.
Alonso ambaye alijunga na Real Madrid
akitokea Liverpool ametambulishwa rasmi leo
hii kwenye mkutano waandishi wa habari na
kutoa sababu ambayo imemfanya mpaka
akaamua kuondoka Santiago Bernabeu.
Kiungo huyo ambaye juzi alitangaza kujiuzulu
kuichezea timu ya taifa ya Hispania amesema
kwamba kilichomfanya kuhama Madrid sio
upinzani wa namba kama inavyodhaniwa na
wengi.
“Klabu haikutaka niondoke, ulikuwa uamuzi
wangu mwenyewe kuondoka. Baada ya
kushinda La Decima, nilihisi nahitaji
changamoto mpya. Nilihisi muda wa kuondoka
umefika,” Alonso aliwaambia waandishi wa
habari.
“Sikuamua kuondoka kwa sababu ya ujio wa
Toni Kroos. Madrid wamefanya usajili mzuri
sana na tungecheza wote kwa muda mwingi.
Hivyo sikuondoka kwa sababu yake, nilihitaji
tu changamoto mpya.
“Bayern ndio lilikuwa chaguo sahih kwangu
mimi.” – Alonso |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment