Tuesday, August 26, 2014

BALOTELLI ALIVYOSHUHUDIA LIVERPOOL YAKE IKITESWA NA TIMU YAKE YA ZAMANI USIKU HUU ETIHAD

Vijana wapya: Mshambuliaji mpya wa Liverpool, Mtaliano Mario Balotelli akiwa na mchezaji mwingine mpya wa klabu hiyo, Adam Lallana jukwaani Uwanja wa Etihad wakati wa mechi dhidi ya wenyeji, Manchester City. Mwingine chini mbele ni gwiji wa klabu, Kenny Dalglish. Man City imeshinda 3-1.

HIKI NDO KITU KINACHOKWAMISHA BEKI MPYA KUANZA KAZI MAN UNITED

BEKI mpya wa Manchester United, Marcos Rojo hajacheza mechi yoyote kutokana na kwamba bado hajapata kibali cha kufanyia kazi nchini Uingereza. Louis van Gaal alitarajia kumtumia Rojo katika mchezo waliomaliza kwa safe ya kufungana bao 1-1 na Sunderland Jumapili, lakini sasa atamsikilizia katika mchezo wa genii dhidi ya Burnley Jumamosi. Beki huyo mwenye umri wa miaka 24, amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 16 Man United wiki iliyopita, lakini atalazimika kusubiri hadi patine kibali cha kufanyia kazi. Rojo anaingia kwenye orodha ndefu ya wachezaji wanaokosekana uwanjani kwa sasa United, wengine wakiwa ni Luke Shaw, Michael Carrick, Marouane Fellaini, Jesse Lingard, Rafael da Silva na Ander Herrera ambao wote ni majeruhi. Van Gaal anatarajiwa kuendelea kuwapa nafasi wachezaji chipukizi usiku wa Jumanne kama Michael Keane na Tyler Blackett katika kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo.

YANGA YAINGIZA MILIONI 7 ZANZIBAR, SIMBA MILIONI 3

Yanga imeingiza mapato mengi zaidi katika mechi yake ya kirafiki dhidi ya Shangani iliyopigwa jana kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa. Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Yanga kushinda kwa mabao 2-0, mapato yaliyopatikana ni Sh milioni 7 na ushee. Lakini wapinzani wake Simba wameingiza Sh milioni 3 tu katika mechi yao ya kirafiki iliyopigwa jana hiyo na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kilimani. Yanga ndiyo ilianza kucheza halafu mashabiki wote wakatolewa nje na kuanza kuingia upya kushuhudia mechi ya pili ambayo ilikuwa ya Simba. Ingawa mapato hayo yamekuwa yakifanywa siri kubwa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), lakini SALEHJEMBE limeng’amua kila kitu kuwa Yanga wameingiza mapato mengi zaidi. Kiingilio katika mechi hizo ilikuwa ni Sh 2,000 na 5,000.credit salehjembe

TIMU ZA ENGLAND ZAENDELEZA KUFANYA USAJILI WAO WA NGUVU,NA HII NDO TIMU AMBAYO ETOO ANATUA LEO HII

Samuel Eto’o anatarajia kutua leo hii na kufanya vipimo kabla ya kumalizia usajili wake na Everton. Imeelezwa mazungumzo na kila kitu kimeshakamilika ili Eto’o atue Everton. Lakini taarifa nyingine zimeeleza, Everton imemtaka Eto’o kupunguza kiwango cha mshara. Mshahara wake akiwa Chelsea msimu uliopita ulikuwa ni pauni 130,000 kwa wiki.

SOMA KISA CHA BALOTELLI KUENDELEA KUITUMIA JEZI NAMBA 45 HATA BAADA YA KUTUA LIVERPOOL

mshambuliaji Mario Balotelli ameamua kuchukua jezi kipenzi chake namba 45 ambayo ataitumia akiwa na Liverpool. Balotelli amekuwa akiitumia namba 45 tokea akiwa Inter Milan, baadaye akajiunga na Man City na hata alipokwenda AC Milan. Jezi hiyo anaamini ndiyo yenye bahati kwa kuwa wakati akiwa kinda anaichezea Inter Milan, alifunga mabao manne katika mechi nne. Katika kikosi cha AC Milan, vijana waliochaguliwa kuchezea timu ya wakubwa huvaa jezi kuanzia namba 36 hadi 45. Kingine Balotelli ambaye leo alishuhudia mechi kati ya Man City dhidi ya timu yake mpya ya Liverpool akiwa jukwaani Ambapo man city ilishinda 3-1, a amekuwa akitania 4+5=9 akiwa ana maana anavaa jezi namba 9, kijanja.

ANGEL DI MARIA AWASILI MAN UNITED KUKAMILISHA USAJILI WA REKODI ENGLAND NA MSHAHARA MNONO

KIUNGO Angel di Maria amewasili viwanja vya mazoezi vya Manchester United, Carrington kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wa Pauni 60 kutoka Real Madrid ya Hispania. Nyota huyo wa Argentina aliyeng'ara kwenye Kombe a Dunia amewasili England huku viongozi wa Old Trafford wakiendelea na mazungumzo na Real Madrid juu ya kukamilisha uhamisho wa dau la rekodi Uingereza. Di Maria, mwenye umri wa miaka 26, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake usiku huu ambao utamfanya alipwe Pauni 200,000 kwa wiki kwa zaidi ya miaka mitano, mshahara ambao pia utamfanya awe mchezaji wa pili kulipwa zaidi katika klabu hiyo baada ya Nahodha, Wayne Rooney. Amenaswa: Di Maria akiwa kiri nyuma kushoto kwenye gari kuelekea viwanja vya mazoezi vya United Di Maria anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake usiku huu Uhamisho wote utaigharimu United zaidi ya Pauni Milioni 90 na mchezaji huyo ataingia moja kwa moja katika kikosi kilichojeruhiwa cha Louis van Gaal kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu iliyopanda Ligi Kuu, Burnley.

Epl: Matokeo na wafungaji wa mechi ya Liverpool vs Man City haya hapa

MABINGWA wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wamewachapa mabao 3-1 wapinzani wao katika mbio za taji hilo msimu uliopita, Liverpool usiku huu Uwanja wa Etihad mjini Manchester. Stevan Jovetic alifunga mabao mawili moja kila kipindi la kwanza dakika ya 41 na pili dakika ya 55 kabla ya Edin Dzeko kuingia na kufunga la tatu katika mpira wa kwanza aliogusa dakika ya 68. Dzeko alifunga bao hilo kabla hata Sergio Aguero aliuemposha hajafika kwenye benchi na Liverpool wakapata bao la kufutia machozi dakika ya 83 kupitia kwa Lambert. Mshambuliaji mpya wa Liverpool, Mario Balotelli alikuwa jukwaani akiishuhudia timu yake ya zamani ikishinda. Kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Nasri, Toure, Fernando, Silva/Jesus Navas DK65, Jovetic/ Fernandinho DK80 na Dzeko/Aguero dk69. Liverpool: Mignolet, Johnson, Skrtel, Lovren, Moreno, Henderson, Gerrard, Allen/Can dk75, Sterling/Lambert dk79, Sturridge na Coutinho/ Markovic dk60.

Monday, August 25, 2014

BALOTELLI ASAINI MIAKA MITATU LIVERPOOL, MSHAHARA MNONO NA JEZI NAMBA 45, AANZA KAZI LEO DHIDI YA MAN CITY

MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan kutua Liverpool kwa Mkataba wa miaka mitatau. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliwasili Melwood leo mchana kukamilisha uhamisho wake kabla ya kwenda kufanya mazoezi maalum na mkuu wa idara ya kuwaweka fiti wachezaji, Ryland Morgans. Nyota huyo wa zamani wa Manchester City atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 125,000 kwa wiki Anfield na atakuwepo kwenye mchezo dhidi ya timu yake hiyo ya zamani usiku wa leo. Pamoja na kusaini mkataba wa miaka mitatu, Balotelli anaweza kuongezewa mwaka mmoja kwa mujibu wa kandarasi hiyo.

Wachezaji bora wa Dunia wanne wacheza Tanzania wajue hapa

TANZANIA haijawahi kushiriki fainali za Kombe la Dunia hata kwa mwaliko maalumu katika historia ya miaka 34 ya michuano hiyo, lakini imeweka historia ya kuwaleta nchini wachezaji wanne waliowahi kutwaa tuzo za Mchezaji Bora wa Dunia wa Fifa. Juzi Jumamosi kikosi cha wakongwe wa Real Madrid kilicheza na wakongwe wa Tanzania na kuwafunga mabao 3-1, lakini ujio huo uliandika historia kwa Tanzania kwa kuwaweka uwanjani wachezaji Luis Figo na Fabio Cannavaro waliowahi kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia. Wachezaji wengine waliowahi kuja Tanzania wenye rekodi hiyo kubwa duniani ni Ricardo Kaka wa Brazili na Geogre Weah wa Liberia. Figo ambaye licha ya kustaafu soka miaka mingi iliyopita, juzi alicheza kwa kiwango cha juu na kuwa kivutio kwa Watanzania waliiofurika uwanjani. Mreno huyo alinyakua tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia mwaka 2000. Cannavaro alinyakuwa tuzo hiyo mwaka 2006 wakati Kaka alinyakua mwaka 2007. Mliberia Weah ambaye ndiye Mwafrika wa kwanza kupata heshima hiyo, alinyakua tuzo hiyo maarufu kwa jina la Ballon d’Or mwaka 1995. Weah alikuja Tanzania mwaka 1994 akiwa na kikosi cha Liberia. Kaka alikwemo kwenye kikosi cha Brazili kilichoifunga Tanzania mabao 5-1 mwaka 2010. Kati ya wana tuzo hao, ni Weah na Kaka pekee ndiyo waliokuja nchini wakiwa bado wanacheza soka la kulipwa na la kimataifa. Ujio wa Figo na Cannavaro umekuja wakiwa tayari wametundika daluga (wamestaafu). Credit mwanaspoti

BAADA YA KIPIGO KIMOJA NA DROO MOJA KOCHA VAN GAAL AFUNGUKA MAZITO

KOCHA Mkuu wa Manchester United, Louis van Gaal amesema itakuwa ni muujiza mkubwa kwa timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu. Mdachi huyo ameilinganisha United ya sasa na Bayern Munich ya mwaka 2009 wakati alipokuwa akiinoa timu hiyo iliyokuwa na kikosi kilichokuwa na kasoro nyingi. Hata hivyo, Van Gaal akamaliza ligi msimu huo kwa kunyakua Ubingwa wa Bundesliga, kitu ambacho haoni kama kitaweza kujirudia kwa sasa akiwa na cha United. Wasiwasi wa Van Gaal umeibuka baada ya wiki iliyopita kuchapwa na Swansea City nyumbani Old Trafford katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu England na kikosi chake jana Jumapili kilitarajia kumenyana na Sunderland kwenye ligi hiyo. Alipoulizwa kama aanze kutazamwa kiwango chake kwenye msimu wa kwanza au wa pili klabuni hapo, Van Gaal alijibu: “Siku zote hiyo ndiyo inakuwa kesi kubwa. Kitu ambacho kimenipa uzoefu ni kwamba nilikuwa bingwa Barcelona na Bayern, hivyo inawekana ila ni ngumu sana. “Nilipokwenda Bayern Munich kikosi kilikuwa hovyo. Kitu ambacho tulikifanya hadi mwisho wa msimu kilikuwa ni muujiza. Hapa Man United pia kikosi hakijatengemaa. Kuna namba 9 watano na namba 10 sita. Hatuna mabeki.” Alipoulizwa kama itakuwa muujiza kwa United kutwaa taji la Ligi Kuu England msimu huu, Van Gaal alisema: “Ndiyo, nadhani ni hivyo. Sawa siku zote inawezekana, lakini itakuwa ngumu sana.” credit mwanaspoti