MABINGWA wa Ligi Kuu ya England,
Manchester City wamewachapa mabao 3-1
wapinzani wao katika mbio za taji hilo msimu
uliopita, Liverpool usiku huu Uwanja wa
Etihad mjini Manchester.
Stevan Jovetic alifunga mabao mawili moja
kila kipindi la kwanza dakika ya 41 na pili
dakika ya 55 kabla ya Edin Dzeko kuingia na
kufunga la tatu katika mpira wa kwanza
aliogusa dakika ya 68.
Dzeko alifunga bao hilo kabla hata Sergio
Aguero aliuemposha hajafika kwenye benchi
na Liverpool wakapata bao la kufutia machozi
dakika ya 83 kupitia kwa Lambert.
Mshambuliaji mpya wa Liverpool, Mario
Balotelli alikuwa jukwaani akiishuhudia timu
yake ya zamani ikishinda.
Kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta,
Kompany, Demichelis, Clichy, Nasri, Toure,
Fernando, Silva/Jesus Navas DK65, Jovetic/
Fernandinho DK80 na Dzeko/Aguero dk69.
Liverpool: Mignolet, Johnson, Skrtel, Lovren,
Moreno, Henderson, Gerrard, Allen/Can dk75,
Sterling/Lambert dk79, Sturridge na Coutinho/
Markovic dk60. |
0 comments:
Post a Comment