Yanga imeingiza mapato
mengi zaidi katika mechi
yake ya kirafiki dhidi ya
Shangani iliyopigwa jana
kwenye Uwanja wa Amaan
mjini hapa.
Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Yanga
kushinda kwa mabao 2-0, mapato
yaliyopatikana ni Sh milioni 7 na ushee.
Lakini wapinzani wake Simba
wameingiza Sh milioni 3 tu
katika mechi yao ya
kirafiki iliyopigwa jana
hiyo na kuibuka na ushindi
wa mabao 2-1 dhidi ya
Kilimani.
Yanga ndiyo ilianza kucheza
halafu mashabiki wote
wakatolewa nje na kuanza
kuingia upya kushuhudia
mechi ya pili ambayo
ilikuwa ya Simba.
Ingawa mapato hayo yamekuwa
yakifanywa siri kubwa na
Chama cha Soka Zanzibar
(ZFA), lakini SALEHJEMBE
limeng’amua kila kitu kuwa
Yanga wameingiza mapato
mengi zaidi.
Kiingilio katika mechi hizo
ilikuwa ni Sh 2,000 na
5,000.credit salehjembe |
0 comments:
Post a Comment