KOCHA Mkuu wa Manchester
United, Louis van Gaal amesema
itakuwa ni muujiza mkubwa kwa
timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi
Kuu England msimu huu.
Mdachi huyo ameilinganisha
United ya sasa na Bayern Munich
ya mwaka 2009 wakati alipokuwa
akiinoa timu hiyo iliyokuwa na
kikosi kilichokuwa na kasoro
nyingi.
Hata hivyo, Van Gaal akamaliza ligi
msimu huo kwa kunyakua
Ubingwa wa Bundesliga, kitu
ambacho haoni kama kitaweza
kujirudia kwa sasa akiwa na cha
United.
Wasiwasi wa Van Gaal umeibuka
baada ya wiki iliyopita kuchapwa
na Swansea City nyumbani Old
Trafford katika mchezo wao wa
kwanza wa Ligi Kuu England na
kikosi chake jana Jumapili
kilitarajia kumenyana na
Sunderland kwenye ligi hiyo.
Alipoulizwa kama aanze
kutazamwa kiwango chake kwenye
msimu wa kwanza au wa pili
klabuni hapo, Van Gaal alijibu:
“Siku zote hiyo ndiyo inakuwa kesi
kubwa. Kitu ambacho kimenipa
uzoefu ni kwamba nilikuwa bingwa
Barcelona na Bayern, hivyo
inawekana ila ni ngumu sana.
“Nilipokwenda Bayern Munich
kikosi kilikuwa hovyo. Kitu
ambacho tulikifanya hadi mwisho
wa msimu kilikuwa ni muujiza.
Hapa Man United pia kikosi
hakijatengemaa. Kuna namba 9
watano na namba 10 sita. Hatuna
mabeki.”
Alipoulizwa kama itakuwa muujiza
kwa United kutwaa taji la Ligi Kuu
England msimu huu, Van Gaal
alisema: “Ndiyo, nadhani ni hivyo.
Sawa siku zote inawezekana, lakini
itakuwa ngumu sana.” credit mwanaspoti |
0 comments:
Post a Comment