TANZANIA haijawahi kushiriki
fainali za Kombe la Dunia hata kwa
mwaliko maalumu katika historia
ya miaka 34 ya michuano hiyo,
lakini imeweka historia ya
kuwaleta nchini wachezaji wanne
waliowahi kutwaa tuzo za Mchezaji
Bora wa Dunia wa Fifa.
Juzi Jumamosi kikosi cha
wakongwe wa Real Madrid
kilicheza na wakongwe wa
Tanzania na kuwafunga mabao
3-1, lakini ujio huo uliandika
historia kwa Tanzania kwa
kuwaweka uwanjani wachezaji Luis
Figo na Fabio Cannavaro waliowahi
kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa
Dunia.
Wachezaji wengine waliowahi kuja
Tanzania wenye rekodi hiyo kubwa
duniani ni Ricardo Kaka wa Brazili
na Geogre Weah wa Liberia.
Figo ambaye licha ya kustaafu soka
miaka mingi iliyopita, juzi alicheza
kwa kiwango cha juu na kuwa
kivutio kwa Watanzania
waliiofurika uwanjani.
Mreno huyo alinyakua tuzo ya
Mchezaji Bora wa Dunia mwaka
2000.
Cannavaro alinyakuwa tuzo hiyo
mwaka 2006 wakati Kaka alinyakua
mwaka 2007.
Mliberia Weah ambaye ndiye
Mwafrika wa kwanza kupata
heshima hiyo, alinyakua tuzo hiyo
maarufu kwa jina la Ballon d’Or
mwaka 1995. Weah alikuja
Tanzania mwaka 1994 akiwa na
kikosi cha Liberia.
Kaka alikwemo kwenye kikosi cha
Brazili kilichoifunga Tanzania
mabao 5-1 mwaka 2010.
Kati ya wana tuzo hao, ni Weah na
Kaka pekee ndiyo waliokuja nchini
wakiwa bado wanacheza soka la
kulipwa na la kimataifa.
Ujio wa Figo na Cannavaro
umekuja wakiwa tayari
wametundika daluga
(wamestaafu). Credit mwanaspoti |
0 comments:
Post a Comment