MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amekamilisha
uhamisho wa Pauni Milioni 16 kutoka AC
Milan kutua Liverpool kwa Mkataba wa miaka
mitatau.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24
aliwasili Melwood leo mchana kukamilisha
uhamisho wake kabla ya kwenda kufanya
mazoezi maalum na mkuu wa idara ya
kuwaweka fiti wachezaji, Ryland Morgans.
Nyota huyo wa zamani wa Manchester City
atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 125,000
kwa wiki Anfield na atakuwepo kwenye mchezo
dhidi ya timu yake hiyo ya zamani usiku wa
leo. Pamoja na kusaini mkataba wa miaka
mitatu, Balotelli anaweza kuongezewa mwaka
mmoja kwa mujibu wa kandarasi hiyo. |
0 comments:
Post a Comment