Monday, October 20, 2014

UONGOZI MZIMA WA MDADISIBLOG UNAMTAKIA HAPPY BIRTHDAY MR BOB MAU

happy birhday my super frend Mr Bob Mau kwa kutimiza miaka kadhaa

MASTAA WOTE WABONGO KWANINI MSIIGE MFANO WA HUYU

Kutoka nianze kufuatilia akaunt mbalimbali za masuper staa wabongo sijawahi kumwona staa yeyoyte anayemsifia mpenzi wake au hata mume au mke zaidi ya floramvungi . Naomba mastaa wengine waige mfano wa huyu dada

BAADA YA VIPIGO MFULULIZO NDANDA FC YAAMUA KUFANYA FUKUZA FUKUZA

UGENINI SHINYANGA. Ndanda FC imemfuta kazi kocha wake, Denis Kitambi. Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa ndanda zinaeleza kuwa, uongozi wa klabu hiyo umechukua uamuzi huo baada ya vipigo viwili dhidi ya Mtibwa Sugar na kile cha nyumbani jana dhidi ya Ruvu Shooting. Taarifa nyingine zimeeleza kuwa Kocha wa Makipa, Mohammed Mwarami 'Shilton' naye ametimuliwa pia. Imeelezwa kumekuwa na kikao cha dharura leo asubuhi na viongozi wamefikia uamuzi huo. Juhudi za kuwapata viongozi wa Ndanda FC zimekuwa zikikwama kutokana na viongozi hao kutopokea simu. Lakini mchezaji mmoja wa Ndanda FC amelithibitisha hilo. “Tumeambiwa kuwa wamemtimua kocha, ila bado viongozi hawajafika kutueleza,” alisema.

HII NI KWA MASHABIKI WA CHELSEA! HIKI NDO KITU KINACHOENDELEA KUHUSU DIEGO COSTA

MSHAMBULIAJI Diego Costa ataukosa mchezo wa Jumanne wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, timu yake Chelsea ikimenyana na NK Maribor Uwanja wa Stamford Bridge, amesema kocha Jose Mourinho. Costa alikuwa nje ya kikosi cha Chelsea jana kikishinda 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika Ligi Kuu ya England na ataendelea kupata tiba kwa muda. Mpachika mabao huyo wa zamani wa Atletico Madrid aliumia akiichezea timu yake ya taifa Hispania na Mourinho amesikitishwa mno na kumkosa nyota wake huyo mkali wa mabao. Diego Costa atakosekana Chelsea ikicheza Ligi ya Mabingwa Ulaya keshokutwa "Baada ya mechi na Arsenal akaenda timu ya taifa, akacheza mechi mbili kubwa na amerudi akiwa na hali ambayo hawezi kucheza,"amesema Mourinho. "Nafikiri atakuwa katika hali nzuri katikati ya Novemba kurejea katika timu ya taifa. Tutakuwa makini mno juu yake. Atacheza kwangu atakapokuwa huru baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa,"amesema.

BAADA YA SARE YAO, HIKI NDICHO KILICHO MBELE YAO SIMBA NA YANGA, MWAKA HUU KAZI IPO!

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MIAMBA ya soka Tanzania, Simba na Yanga iligawana pointi Jumamosi baada ya sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sare hiyo inaifanya Simba SC itimize pointi nne baada ya awali kutoa sare tatu pia, wakati Yanga SC inafikisha pointi saba baada ya mechi nne, ikiwa nyuma ya Azam FC na Mtibwa Sugar zenye pointi 10 kila moja kileleni mwa Ligi.
Pamoja na kushinda 2-1 mara mbili dhidi ya Prisons na JKT Ruvu, lakini Yanga SC ilikutana na upinzani mkali na matokeo yangeweza kuwa kinyume kama si bahati yao.

RATIBA RAUNDI MBILI ZIJAZO LIGI KJUU BARA
Oktoba 25, 2014
Stand United Vs Yanga SC
Ndanda FC Vs Mgambo JKT
Kagera Sugar Vs Coastal Union
Azam Fc Vs  JKT Ruvu
Prisons Vs Simba SC
Ruvu Shoot Vs Polisi Moro
Oktoba 26, 2014
Mbeya City Vs Mtibwa Sugar
Novemba 1, 2014
Kagera Sugar Vs Yanga SC
Coastal Union  Vs Ruvu Shooting
JKT Ruvu Vs Polisi Morogoro
Ndanda FC Vs Azam FC
Stand United Vs Prisons
Mtibwa Sugar Vs Simba SC
Novemba 2, 2014
Mgambo JKT Vs Mbeya City
Yanga SC sasa watasafiri hadi Shinyanga kuwafuata Stand United waliopanda Ligi Kuu msimu huu, mchezo utakaofanyika Jumamosi Uwanja wa Kambarage.
Stand imeonyesha ni timu imara ikifanikiwa kuvuna pointi tano katika mechi za ugenini, kutokana na sare mbili dhidi ya Simba SC na Kagera Sugar na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Mgambo.
Stand ilipoteza mchezo wa kwanza nyumbani kwa kufungwa 4-1 na Ndanda FC ya Mtwara iliyopanda pia Ligi Kuu msimu huu, lakini baada ya hapo imecheza mechi tatu ugenini bila kufungwa.
Pata picha Yanga SC wanakwenda kukutana na upinzani wa aina gani katika mchezo huo Jumamosi.
Simba SC sasa. Watacheza na Prisons ya Mbeya Jumamosi Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Prisons ilionyesha upinzani ikifungwa na Yanga SC 2-1 na pia ilishinda ugenini 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya kutoa sare ya 0-0 na Azam FC Mbeya.
Jana, Prisons wamefungwa 2-1 na JKT Ruvu Mbeya na baada ya mchezo huo, kocha Juma Mwambusi akasema amekubali matokeo na anaelekeza nguvu zake katika mchezo ujao.
Simba SC ambayo haijashinda mechi msimu huu kwa kutoa sare nne, unafikiri inakabiliwa na mechi ya aina gani mwishoni mwa wiki?  

Sunday, October 19, 2014

TAZAMA PICHA ZA HARUSI YA MSANII HUSSEIN MACHOZI

DIVA WA CLOUDS AFUNGUKA MAZITO KUHUSU MAHUSIANO YAKE YA KIMAPENZI!

Diva Loveness wa Clouds Fm Kwa Mara Nyingine Amemuongelea Mpenzi Aliye nae Kwa Sasa Grazy GK Kupitia Blog yake, na Haya Ndio aliyoyasema: “The secret life to My happiness is the love of My life.. i believe that Love is the Greatest Gift life can give you, nilipo separate na hao waliopita thought i’d never love again but you can’t rule your heart, My bae is sucha great Person and incredibly loyal , he is the only man who seduced me with not only his charm but also his intelligence , he is matured positive and optimistic , very Passionate . we always on dinner for two with flowers ,table settings and the conversation always Brilliant and lovely….. you know when we started dating i had a feeling that i wasn’t a good enough person for him and normally that feeling wuld have made me want to leave but this time i couldn’t because i was too much in love with him, and its not about the money or fame but amma grown up sitaki mtu anieleze nani ananifaa nani type yangu nani niwe nae. i just go wit My territory. setting up my own rules in life. nishakuwa na hao wenye vyeo, pesa, majina but sikuwa na Amani. and Yol know that I am at Peace and am so Happy nilipo , am just with the Person i love most and there is no better feeling than that, couldn’t ask for more , i always put joyous smile on my face , My baby is like An Angel , the plan kati yangu na yeye was to be happy and creating some nice memories , we’ve been in tears and laughter, #PerfectMoment.❤️��

MATOKEO YA LIVERPOOL vs QPR HAYA HAPA

LIVERPOOL imeshinda 3-2 dhidi ya Queens Park Rangers jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa ugenini. Mabao ya Liverpool yamefungwa na Richard Dunne aliyejifunga dakika ya 67, Philip Coutinho dakika ya 90 na Steven Caulker aliyejifunga pia dakika hiyo hiyo ya 90. Richard Dunne leo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kujifunga mabao 10 katika historia ya Ligi Kuu ya England. Raheem Sterling alianza leo kwenye kikosi cha Liverpool na kocha wa England, Roy Hodgson akamshuhudia kutokea jukwaani. Mario Balotelli alikosa bao akiwa amebaki yeye na nyavu, baada ya kupiga juu akiwa umbali wa mita tatu wakati huo matokeo bado yapo sare.

WATOTO WA SHILOLE WAMPA MTIHANI NUH MZIWANDA!

Watoto wawili wa kike wa muimbaji wa Tanzania, Shilole, hawamuiti mpenzi wa staa huyo Nuh Mziwanda ‘baba’ bali ‘uncle’ Akiongea na Power Jams ya East Africa Radio, Nuh amesema watoto hao wanampenda. “Watoto wananiita uncle,” amesema Nuh. “Nafurahi nikiamka asubuhi ‘uncle good morning’, yaani fresh, ‘uncle maji ya kuoga’. Ni watoto lakini wananipenda, wana love kwangu. Kuna

 BOFYA HAPA KUSOMA ZAID> 

TAZAMA PICHA ZAIDI YA 2O KILICHOJIRI JANA KWENYE SERENGETI FIESTA 2014 VIWANJA VYA LEADERS

Msanii kutoka Nchini Marekani T.I akitoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Dar Katika Show ya FIesta iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Leaders.
Msanii Davido kutoka nchini Nigeria Akiwajibika
Diamond Platnumz akitoa burudani

 BONYEZA HAPA KUANGALIA PICHA ZINGINE 

WATANGAZAJI MAMBURULAAZ WA TELEVISHENI WAAMUA KUTANGAZA KIPINDI WAKIWA HIVI

Watangazaji wawili wa kipindi cha
televishen "The View" wamewapa
watazamaji wao mshangao pale walipovua nguo zao na kubaki uchi wakati show hiyoikiendelea Sherri Shepard na Jenny McCarthy wliamua kubadilisha mambo na kutangaza kipindi chao wakiwa uchi wa mnyama. Watazamajihawakuonekana kujali
kutokana na tukio hilo na kuwapigia
makofi na kelele nying

Saturday, October 18, 2014

LIVE KUTOKA TAIFA; YANGA VS SIMBA

Dk 4 Okwi anaingia na
kujaribu lakini shuti lake
linakuwa nyanya.
Dk 6, Jaja anapiga kichwa
lakini kinatoka nje kidogo ya
lango la Simba.

Picha na salehally

KALI DUNIA NZIMA HAIJAWAHI KUTOKEA, REFA NICOLAS AMLIMA KADI NYEKUNDU CAVANI KISA KUSHANGILIA KWA STAILI YA MTUTU WA BUNDUKI

MSHAMBULIAJI Edinson Cavani jana alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu walioonyeshwa kadi nyekundu wakati Paris St Germain ikiitandika RC Lens mabao 3-1 katika mchezo wa Ligue 1 Uwanja wa Stade de France. Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa alipewa kadi hiyo na refa Nicolas Rainville, baada ya kushangilia bao la mwisho la timu yake kwa ishara ya kupiga bunduki, staili maarufu kwa klabu ya Arsenal ya England. Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi ameponda maamuzi hayo ya utata akisema kwamba kama adhabu zitatolewa kwa ushangiliaji wa aina hiyo, ni mbaya kwa soka ya Ufaransa. Mabao ya PSG yalifungwa na Cabaye dakika ya 28, Maxwell dakika ya 33 na Cavani dakika ya 55, wakati Lens pia ilipoteza wachezaji wawili waliotelewa kwa kadi nyekundu, Gbamin na Le Moigne, huku bao lao la kufutia machozi likifungwa ma Coulibaly dakika ya 10.
Mshambuliaji wa Paris Saint Germain, Edinson Cavani akiwa hamming macho yake wakati analimwa kadi nyekundu
Hiruhusiwi Ufaransa; Edinson Cavani akishangi kwa staili ya mtutu wa bunduki kabla ya kutol kwa kadi nyekundu

HILI NI PIGO LINGINE KUBWA WALILOLIPATA TIMU YA LIVERPOOL

KLABU ya Liverpool imepata pigo kubwa jana wakati Daniel Sturridge alipotakiwa kuwa nje kwa angalau wiki tatu zaidi baada ya kuumia tena mazoezini.
Kocha Brendan Rodgers amekuwa na matumaini kupona kwa mshambuliaji huyo kungeimarisha kikosi chake.
Sasa Sturridge, ambaye aliumia ndama wakati wa kupasha misuli moto Melwood Alhamisi, atakosa mechi kadhaa ngumu zikiwemo za nyumbani na ugenini za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge anatarajiwa kuendelea kuwa nje kwa wiki tatu zaidi

MECHI ZA LIVERPOOL AMBAZO SASA STURRIDGE ATAZIKOSA
1. QPR v Liverpool
2. Liverpool v Real Madrid
3. Liverpool v Hull
4. Liverpool v Swansea
5. Newcastle v Liverpool
6. Real Madrid v Liverpool
7. Liverpool v Chelsea
Liverpool itakuwa na mechi saba katika wiki tatu zijazo ikiwemo ya hatua ya 16 Bora ya Kombe la Ligi, au Capital One dhidi ya Swansea Oktoba 28 na ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Chelsea Uwanja wa Anfield Novemba 8.
Sturridge alipona maumivu ya mguu aliyopata akiichezea timu ya taifa ya England Septemba mwaka huu, maumivu ambayo yalizua mtafaruku baina ya Rodgers na kocha wa Three Lions, Roy Hodgson juu ya muda wa kupona kwa mpachika mabao huyo.

TUKIO ZIMA LA MAMA MCHAWI ALIYEDONDOKA WAKATI AKIJIANDAA KWENDA KUMUUA MJUKUU WAKE

hivi karibuni tuliweka hewani tukio zima la mama mchawi wa kinigeria aliyekuwa amedondoka chini huku akiwa uchi na mwili ukiwa na vidonda sehemu zote... Mama huyo alidondoka dakika chache baada ya kujigeuza ndege na kupaa hewani akienda kuua mtoto mchanga wa binti yake wa kumzaa. Inadaiwa kuwa. binti huyo amekuwa akizaa watoto na kufariki dakika chache baada ya kuzaliwa. Kumbe mbaya wake alikuwa ni mama yake mzazi ambaye alikuwa akivifuata vitoto hivyo na kisha kuviua.Imearifiwa kuwa dada wa watu kazunguka kwa waganga mbalimbali kutafuta tiba bila mafanikio, na ndipo alipoamua kumrudia mwenyezi mungu kwa kumpigia magoti, kumlilia na kumweleza shida zake kwa njia ya maombi, kitu ambacho Mungu baba wa mbinguni amekijibu na kumdondosha mama huyo baada ya nguvu ya maombi kumzidi.Hapo chini nimekuwekea video nzima toka Nigeria ikionesha tukio zima la mama huyo na jinsi polisi walivyokuwa wakihangaika kumnusuru asichomwe moto.

 BOFYA HAPA KUIANGALIA VIDEO 

ANGALIA HII VIDEO ALICHOFANYIWA BAADA YA KUMSHIKA MCHEZAJI

Muamuzi Manuel Zeleya ameingia katika lindi la lawama kutoka kwa wachezaji pamoja na viongozi wa klabu ya Marathon inayoshiriki ligi kuu ya nchini Honduras, kufuatia adhabu ya kadi nyekundu aliyompa mlinda mlango wa klabu hiyo. Viongozi pamoja na wachezaji wamekuwa wakimlalamikia muamuzi huyo kufuatia maamuzi mazito aliyoyachukua, na kupelekea kikosi chao kicheza pungufu. Muamuzi Zeleya alichukua jukumu la kumuadhibu mlinda mlango wa klabu ya Marathon, Junior Morales wakati wa mchezo wa ligi uliowakutanisha na Real Sociedad, kutokana na utovu wa nidhamu aliouonyesha wa kumshika makalio kwa makusudi mchezaji wa timu pinzani. Hata hivyo muamuzi huyo hakuona kosa hilo, mpaka pale aliposhtuliwa na msaidia wake namba mbili, na katika hali ya mshangao alichukua maamuzi ya kumuonyesha kadi nyekundu Junior Morales na mwisho wa mambo aliamuru mkwaju wa penati kupigwa kwenye lango la Marathon. Wakati maamuzi hayo yanachukuliwa tayari timu hizo zilikuwa zimefungana bao moja kwa moja. Katika picha za televisheni Junior Morales ameonekana akimshika makalio mshambuliaji wa Real Sociedad, Morales kwa makusudi baada ya kuumiliki mpira uliokuwa unaambaa ambaa kwenye lango lake. Hata hivyo Henry Martinez aliechukua jukumu la kupiga mkwaju wa penati kufuatia maamuzi yaliyochukuliwa na Manuel Zeleya, alikosa na hivyo kuufanya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

 BOFYA HAPA KUIONA VIDEO HIYOO 

MREMBO ANAYEONGOZA BONGO KWA KUWAZUZUA WANAUME HUYU HAPA

UNAJUA KUWA KUNA UWEZEKANO DAVIDO ASISHIRIKI TAMASHA LA FIESTA KWA AMRI YA MAHAKAMA! SHUKA NAYO HAPA

Friday, October 17, 2014

KILICHOMPATA ADMIN WA BLOG MOJA HIVI KUHUSIANA NA KUMTETEA MISS TANZANIA 2014 WEE...SOMA HAPO CHINI

Sekeseke hilo limeendelea kutokea katika blog moja ambayo inahusika na umbea wa hapa Mjini ambapo admin wake aliweka mada kuhusiana na Ushindi na Umri wa Miss Tanzania 2014 aka Miss France, Miss 23 mara baada ya kuweka mada hiyo Basi Wachangiaji wakachangia na ndipo Baadae Admin wa Blog hiyo akaweka post Yenye kumtete Unajua Alichokipata Fuatilia threat hizo chini hapo........................ Na Haya ndio Maneno ya Admi wa Blog hiyo Ya Udaku aka Umbea.... Duuh ..Nimekoma! Leo nilipost Post Moja Nikimtetea Miss Tanzania kwa Kile Kinachoendelea Mitandaoni Kuhusu Ushindi wake na Umri ..Yenye Kichwa cha habari : Tumechokaaa na Story za Miss Tanzania ooh Hana Vigezo ooh Sijui Mkubwa Mara Nini na Nini "Watz bwana hata angepewa nani hilo taji la miss Tanzania msingerizika mngemchamba tu ! Muacheni Mtoto wa watu apumue kama kushinda ndio kashashinda umri wake unaingiliana vipi na umiss?" Nilichoambulia nia Kupewa za uso live Bila chenga ....Hii inaonesha Issue hii ya Miss Tanzania Bado Inaendelea kuwagusa Watu Sana Kiasi kikubwa. Soma Hapo chini Nilichoambia na Wadau wa Udaku ...Mekoma mie...Wapi Lundenga?

WEMA SEPETU USO KWA USO NA MUME WA LADY JAY DEE, GADNER!

Muigizaji maarufu nchini Wema Sepetu na Mchekeshaji MC Pilipili wanatarajiwa kuwa wa kwanza kukizindua kipindi cha Kili Chat Shows kinachotarajiwa kuanza leo. Kipindi hicho kitakachokuwa kikiendeshwa na Gadner G Habash kitakuwa ni cha nusu saa na kitakuwa kikiwakutanisha mastaa wawili wanaoshabikia timu za Yanga na Simba ambapo watapata nafasi ya kushindana namna wanavyozielewa klabu hizo. Pia mashabiki watapata nafasi ya kuwahoji maswali kuhusu shughuli zao.Kipindi hicho kitakachokuwa kikirushwa Alhamisi saa tatu usiku katika kituo cha East Africa TV ni wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo ilianza mwanzoni mwa mwezi huu kwa mashabiki wa Yanga na Simba kushiriki kampeni hiyo ambayo jumla ya Sh 100 zinashindaniwa kwa mashabiki kupiga kura kwa SMS kwa kutuma namba za ndani ya kizibo kila wanapokunywa bia ya Kilimanjaro.