Saturday, October 18, 2014
 |
Muamuzi Manuel Zeleya ameingia katika lindi la
lawama kutoka kwa wachezaji pamoja na
viongozi wa klabu ya Marathon inayoshiriki ligi
kuu ya nchini Honduras, kufuatia adhabu ya kadi
nyekundu aliyompa mlinda mlango wa klabu
hiyo.
Viongozi pamoja na wachezaji wamekuwa
wakimlalamikia muamuzi huyo kufuatia maamuzi
mazito aliyoyachukua, na kupelekea kikosi chao
kicheza pungufu.
Muamuzi Zeleya alichukua jukumu la
kumuadhibu mlinda mlango wa klabu ya
Marathon, Junior Morales wakati wa mchezo wa
ligi uliowakutanisha na Real Sociedad, kutokana
na utovu wa nidhamu aliouonyesha wa
kumshika makalio kwa makusudi mchezaji wa
timu pinzani.
Hata hivyo muamuzi huyo hakuona kosa hilo,
mpaka pale aliposhtuliwa na msaidia wake
namba mbili, na katika hali ya mshangao
alichukua maamuzi ya kumuonyesha kadi
nyekundu Junior Morales na mwisho wa mambo
aliamuru mkwaju wa penati kupigwa kwenye
lango la Marathon.
Wakati maamuzi hayo yanachukuliwa tayari timu
hizo zilikuwa zimefungana bao moja kwa moja.
Katika picha za televisheni Junior Morales
ameonekana akimshika makalio mshambuliaji wa
Real Sociedad, Morales kwa makusudi baada ya
kuumiliki mpira uliokuwa unaambaa ambaa
kwenye lango lake.
Hata hivyo Henry Martinez aliechukua jukumu la
kupiga mkwaju wa penati kufuatia maamuzi
yaliyochukuliwa na Manuel Zeleya, alikosa na
hivyo kuufanya mchezo huo kumalizika kwa
matokeo ya sare ya bao moja kwa moja. |
BOFYA HAPA KUIONA VIDEO HIYOO
0 comments:
Post a Comment