Muigizaji maarufu nchini Wema Sepetu na
Mchekeshaji MC Pilipili wanatarajiwa kuwa
wa kwanza kukizindua kipindi cha Kili Chat
Shows kinachotarajiwa kuanza leo. Kipindi
hicho kitakachokuwa kikiendeshwa na
Gadner G Habash kitakuwa ni cha nusu saa
na kitakuwa kikiwakutanisha mastaa
wawili wanaoshabikia timu za Yanga na
Simba ambapo watapata nafasi ya
kushindana namna wanavyozielewa klabu
hizo. Pia mashabiki watapata
nafasi ya kuwahoji maswali kuhusu
shughuli zao.Kipindi hicho kitakachokuwa
kikirushwa Alhamisi saa tatu usiku katika
kituo cha East Africa TV ni wa kampeni ya
Nani Mtani Jembe ambayo ilianza mwanzoni
mwa mwezi huu kwa mashabiki wa Yanga
na Simba kushiriki kampeni hiyo ambayo
jumla ya Sh 100 zinashindaniwa kwa
mashabiki kupiga kura kwa SMS kwa
kutuma namba za ndani ya kizibo kila
wanapokunywa bia ya Kilimanjaro. |
0 comments:
Post a Comment