Saturday, October 18, 2014
 |
MSHAMBULIAJI Edinson Cavani jana
alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu
walioonyeshwa kadi nyekundu wakati Paris
St Germain ikiitandika RC Lens mabao 3-1
katika mchezo wa Ligue 1 Uwanja wa Stade
de France.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa
alipewa kadi hiyo na refa Nicolas Rainville,
baada ya kushangilia bao la mwisho la timu
yake kwa ishara ya kupiga bunduki, staili
maarufu kwa klabu ya Arsenal ya England.
Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi ameponda
maamuzi hayo ya utata akisema kwamba
kama adhabu zitatolewa kwa ushangiliaji wa
aina hiyo, ni mbaya kwa soka ya Ufaransa.
Mabao ya PSG yalifungwa na Cabaye dakika
ya 28, Maxwell dakika ya 33 na Cavani
dakika ya 55, wakati Lens pia ilipoteza
wachezaji wawili waliotelewa kwa kadi
nyekundu, Gbamin na Le Moigne, huku bao
lao la kufutia machozi likifungwa
ma Coulibaly dakika ya 10. |
 |
Mshambuliaji wa Paris Saint Germain,
Edinson Cavani akiwa hamming macho yake
wakati analimwa kadi nyekundu |
 |
Hiruhusiwi Ufaransa; Edinson Cavani akishangi
kwa staili ya mtutu wa bunduki kabla ya kutol
kwa kadi nyekundu |
0 comments:
Post a Comment