Thursday, September 04, 2014

ANGEL DI MARIA MAN UNITED HAWAKUPOTEA NJIA, JAMAA ASETI BAO TATU NA KUPGA MOJA YEYE MWENYEWE ARGENTINA IKIIFUMUA UJERUMANI 4-2

WINGA Angel di Maria ametengeneza mabao matatu na kufunga moja, Argentina ikilipa kisasi cha Kombe la Dunia kwa kuifunga 4-2 Ujerumani usiku huu katika mchezo wa kirafiki mjini Dusseldorf, Ujerumani. Mchezaji huyo ghali zaidi kuwahi kusajiliwa Manchester United na Uingereza nzima alipika mabao ya Sergio Aguero, Erik Lamela na Federico Fernandez kabla ya kufunga na lake mwenyewe siku 52 tangu bao la Mario Gotze katika muda wa nyongeza liipe Ujerumani ubingwa wa dunia nchini Brazil. Mabao matano kati ya sita yamefungwa na wachezaji wa Ligi Kuu ya England, huku Andre Schurrle akiifungia Ujerumani kabla ya Gotze kuwafungia bao la pili mabingwa hao wa dunia.

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA ILI KILA NIKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI PUNDE NIZIPATAPO 


Posted via Blogaway

Wednesday, September 03, 2014

Uhamisho mkubwa katika usajili msimu huu EPL huu hapa

Angel Di Maria [Real Madrid - Manchester United] pauni milioni 59.7 Alexis Sanchez [Barcelona - Arsenal] Pauni milioni 35 Diego Costa [Atletico Madrid - Chelsea] pauni milioni 32 Eliaquim Mangala [FC Porto - Manchester City] pauni milioni 32 Cesc Fabregas [Barcelona - Chelsea] pauni milioni 30 Ander Herera [Athletic Bilbao - Manchester United] pauni milioni 29 Romelu Lukaku [Chelsea - Everton] pauni milioni 28 Luke Shaw [Southampton - Manchester United] pauni milioni 27 (Huenda ikapanda hadi £31m) Adam Lallana [Southampton - Liverpool] pauni milioni 25 Dejan Lovren [Southampton - Liverpool] pauni milioni 20 Lazar Markovic [Benfica - Liverpool] pauni milioni 20 Fedha zilizotumika katika uhamisho msimu huu ni pauni milioni 835. Msimu uliopita ilikuwa pauni milioni 760.

ROJO, DI MARIA WATAONGOZA KWA 'MITATUU' MANCHESTER UNITED

MARCO ROJO NA ANGEL DI MARIA RAIA WA ARGENTINA AMBAO WAMEJIUNGA NA MANCHESTER UNITED NDIYO WACHEZAJI WATAONGOZA KUWA NA MICHORO MINGI MWILINI KATIKA WALE WALIOJIUNGA NA MANCHESTER UNITED.

DI MARIA AELEZEA UHUSIANO WAKE NA CLUB YAKE YA ZAMANI REAL MADRID: SOMA HAPA ===>

Mchezaji mpya wa klabu ya Manchester United Angel Di Maria amezungumzia juu ya uhamisho wake kutoka Madrid na huku akisema kwamba isingekuwa mmoja wa marafiki zake kwenye klabu ya Snatiago Bernabeu basi angeweza kuihama timu hiyo msimu uliopita. Di Maria amejiunga na Manchester United mapema wiki iliyopita kwa ada ya uhamisho wa £59m ambayo imeweka rekodi mpya nchini Uingereza Winga huyo wa kimataifa wa Argentina ambaye tayari alishaanza kuhususishwa na uhamisho wa kutoka Real wakati wa dirisha la usajili la msimu uliopita, lakini baadae aliendelea kubaki Santiago Bernabeu kwa sababu ya mchezaji Cristiano Ronaldo, abaye kwa mujibu wa Di Maria ni marafiki sana. “Ukweli ni kwamba nina mahusiano mazuri mno na Cristiano Ronaldo na nilibaki Madrid msimu uliopita shukrani kwa Ronaldo,” Muargentina huyo aliiambia ESPN Radio. Di Maria ameshaanza kuitumikia Manchester United ambapo alianza kwenye mechi ya ligi kuu ya England dhidi ya Burnley.

LIGI KUU ENGLAND MSIMU HUU NI SHIDAAAA....!!!. CHEKI HAWA WASHAMBULIAJI

LIGI KUU ENGLAND MSIMU HUU KAZI IPO.WASHAMBULIAJI HAWA KUCHUANA
VILIVYO

MAKALIO FAKE YAMUUMBUA LIVE STAA HUYU MJINI KWEUPE

Oops! wahenga walisema ajali haina kinga........ Blac Chyna ni rafiki yake kipenzi kim kardashian na pia ni mama mtoto wa rapper Tyga. Mdada huyo ambaye zamani alikuwa ni stripper, amekuwa ni gumzo kwa muda mrefu kutokana na makalio yake ambayo watu wengi wanasema ni ya bandia yaani fake. Lakini mrembo humbo ambaye kwa sasa ni model, alikanusha uvumi huo na kusema makalio yake ni zawadi kutoka kwa Mungu. Yaliyojiri hivi karibuni, ni kwamba makalio hayo yalianza kuporomoka taratibu wakati anatembea na alipigwa picha akijaribu kuyafunika na sweta. Inasemekana dada huyo alioneka akikimbilia kwa dotka kwa ajili ya marekebisho ya fasta.....majanga!! Watu wanasema makalio ya Kim yanaweza kuwa bandia pia―Samaki mmoja akioza, wote wameoza heheh

 BONYA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI KIRAHISI PUNDE ZITUFIKIAPO 

HIKI NDO KINACHOSABABISHA KHEDIRA KUKAA NJE KIPINDI KIREFU MSIMU HUU

Kiungo Sami Khedira wa Real Madrid atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita. Mjerumani huyo ni majeruhi baada ya kuumia ‘kiazi’ cha mguu wake wa kushoto. Daktari wa Real Madrid amesema atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita, maana yake atarejea uwanjani katikati ya mwezi Oktoba. Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kwamba Khedira ana mpango wa kujiunga na Arsenal, lakini mwishoni Madrid ilieleza kuwa bado inamhitaji.

VITA YA NAMBA NJE NJE MAN UNITED, VAN PERSIE NAYE AMKARIBISHA NA MANENO FALCAO; "NJOO TUGOMBEE KUCHEZA"

MSHAMBULIAJI Robin van Persie amepuuzia madai kwamba matatizo yake ya goti ndiyo yameifanya Manchester United imsajili Radamel Falcao, na amesema anajiandaa kufanya kazi na mkali huyo mpya. Iliripotiwa kwamba kocha Louis van Gaal alikuwa anahofia majeruhi ya Mholanzi mwenzake huyo kama angehitaji upasuaji na ndiyo maana akatoa Pauni Milioni 6 kumsajili Falcao kwa mkopo, lakini Van Persie amesema maneno hayo hayana maana hata kidogo na atapambana kupata nafasi ya kucheza na Mcolombia huyo. "Inanifurahisha watu wanavyotengeneza maneno ya uzushi namna hii. Sijui yanatoka wapi na naweza kusema na mono wangu ukiwa moyoni mwangu kwamba sitakwenda kufanyiwa upasuaji hospitali. Falcao atavaa jezi namba 9 Old Trafford baada ya kusajiliwa kwa mkopo kutoka Monaco na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atakuwa analipwa kiasi cha Pauni 280,000 kwa wiki. Na katokana na rekodi yake nzuri ya kufunga mabao ukilinganisha na kwamba Wayne Rooney ameteuliwa kuwa Nahodha wa timu, inafikiriwa Van Persie atasotea namba kikosi cha kwanza. Lakini mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal amesema anakaribisha ushindani wa namba. "Nakaribisha ujio wake, atatufanya tube bora. Katika klabu kubwa lazima wakati wote uwe na wachezaji bora, ambayo pia ndiyo falsafa yangu. Falcao lazima apiganie nafasi yake, nami pia kadhalika. Lazima tupambane na Wayne Rooney na James Wilson kuona nani watacheza. Van Persie ameukosa mwanzo wa msimu baada ya kupewa mapumziko kufuatia kumalizika kwa Kombe la Dunia, lakini alicheza kwa dakika 60 dhidi ya Burnley mwishoni mwa wiki.

Tuesday, September 02, 2014

MAJINA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE 2013 WALIOCHAGULIWA AWAMU YA PILI KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO HAYA HAPA

MAJINA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE 2013 WALIOCHAGULIWA AWAMU YA PILI KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO YAMETANGAZWA RASMI LEO BONYEZA HAPA KUYAONA 

Na festo saimon/0657035125

Masaa kadhaa baada ya usajili wa Kagawa Dortmund – Idadi ya jezi alizouza hii hapa

Dirisha la usajili barani ulaya limefungwa usiku wa jana – Shinji Kagawa ni mmoja wa wachezaji waliofanya uhamisho katika dirisha hili la usajili. Kiungo wa Japan, aliuzwa kutoka Manchester United kwenda Borussia Dortmund kwa ada ya uhamisho wa £6.3million. Fedha hizo walizolipa Dortmund zinaweza kuwa zimerudi ndani ya siku kadhaa baada ya ripoti ya gazeti la BILD kusema kwamba mauzo ya jezi namba 7 atakayoivaa Kagawa akiwa Dortmund yamekuwa ya kasi mno. Ripoti zinasema jezi ya Shinji Kagawa iliuzwa mpaka kufikia idadi ya jezi 5,000 katika kipindi cha masaa kadhaa tangu alipotangazwa rasmi kurudi kwenye klabu yake hiyo aliyohama na kwenda United mnamo mwaka 2010.

ZENGWE ZITO LAIBUKA LEO HII KUHUSU USAJILI WA FALCAO,MAN UNITED HOI

ZENGWE. Manchester United inadaiwa kubebwa katika usajili wake, baada ya kukiuka kanuni hususan katika usajili wa mshambuliaji Radamel Falcao. Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeandika kwamba, Falcao amesajiliwa baada ya dirisha la usajili kufungwa Saa 5:00 usiku jana- wakati beki Marcos Rojo pamoja kusajiliwa mapema, lakini bado hajapatiwa visa ya kufanyia kazi. Inaelezwa Jumatatu ndiyo pazia la usajili limefungwa, lakini hadi Saa 5:00 usiku uhamisho wa Falcao ulikuwa haukamilika. Sheria za usajili zinasema usajili wote uwe umekamilishwa ifikapo Saa 5:00 usiku wa kufungwa pazia na baada ya hapo, vielelezo vyote kama mikataba, makubaliano ya uhamisho na vibali vya kufanyia kazi Uingereza lazima viwasilishwe. Ligi Kuu ya England inaruhusu saa mbili, huo ni uamuzi wao – lakini uhamisho wa kimataifa lazima uaendane na mfumo wa FIFA wa elektroniki (TMS) kufungwa usiku huo. Mfumo wa FIFA wa TMS ni wa mtandao ambao unatoa fursa kwa data zote muhimu kuingizwa ili kuweka sawa uhamisho wa kimataifa. Angalau usajili wa Rojo wa Pauni Milioni 16 kutoka Sporting Lisbon umekamilika katika masuala ya kisoka. Amepewa hati ya kimataifa na Chama cha Soka na aliwasili England wiki iliyopita kukamilsha dili lake. Lakini sheria za uhamiaji zinasema wachezaji wanaoingia nchini humo, lazia wawe na visa za kufanyia kazi. Na maofisa wa Ubalozi kwanza watafuatilia madai ya kwamba kukwama kwa visa yake kunatokana na ugomvi baina yake na jirani yake nchini kwao, Argentina mwaka 2010 kabla ya kumpatia visa ya kufanyia kazi, huku tukio hilo bado linachunguzwa na Polisi. Lakini wakati wachezaji wa Man United wamepitishwa pamoja na kuwa nje ya muda au kukwama kwenye baadhi ya mambo ya msingi katika usajili wao, wachezaji wengine wamekwamishwa na hapo ndipo Daily Mail wanapouliza haki wapi?

STAR WA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014, MWANAAFA MWINZAGO AWA KIVUTIO MITAA YA KARIAKOO

Mshindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago (Katikati) akisindikizwa na Matron pamoja na Mfanyakazi wa TMT huku akilindwa na Mabaunsa wakati alipopelekwa Katika Mitaa ya Kariakoo kwaajili ya kununua zawadi Kwaajili ya Wazazi wake.
Mfanyakazi wa TMT, Happy Ngatunga (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Mabaunsa na Mshindi wa TMT aliyejinyakulia Kitita Cha Shilingi milioni 50 katika fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Mlimani City Mwanaafa Mwinzago wakati walipokuwa katika matembezi Kariakoo.
Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa na furaha mara baada ya kupongezwa na mashabiki waliopata nafasi ya Kumsalimia na kumpongeza wakati akikatiza mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua Zawadi kwaajili ya Wazazi wake
Baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo wakimpungia Mikono kama ishara ya kumpongeza kwa kuibuka mshindi wa fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) Star wa TMT 2014 kutoka Mtwara, Mwanaafa Mwinzago Wakati alipokatiza kwenye mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua zawadi kwaajili ya wazazi wake
Wanafunzi wa Shule ya Msingi wakimpongeza Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago kwa kuweza kuibuka mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 kwa kuwabwaga mwenzake 9 na kuondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania wakati walipomuona katika moja ya mitaa ya Kariakoo wakati Star Huyo wa TMT 2014 alipokwenda Kununua Zawadi kwaajili ya kuwapatia wazazi wake ikiwa kama ishara ya Upendo na shukrani kwao
Matron wa Kambi ya TMT 2014, Kemmy akichagua baadhi ya vitenge kwa Niaba ya Star Wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipopelekwa Kariakoo kwaajili ya Kununua Vitenge kama zawadi kwa wazazi wake.

KAMPUNI ILIYOANDAA SHOW YA DIAMOND ILIYOVURUGIKA UJERUMANI YANENA

Kampuni ya Britts Event iliyohusika kuandaa show ya Diamond Stuttgart, Ujerumani imeeleza kwa kina kiini cha vurugu kubwa zilizotokea kwenye show hiyo na kusababisha uharibifu mkubwa huku baadhi ya watu wakijeruhiwa vibaya.
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Awin Williams Akpomiemie ameeleza kwa kina kuhusu mzozo uliokuwepo ndani ya kampuni hiyo ulioathiri show hiyo kwa ujumla.

Hiki ndicho alichokisema:
Watu wangu awali ya yote, ningependa kuelezea moyo wangu kwa kuuambia umma na mashabiki wa Diamond Platnumz, kwamba sisi kutoka uongozi wa Britts Events tunaomba radhi kwa kile kilichotokea usiku uliopita, wakati wa show ya Diamond Platnumz. Haikuwa imepangwa show ichelewe kuanza au kwa msanii kutotumbuiza. Hapa ntawaeleza ukweli wote wa kile kilichotokea katika tamasha hilo kwakuwa ninyi nyote mnataka kuujua ukweli.

Mradi wa Diamond ulikuwa wa gharama kubwa sana kwakuwa uongozi Britts Events ulitaka kila kitu kiwe professional. Kama kampuni tuliamua kutafuta wawekezaji watakaowekeza kwenye mradi huu hivyo tuliwafuata wawekezaji watatu lakini mmoja wao hakuwekeza sana kwani alidai hatokuwa nchini.

Wawekezaji wawili ni watu wanaofahamika sana jijini Stuttgart, mmoja anafanya kazi na jeshi la Marekani na mwingine anamiliki kampuni ya usafirishaji mjini Stuttgart. Hawa ndio wawekezaji wakubwa tuliowapata. Tuliwapa mikataba wasaini lakini yule mwenye kampuni ya usafirishaji alikataa kusaini mkataba wa mradi huo kwakuwa alitaka kuwa na mkataba wake binafsi na yule jamaa wa Marekani. Kisha nilimwambia Mr.USA kuwa hiyo haikuwa hatua sahihi lakini Mr.USA alisema ‘Britts msiwe na shaka, kila kitu kitakuwa poa.

Watu wangu, mradi ulianza na kisha wale wawekezaji wawili wakagundua kuwa Diamond ni msanii mkubwa na angevuta umati mkubwa wa watu na watu wanampenda. Kisha walijiunga pamoja dhidi ya Britts waliowaalika kama wawekezaji kwenye mradi huo na walitaka kuuchukua kutoka kwa Britts sababu ni wao ndio walioleta sehemu ya fedha kwaajili ya mradi huu wakati Britts ndio wanaommiliki msanii na mradi wenyewe. Ila tu kwakuwa Britts ni kampuni mpya mjini Stuttgart, Mr. Shipping Guy aliamua kuungana na yule jamaa wa Marekani na DJ Wanted, kuuchukua mradi.

Pindi Britts ilipokaa chini na kufanya mkutano nao, walikuwa wakifanya mkutano wao wenyewe na kubadilisha mipango yote hivyo walikuwa wanahujumu na kuendelea na mradi nyuma ya Britts. Britts ina makubaliano nao kuwa pindi msanii atakapowasili Ujerumani, watampa balance ya 3.250 euros, na walikubaliana na kigezo hicho kwasababu Diamond aliweka wazi kuwa bila fedha asingepanda ndege.

Waliniomba mimi niongee na Diamond kuwa watampa fedha kwenye uwanja wa ndege, lakini unajua nini? Kabla Diamond hajawasili Mr. USA na Mr. Shipping Guy pamoja na DJ Wanted walitaka kuandaa wahuni kumuiba msanii kutoka kwenye show ya Britts lakini Britts walikuwa wajanja na walimchukua msanii kabla hawajafanya chochote. Hapo ndipo shida ilipoanzia.

Huko Essen kabla Britts haijafika huko, USA Guy na Shipping Guy, walikuwa wameshapeleka wafanyakazi wapya kuchukua show na kuwafukuza wafanyakazi wa mwanzo. Kisha Britts ilikuwa ikilumbana nao kuwa wao ni wawekezaji tu na sio waratibu wa kampuni, kwanini wanataka kuhodhi tukio kwasababu mnataka kutengeneza fedha na sio kujali watu. Britts baadaye ilikuja kugundua kuwa wafanyakazi waliowapeleka walikuwa wapenzi wao wa zamani na ndugu zao.

Dhumuni la kufanya hivyo lilikuwa ni kuiba fedha na kutofuata mkataba na Britts, hivyo baada ya Diamond kuwasili Stuttgart usiku wa saa tano, alikuwa amechoka lakini wawekezaji hawakujali. Walikuwa wakifirikia tu jinsi wanavyoweza kurudisha fedha zao. Diamond alisema anahitaji fedha yake lakini Shipping Guy na USA Guy walikataa kumpa fedha Diamond wakihisi kuwa Britts wanataka fedha ya ziada.

Kisha usiku ulipoingia sana, waliweza kutoa 3.000 euros na ilikuwa saa tisa na nusu tayari lakini Diamond aliendelea kukataa kutumbuiza kwakuwa alidai ni lazima wamlipe fedha iliyosalia ambayo ni 250 euros, kitu ambacho ni haki yake kutokana na makubaliano Mpaka muda Mr Shipping Guy na Mr USA Guy wanagundua kuwa Britts walikuwa wakifanya kitu sahihi kwa kuwaomba walipe fedha hizo kwa Diamond, tulikuwa tumeshachelewa na watu walikuwa wameshaanza kupigana wakati huo Diamond alikuwa ndani ya gari mbele tu ya ukumbi, na kama ningemruhusu atoke wangemuua.

Tunavyoongea hapa, Mr USA anadai kuwa fedha tulizoingiza kwenye tukio zima ziliibwa na watu hivyo Britts Events haiwezi kupata fedha kutoka kwenye tukio tuliloliandaa na kulimiliki. Hiyo ilikuwa mipango yao kuchukua biashara ya mtu mwingine kutokana na tama.

Britts Events inawapenda, Britts Events ilitaka kila mtu awe na furaha, Britts Event haijawahi kuahidi msanii yeyote na asije. Na niamini hata tulipofanya show ya Bracket tulikuwa na kitu kile kile kutoka kwa wawekezaji.

Walipoona kuwa show inaweza kuwa na mafanikio walitaka kupewa asilimia 50% ya kampuni.
Well, sitakiwi kusema yote haya kwakuwa ni jambo la uongozi lakini niliamua kuweka mambo sawa, siwezi kuficha tena. Tuna Waafrika wengi wenye tamaa wanaotaka kuchukua biashara za watu wengine sababu ya tamaa. Lengo letu ni kuwafanya muwe na furaha na sio kupoteza muda na fedha zenu. Tunafahamu kuwa nyote mlitoka sehemu za mbali, mliacha watoto wenu na familia.
Uongozi wa Britts Events unaomba radhi kwa hili.

Hivyo msiilamu Britts Events lakini laumuni tamaa za Mr. USA Guy na Mr. Shipping Guy. Tunawapenda na tunaahidi show ya bure ya Diamond hivi karibuni.

Audio: Dogo D amdiss Mo Music, Young Killer na Nay wa Mitego, Mo asema kuna watu wanampotosha

Rapper wa Mwanza mwenye umri mdogo aitwaye Dogo D amemdiss hitmaker wa ‘Basi Nenda’ Mo Music, Young Killer na Nay wa Mitego, kwenye ngoma yake, Wamenichokoza. Dogo D Kisa cha kumchana Mo Music ni kutokana na kudai alitaka amshirikishe kwenye wimbo wake aliourekodi kwenye studio za Classic Sounds zilizo chini ya producer Mona Gangster lakini hadi leo amekuwa akimchenga. “Mwanzoni ulipokwenda, pamoja tulikwenda, kuhit Basi Nenda kufanya ngoma yangu ndio unanipiga kalenda,” anarap Dogo D kwenye wimbo huo ambao ni muendelezo wa wimbo wa Nay wa Mitego, Wamenichokoza. Akiongea kwenye kipengele cha Inbox kwenye kipindi cha Next Chapter cha Radio Free Africa, Dogo amedai kuwa kila akimpigia simu Mo Music aende kuweka kipande chake kwenye wimbo huo amekuwa akimpiga kalenda kwa sababu za kuwa kwenye shows. Kwa upande wake Mo Music amedai kuwa hajakataa kufanya chorus ya wimbo huo bali ratiba zao zimekuwa zikichengana. Mo anasema yeye na producer wake aitwaye Lollipop wamekuwa na mpango wa kumsaidia rapper huyo kwa kugharamia miradi yake ikiwemo video na hivyo anashangaa kumsikia Dogo akimdiss tena. “Imani yangu sio yeye ndio maana siwezi kumchukia Dogo. Nahisi alichokiandika it’s not Dogo D, yaani nyuma yake kuna watu wanampotosha, hayupo hivyo namfahamu,” Mo Music ameimbia Inbox. “Kwahiyo wakamjaza sumu kwasababu namfahamu Dogo D, ana love na mimi mpaka inapitiliza, kwahiyo kuna watu wanamtengeneza.” Sikiliza kipengele hicho hapo chini kwa kubonyeza link

>>>>>>>>> BONYA HAPA KUSIKILIZA <<<<<<<<<<<