Wednesday, September 03, 2014

HIKI NDO KINACHOSABABISHA KHEDIRA KUKAA NJE KIPINDI KIREFU MSIMU HUU

Kiungo Sami Khedira wa Real Madrid atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita. Mjerumani huyo ni majeruhi baada ya kuumia ‘kiazi’ cha mguu wake wa kushoto. Daktari wa Real Madrid amesema atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita, maana yake atarejea uwanjani katikati ya mwezi Oktoba. Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kwamba Khedira ana mpango wa kujiunga na Arsenal, lakini mwishoni Madrid ilieleza kuwa bado inamhitaji.

0 comments:

Post a Comment