Wednesday, September 03, 2014
|
Mchezaji mpya wa klabu ya Manchester United
Angel Di Maria amezungumzia juu ya uhamisho
wake kutoka Madrid na huku akisema kwamba
isingekuwa mmoja wa marafiki zake kwenye
klabu ya Snatiago Bernabeu basi angeweza
kuihama timu hiyo msimu uliopita.
Di Maria amejiunga na Manchester United
mapema wiki iliyopita kwa ada ya uhamisho wa
£59m ambayo imeweka rekodi mpya nchini
Uingereza
Winga huyo wa kimataifa wa Argentina ambaye
tayari alishaanza kuhususishwa na uhamisho
wa kutoka Real wakati wa dirisha la usajili la
msimu uliopita, lakini baadae aliendelea kubaki
Santiago Bernabeu kwa sababu ya mchezaji
Cristiano Ronaldo, abaye kwa mujibu wa Di
Maria ni marafiki sana.
“Ukweli ni kwamba nina mahusiano mazuri
mno na Cristiano Ronaldo na nilibaki Madrid
msimu uliopita shukrani kwa Ronaldo,”
Muargentina huyo aliiambia ESPN Radio.
Di Maria ameshaanza kuitumikia Manchester
United ambapo alianza kwenye mechi ya ligi
kuu ya England dhidi ya Burnley. |
0 comments:
Post a Comment