Tuesday, September 02, 2014
 |
Rapper wa Mwanza mwenye umri mdogo
aitwaye Dogo D amemdiss hitmaker wa ‘Basi
Nenda’ Mo Music, Young Killer na Nay wa
Mitego, kwenye ngoma yake, Wamenichokoza.
Dogo D
Kisa cha kumchana Mo Music ni kutokana na
kudai alitaka amshirikishe kwenye wimbo wake
aliourekodi kwenye studio za Classic Sounds
zilizo chini ya producer Mona Gangster lakini
hadi leo amekuwa akimchenga.
“Mwanzoni ulipokwenda, pamoja tulikwenda,
kuhit Basi Nenda kufanya ngoma yangu ndio
unanipiga kalenda,” anarap Dogo D kwenye
wimbo huo ambao ni muendelezo wa wimbo
wa Nay wa Mitego, Wamenichokoza. Akiongea
kwenye kipengele cha Inbox kwenye kipindi cha
Next Chapter cha Radio Free Africa, Dogo
amedai kuwa kila akimpigia simu Mo Music
aende kuweka kipande chake kwenye wimbo
huo amekuwa akimpiga kalenda kwa sababu za
kuwa kwenye shows.
Kwa upande wake Mo Music amedai kuwa
hajakataa kufanya chorus ya wimbo huo bali
ratiba zao zimekuwa zikichengana. Mo anasema
yeye na producer wake aitwaye Lollipop
wamekuwa na mpango wa kumsaidia rapper
huyo kwa kugharamia miradi yake ikiwemo
video na hivyo anashangaa kumsikia Dogo
akimdiss tena.
“Imani yangu sio yeye ndio maana siwezi
kumchukia Dogo. Nahisi alichokiandika it’s not
Dogo D, yaani nyuma yake kuna watu
wanampotosha, hayupo hivyo namfahamu,” Mo
Music ameimbia Inbox. “Kwahiyo wakamjaza
sumu kwasababu namfahamu Dogo D, ana love
na mimi mpaka inapitiliza, kwahiyo kuna watu
wanamtengeneza.”
Sikiliza kipengele hicho hapo chini kwa kubonyeza link |
>>>>>>>>> BONYA HAPA KUSIKILIZA <<<<<<<<<<<
0 comments:
Post a Comment