Thursday, September 04, 2014

ANGEL DI MARIA MAN UNITED HAWAKUPOTEA NJIA, JAMAA ASETI BAO TATU NA KUPGA MOJA YEYE MWENYEWE ARGENTINA IKIIFUMUA UJERUMANI 4-2

WINGA Angel di Maria ametengeneza mabao matatu na kufunga moja, Argentina ikilipa kisasi cha Kombe la Dunia kwa kuifunga 4-2 Ujerumani usiku huu katika mchezo wa kirafiki mjini Dusseldorf, Ujerumani. Mchezaji huyo ghali zaidi kuwahi kusajiliwa Manchester United na Uingereza nzima alipika mabao ya Sergio Aguero, Erik Lamela na Federico Fernandez kabla ya kufunga na lake mwenyewe siku 52 tangu bao la Mario Gotze katika muda wa nyongeza liipe Ujerumani ubingwa wa dunia nchini Brazil. Mabao matano kati ya sita yamefungwa na wachezaji wa Ligi Kuu ya England, huku Andre Schurrle akiifungia Ujerumani kabla ya Gotze kuwafungia bao la pili mabingwa hao wa dunia.

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA ILI KILA NIKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI PUNDE NIZIPATAPO 


Posted via Blogaway

1 comment: