Wednesday, September 03, 2014
|
MSHAMBULIAJI Robin van Persie amepuuzia
madai kwamba matatizo yake ya goti ndiyo
yameifanya Manchester United imsajili
Radamel Falcao, na amesema anajiandaa
kufanya kazi na mkali huyo mpya.
Iliripotiwa kwamba kocha Louis van Gaal
alikuwa anahofia majeruhi ya Mholanzi
mwenzake huyo kama angehitaji upasuaji na
ndiyo maana akatoa Pauni Milioni 6 kumsajili
Falcao kwa mkopo, lakini Van Persie amesema
maneno hayo hayana maana hata kidogo na
atapambana kupata nafasi ya kucheza na
Mcolombia huyo.
"Inanifurahisha watu
wanavyotengeneza maneno ya uzushi namna
hii. Sijui yanatoka wapi na naweza kusema
na mono wangu ukiwa moyoni mwangu
kwamba sitakwenda kufanyiwa upasuaji
hospitali.
Falcao atavaa jezi namba 9 Old Trafford baada
ya kusajiliwa kwa mkopo kutoka Monaco na
mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28
atakuwa analipwa kiasi cha Pauni 280,000 kwa
wiki.
Na katokana na rekodi yake nzuri ya kufunga
mabao ukilinganisha na kwamba Wayne
Rooney ameteuliwa kuwa Nahodha wa timu,
inafikiriwa Van Persie atasotea namba kikosi
cha kwanza. Lakini mshambuliaji huyo wa
zamani wa Arsenal amesema anakaribisha
ushindani wa namba.
"Nakaribisha ujio wake, atatufanya tube bora.
Katika klabu kubwa lazima wakati wote uwe na
wachezaji bora, ambayo pia ndiyo falsafa
yangu. Falcao lazima apiganie nafasi yake,
nami pia kadhalika. Lazima tupambane na
Wayne Rooney na James Wilson kuona nani
watacheza.
Van Persie ameukosa mwanzo wa msimu
baada ya kupewa mapumziko kufuatia
kumalizika kwa Kombe la Dunia, lakini alicheza
kwa dakika 60 dhidi ya Burnley mwishoni
mwa wiki. |
0 comments:
Post a Comment