Tuesday, September 02, 2014

Masaa kadhaa baada ya usajili wa Kagawa Dortmund – Idadi ya jezi alizouza hii hapa

Dirisha la usajili barani ulaya limefungwa usiku wa jana – Shinji Kagawa ni mmoja wa wachezaji waliofanya uhamisho katika dirisha hili la usajili. Kiungo wa Japan, aliuzwa kutoka Manchester United kwenda Borussia Dortmund kwa ada ya uhamisho wa £6.3million. Fedha hizo walizolipa Dortmund zinaweza kuwa zimerudi ndani ya siku kadhaa baada ya ripoti ya gazeti la BILD kusema kwamba mauzo ya jezi namba 7 atakayoivaa Kagawa akiwa Dortmund yamekuwa ya kasi mno. Ripoti zinasema jezi ya Shinji Kagawa iliuzwa mpaka kufikia idadi ya jezi 5,000 katika kipindi cha masaa kadhaa tangu alipotangazwa rasmi kurudi kwenye klabu yake hiyo aliyohama na kwenda United mnamo mwaka 2010.

0 comments:

Post a Comment