Monday, September 01, 2014
PERUZI KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI YA LEO JUMATATU HAPA
SEHEMU:1 KIONGOZI WA FREMASOON MTANZANIA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU ALIVOJIUNGA NA MAMBO MENGINE YANAYO WAHUSU
#Exclusive: Mambo 6 ya kufahamu kuhusu Linah na hit single ya ‘Ole Themba’
Nafasi yake nyingine kubwa ya kuzungumziwa toka ameanza muziki ni hii aliyoipata baada ya kufanya wimbo wa ‘Ole Themba’ na kundi maarufu la Uhuru South Africa.Ni kolabo ambayo mpaka August 31 2014 usiku video yake YouTube ilikua imebakiza sio chini ya views elfu mbili ili kufikisha views laki moja za wote walioitazama toka iweke July 2014.
Yafuatayo ni mambo 6 ya kufahamu kuhusu Linah na hit single ya ‘Ole Themba’.
1. Video hii ya ‘Ole Themba’ imeanza kuchezwa kwenye vituo vikubwa vya TV Africa ikiwemo MTV Base pamoja na TV ya Ufaransa ya TRACE Urban ambao tayari wameshamtumia Linah mkataba wa makubaliano.
2. Wakati aliposafiri kwenda Afrika Kusini kuirekodi hii single na Uhuru, alikaa kwa mwezi mmoja bila kufanya chochote mpaka kufikia kukata tamaa manake Uhuru kama walimuwekea ‘pozi’ japokua Linah alikua na pesa mkononi tena milioni za Tanzania kwa ajili ya kulipia kurekodi nao hiyo single kama makubaliano yalivyokuwa.
3. Linah anasema Producer wa Uhuru aliwatajia hela nyingi kurekodi hiyo kolabo akidhani watashindwa kuilipia lakini haikua hivyo, mwanzoni aliwawekea pozi kwa kuagiza atumiwe link za video za Linah YouTube ili ajue uwezo wake lakini hakuwahi kuzitazama.
4. Producer huyu alikua akipigiwa simu mara nyingi lakini hakuwa anapokea na hata msg anaweza kujibu au kutojibu ambapo linah anasema ‘ilikua ngumu sana mwanzoni lakini baada tu ya kuingia studio kuweka voco ya kwanza nikapata na kolabo hapohapo, yani walikubali uwezo wangu’
5. Baada ya Uhuru kuona single ya ‘Ole Themba’ imeanza kuwa kubwa kwa kufanya vizuri kwenye Radio na TV kulitokea kama kutokuelewana kidogo kwa kuona Linah anaanza kupata hela.
6. ‘Waliitengeneza kama na wao wana haki na wimbo wenyewe lakini uzuri ni kwamba tulishasaini mkataba mwanzoni kuwa wimbo wametuuzia ni mali yetu na wala hawana haki yoyote, alietunga melody alisaini na tumemlipa so hausiki tena, tulimlipa kila mtu na kazi yake…. namshukuru Mungu iliisha vizuri’- Linah
HAYA NDO MAPYA YALIYOMKUTA DIAMOND PLATINUM HUKO UJERUMANI BILA POLISI LEO HII TUNGEKUWA TUNASEMA MENGINE
Stuttgart, Ujerumani - Usiku wa Jumamosi ya tarehe 30 Agosti 2014, majira ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa Bongo Flavor, Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.
Washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake.
Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki.
Ma-Djs walishambuliwa na wapo hosptalini kwa sasa. Mmoja wa Djs hao alipoteza laptop yake, mwanadada Dj Flor alipatwa shock (mstuko wa moyo) na kukimbizwa hosptali.
Washabiki hao walimpa kipigo Dj Drazee ambaye naye yupo hoi hospitalini.
Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hili la aibu alijawahi kutokea. Kwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria, ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND" Na mdadisiblog/festosaimon
Shinji Kagawa ameondoka Man United – hii ndio timu aliyoenda
RONALDO AMCHANA VIBAYA MOURINHO,AMPA TANO FERGUSON
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII NA KALIBU TENA NA KAMA UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA
HUYU NDO MCHEZAJI ALIYEKAMILISHA UHAMISHO WAKE CHELSEA KUTOKA QPR
Sunday, August 31, 2014
MATOKEO YA MECHI KATI YA LIVERPOOL vs TOTTENHAM HAYA HAPA
HII NDIYO 'FIRST ELEVEN' YA PHIRI SIMBA SC, HAKUNA OKWI, MKUDE WALA KIONGERA...NA BADO KUNA WAKALI WENGINE WA KIKOSI CHA PILI WANATISHA
HII NDIYO 'FIRST ELEVEN' YA PHIRI SIMBA SC, HAKUNA OKWI, MKUDE WALA KIONGERA...NA BADO KUNA WAKALI WENGINE WA KIKOSI CHA PILI WANATISHA
HAYA NDO MAPYA YALIYOBUKA OLD TRAFORD KUHUSU ROJO
LICHA YA SKENDO, MIGOGORO KATIKA FAMILIA: FLORA MBASHA AJA NA MPYA:
BAADA YA DIAMOND PLATNUMZ KUPELEKWA KWENYE SHOW SAA 10 ALFAJIRI HUKO GERMANY, DIAMOND ATOA YA MOYONI
Beki hii ya Simba, mh!
Maximo: Wananichunguza? Wanapoteza muda wao
Manji jeuri, aapa Okwi hachezi Simba
Amissi Tambwe azua balaa jipya Msimbazi







