Monday, September 01, 2014
 |
| Yamebaki masaa takribani 18 kabla ya dirisha
la usajili kufungwa, taarifa mpya ni kwamba
kiungo wa kimataifa wa Japan na Manchester
United Shinji Kagawa ameihama klabu hiyo.
Kagawa aliyejiunga na Man United misimu
miwili iliyopita amerudi kwenye klabu
aliyotoka ya Borrusia Dortmund ya
Ujerumani.
Man United walimnunua Shinji kwa ada ya
uhamisho wa £12m na leo hii imethibitishwa
kwamba amejiunga na Dortmund kwa £8m.
Wakati huo huo mwanasoka wa Uholanzi
aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Ajax
Daley Blind amefanyiwa vipimo vya afya tayari
kujiunga na Man United kwa ada ya £13m. |
KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment