Monday, September 01, 2014
 |
| Cristiano Ronaldo ameamua
kufunguka kuhusiana na
uhusiano wake na Kocha Jose
Mourinho na kusema hakuwahi
kuwa rafiki yake hata
chembe.
Licha ya Mourinho kuwahi
kuwa rafiki yake na raia
mwenzake wa Ureno, Ronaldo
amesema hajawahi kuwa na
urafiki naye, badala yake
akasisitiza katika makocha,
rafiki yake ni mmoja tu,
Alex Ferguson aliyekuwa
naye Manchester United.
Aidha, Ronaldo amemlaumu
Mourinho kwamba wakati
akiwa kocha wa Madrid
alisababisha mambo mengi
kama ugomvi kati ya
wachezaji na hata
mashabiki.
Mourinho hakuelewana na
Iker Casillas, Angel Di
Maria, Sergio Ramos na hata
Mreno mwenzake, Pepe.
Ronaldo amesema Mourinho
alifanya hali ya hewa
kutotulia ndani ya kikosi
chao huku akisisitiza
hayuko kwenye soka kutafuta
marafiki, badala yake
anataka kushinda. |
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII NA KALIBU TENA NA KAMA UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment