| Hiki ndicho kikosi cha kwanza cha Simba SC,
ambacho kocha Patrick Phiri amekuwa
akikitanguliza dakika 45 za kwanza katika
mechi zake visiwani Zanzibar. Na hiki
ndicho kikosi kilichomaliza kipindi cha
kwanza kinaongoza 4-0 dhidi ya KMKM jana
katika ushindi wa 5-0. Kutoka kulia
waliosimama ni Joram Mgeveke, Miraj
Adam, Ivo Mapunda, Joseph Owino, Amri
Kiemba, na Haroun Chanongo.
Waliochuchumaa kutoka kulia ni
Ramadhani Singano 'Messi', Pierre Kwizera,
Shaaban Kisiga, Amisi Tambwe na Issa
Rashid. Wachezaji watatu wa kiwango cha
juu, Emmanuel Okwi, Paul Kiongerea na
Jonas Mkude hawapo hapa. Na kuna
wachezaji wa kikosi cha pili kama Said
Ndemla, Elias Maguri, Twaha Ibrahim
'Messi' wanafanya vizuri. Hii inamaanisha
Simba SC ipo vizuri kuelekea msimu ujao. |
0 comments:
Post a Comment