| LIVERPOOL imeichapa mabao 3-0 Tottenham
Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England
jioni ya leo Uwanja wa White Hart Lane.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Raheem
Sterling dakika ya nane kwa shuti la umbali wa
mita saba, Steven Gerrard dakika ya 48 kwa
penalti baada ya Eric Dier kumchezea rafu Joe
Allen na Alberto Moreno dakika ya 60.
Mshambuliaji mpya, Mario Balotelli
aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka AC
Milan wiki iliyopita, leo amecheza mechi yake
ya kwanza Liverpool, lakini hakufunga licha ya
kucheza soka nzuri.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet,
Manquillo, Moreno, Gerrard, Lovren, Sakho,
Henderson, Sterling/Enrique dk86, Sturridge,
Balotelli/Markovic dk61 na Allen/Can dk61.
Tottenham Hotspur: Lloris, Dier, Rose/Davies
dk72, Capoue, Kaboul, Vertonghen, Lamela,
Bentaleb/Dembele dk59, Adebayor, Eriksen/
Townsend dk59 na Chadli. |
0 comments:
Post a Comment