| Msanii wa muziki Florah Mbasha, Baada ya
kufunguka mengi kuhusiana na matatizo katika
ndoa yake wiki hii, ameweka wazi kuwa
shughuli zake za muziki bado zinaendelea huku
akiwa na albam mpya kabisa kwaajili ya
wapenzi wa sanaa yake.
Frorah Mbasha amesema kuwa, anamshukuru
Mungu kwa kufanikisha kutoa albam mpya
inayokwenda kwa jina Nipe Nguvu ya Kushinda,
kazi ambayo tayari jamii imeipokea vizuri.
Msanii huyu ambaye amezoeleka kufanya kazi
ya muziki pamoja na mumewe Emmanuel
Mbasha, amewatoa wasiwasi mashabiki kuwa
licha ya mgogoro, Mumewe yupo katika kazi
hii. |
0 comments:
Post a Comment