Sunday, August 31, 2014

Amissi Tambwe azua balaa jipya Msimbazi

UVUMI kwamba uongozi wa Simba ulikuwa na mpango wa kumtema straika namba moja, Mrundi Amissi Tambwe, ili kumpisha Mganda Emmanuel Okwi, jana ulizua balaa kubwa baada ya baadhi ya mashabiki kutaka kuandamana Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, jijini Dar es Salaam kupinga, kabla ya uongozi kuzima mambo. Uvumi huo ulianza baada ya kudaiwa kwamba kocha Patrick Phiri amewaambia viongozi kwamba Mrundi mwingine, Pierre Kwizera na Okwi wanatosha katika safu yake ya mbele. Mapenzi ya mashabiki hao kwa Tambwe, yamejengwa na kiwango alichokionyesha straika huyo tangu alipotua klabuni hapo ambapo msimu uliopita ndiye aliyekuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara kwa kufunga mabao 19. Hadi tulipokuwa tunakwenda mitamboni jana usiku huku usajili ukiwa katika dakika za lala salama, Simba ilikuwa katika mazungumzoa na mabeki, Salum Salim Mbonde, wa Mtibwa na Juma Nyosso (huru) ili kumpata mmoja wao kuziba nafasi ya Mkenya, Donald Mosoti, ambaye ameomba kuachwa ili akacheze soka Qatar. Lakini Mwanaspoti linajua kwamba viongozi hao walikuwa wamewekeza akili zao kwa Mbonde kuliko Nyosso ambaye hata kocha Phiri anamkubali.credit mwanaspoti

0 comments:

Post a Comment