Monday, September 01, 2014

SEHEMU:1 KIONGOZI WA FREMASOON MTANZANIA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU ALIVOJIUNGA NA MAMBO MENGINE YANAYO WAHUSU

Mtanzania mmoja, ambaye alianzia ngazi ya chini hadi kufikia kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki, akiongoza zaidi ya vitengo 50, anaeleza kwa undani namna alivyojiunga na chama hicho akiwa bado kijana. Akiwa na umri wa miaka 24, Jayantilal Keshvji Chande, maarufu zaidi kwa jina la Sir Chande, alikuwa tayari ameshavutiwa kujiunga na Freemason, lakini hakujua vipi na wapi kwa kuanzia. Kwa maneno yake, Sir Chande anasema kuwa hamu ya kujiunga na Freemason ilichochewa na tabia ya rafiki zake wawili wa wakati huo, Mwingereza, Bob Campbell Ritchie na John McLean kutoka Scotland. Rafiki zake hao walikuwa na ratiba isiyokuwa ya kawaida hasa wakati wa jioni. Kila Jumatatu baada ya kutoka kazini, walikuwa wakihudhuria kile alichokiita ‘vikao vya kushangaza’ kwenye jengo moja lililopo karibu na bahari, Dar es Salaam. Taratibu, udadisi wa Sir Chande kuhusu sehemu waliyokuwa wakienda rafiki zake ikajulikana, baada ya wao wenyewe kumweleza kuwa walikuwa ni wanachama wa Freemason. ‘Haraka nilitaka kuwa mwanachama’, anaandika Sir Chande katika kitabu chake “Usiku Afrika; Njia kutoka Bukene.” Kwa kuwa kujiunga Freemason siyo kwa kutuma maombi au kwa usaili, bali kwa kupendekezwa, haikuwepo njia nyingine ya kufanya hivyo. Marafiki zake Sir Chande walimtambulisha kwa wanachama wa Freemason wengine, Sheikh Mustafa na Jivraj Patel, ambao kwa mwanzoni walilazimika kuwa kama ndugu yao kwa kuwa walikuwa wakifahamika ndani ya chama hicho. Ilimchukua Sir Chande miaka miwili ya kusubiri, kuchunguzwa na kuona kama alikuwa na uadilifu unaohitajika kujiunga katika chama hicho, kinachodaiwa kujihusisha na giza na siri ikiwamo matambiko na kutoa kafara za binadamu kupata utajiri na nguvu. “Kama ambavyo nilitarajia,” anaandika Sir Chande akieleza: “Nilitakiwa kusubiri kwa miaka miwili wakati naangaliwa kama ninaweza kufaa.” “Hakuna mtu ambaye alinionya kuhusu maumivu anayoyapata mtu wakati wa kipindi cha matazamio, bila kujali masuala ya kifedha au msimamo wake kwenye jamii,” anaandika. Kwa mujibu wa Sir Chande, wakati wa kuchunguzwa, kazi zake zote za kila siku, ndani na nje ya ofisi zilikuwa zikifuatiliwa kwa umakini mkubwa. Baadhi ya rafiki na ndugu zake pia walihojiwa. “Ingawa nilikuwa natoka katika familia za watu wenye asili ya Asia waliofanikiwa kibiashara Afrika Mashariki, haikusaidia kurahisisha,” anaandika na kuongeza kuwa baada ya miaka miwili alijiunga na moja ya taasisi hatari duniani. Kujiunga Freemason siyo kwa kuomba au kusailiwa tu. Kinyume na wengi wanavyodhani, badala yake kwa mujibu wa Sir Chande, mtu anakuwa mwanachama kwa kupendekezwa na mtu ambaye tayari ni mwanachama. Itaendelea Jumanne ,fatilia ujue ukweli kuhusu tuhuma za kuabudu mashetani na kama kweli Freemason ni taasisi ya siri.

#Exclusive: Mambo 6 ya kufahamu kuhusu Linah na hit single ya ‘Ole Themba’


Nafasi yake nyingine kubwa ya kuzungumziwa toka ameanza muziki ni hii aliyoipata baada ya kufanya wimbo wa ‘Ole Themba’ na kundi maarufu la Uhuru South Africa.Ni kolabo ambayo mpaka August 31 2014 usiku video yake YouTube ilikua imebakiza sio chini ya views elfu mbili ili kufikisha views laki moja za wote walioitazama toka iweke July 2014.
Yafuatayo ni mambo 6 ya kufahamu kuhusu Linah na hit single ya ‘Ole Themba’.

1. Video hii ya ‘Ole Themba’ imeanza kuchezwa kwenye vituo vikubwa vya TV Africa ikiwemo MTV Base pamoja na TV ya Ufaransa ya TRACE Urban ambao tayari wameshamtumia Linah mkataba wa makubaliano.

2. Wakati aliposafiri kwenda Afrika Kusini kuirekodi hii single na Uhuru, alikaa kwa mwezi mmoja bila kufanya chochote mpaka kufikia kukata tamaa manake Uhuru kama walimuwekea ‘pozi’ japokua Linah alikua na pesa mkononi tena milioni za Tanzania kwa ajili ya kulipia kurekodi nao hiyo single kama makubaliano yalivyokuwa.

3. Linah anasema Producer wa Uhuru aliwatajia hela nyingi kurekodi hiyo kolabo akidhani watashindwa kuilipia lakini haikua hivyo, mwanzoni aliwawekea pozi kwa kuagiza atumiwe link za video za Linah YouTube ili ajue uwezo wake lakini hakuwahi kuzitazama.

4. Producer huyu alikua akipigiwa simu mara nyingi lakini hakuwa anapokea na hata msg anaweza kujibu au kutojibu ambapo linah anasema ‘ilikua ngumu sana mwanzoni lakini baada tu ya kuingia studio kuweka voco ya kwanza nikapata na kolabo hapohapo, yani walikubali uwezo wangu’

5. Baada ya Uhuru kuona single ya ‘Ole Themba’ imeanza kuwa kubwa kwa kufanya vizuri kwenye Radio na TV kulitokea kama kutokuelewana kidogo kwa kuona Linah anaanza kupata hela.

6. ‘Waliitengeneza kama na wao wana haki na wimbo wenyewe lakini uzuri ni kwamba tulishasaini mkataba mwanzoni kuwa wimbo wametuuzia ni mali yetu na wala hawana haki yoyote, alietunga melody alisaini na tumemlipa so hausiki tena, tulimlipa kila mtu na kazi yake…. namshukuru Mungu iliisha vizuri’- Linah

HAYA NDO MAPYA YALIYOMKUTA DIAMOND PLATINUM HUKO UJERUMANI BILA POLISI LEO HII TUNGEKUWA TUNASEMA MENGINE

Stuttgart, Ujerumani - Usiku wa Jumamosi ya tarehe 30 Agosti 2014, majira ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa Bongo Flavor,  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.

Washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake.

Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki.

Ma-Djs walishambuliwa na wapo hosptalini kwa sasa. Mmoja wa Djs hao alipoteza laptop yake, mwanadada Dj Flor alipatwa shock (mstuko wa moyo) na kukimbizwa hosptali.

Washabiki hao walimpa kipigo Dj Drazee ambaye naye yupo hoi hospitalini.

Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hili la aibu alijawahi kutokea. Kwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria, ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND"  Na mdadisiblog/festosaimon

Shinji Kagawa ameondoka Man United – hii ndio timu aliyoenda

Yamebaki masaa takribani 18 kabla ya dirisha la usajili kufungwa, taarifa mpya ni kwamba kiungo wa kimataifa wa Japan na Manchester United Shinji Kagawa ameihama klabu hiyo. Kagawa aliyejiunga na Man United misimu miwili iliyopita amerudi kwenye klabu aliyotoka ya Borrusia Dortmund ya Ujerumani. Man United walimnunua Shinji kwa ada ya uhamisho wa £12m na leo hii imethibitishwa kwamba amejiunga na Dortmund kwa £8m. Wakati huo huo mwanasoka wa Uholanzi aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Ajax Daley Blind amefanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na Man United kwa ada ya £13m.

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA 

RONALDO AMCHANA VIBAYA MOURINHO,AMPA TANO FERGUSON

Cristiano Ronaldo ameamua kufunguka kuhusiana na uhusiano wake na Kocha Jose Mourinho na kusema hakuwahi kuwa rafiki yake hata chembe. Licha ya Mourinho kuwahi kuwa rafiki yake na raia mwenzake wa Ureno, Ronaldo amesema hajawahi kuwa na urafiki naye, badala yake akasisitiza katika makocha, rafiki yake ni mmoja tu, Alex Ferguson aliyekuwa naye Manchester United. Aidha, Ronaldo amemlaumu Mourinho kwamba wakati akiwa kocha wa Madrid alisababisha mambo mengi kama ugomvi kati ya wachezaji na hata mashabiki. Mourinho hakuelewana na Iker Casillas, Angel Di Maria, Sergio Ramos na hata Mreno mwenzake, Pepe. Ronaldo amesema Mourinho alifanya hali ya hewa kutotulia ndani ya kikosi chao huku akisisitiza hayuko kwenye soka kutafuta marafiki, badala yake anataka kushinda.

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII NA KALIBU TENA NA KAMA UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA 

AMBAVYO WENGER HAKUAMINI MACHO YAKE LEO LEICESTER

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger wa pili kulia mbele akifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Englad kati yake na Leicester City jioni hii. Timu hizo zimetoka sare ya 1-1.

HUYU NDO MCHEZAJI ALIYEKAMILISHA UHAMISHO WAKE CHELSEA KUTOKA QPR

KLABU ya Chelsea imekamilisha uhamisho wa Loic Remy kwa dau la Pauni Milioni 8 kutokaq QPR. Remy aliyekuwa anatakiwa pia na Arsenal, anakwedna kuziba nafasi ya Fernando Torres aliyehamia AC Milan kwa mkopo wa mural mrefu. Uhamisho huu ni faraja kwa Remy ambaye sasa anakwenda kujiunga na klabu inayocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kocha Mreno, Jose Mourinho alihitaji mshambuliaji baada ya kumtoa kwa mkopo Torres.

Sunday, August 31, 2014

MATOKEO YA MECHI KATI YA LIVERPOOL vs TOTTENHAM HAYA HAPA

LIVERPOOL imeichapa mabao 3-0 Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa White Hart Lane. Mabao ya Liverpool yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya nane kwa shuti la umbali wa mita saba, Steven Gerrard dakika ya 48 kwa penalti baada ya Eric Dier kumchezea rafu Joe Allen na Alberto Moreno dakika ya 60. Mshambuliaji mpya, Mario Balotelli aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan wiki iliyopita, leo amecheza mechi yake ya kwanza Liverpool, lakini hakufunga licha ya kucheza soka nzuri. Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Manquillo, Moreno, Gerrard, Lovren, Sakho, Henderson, Sterling/Enrique dk86, Sturridge, Balotelli/Markovic dk61 na Allen/Can dk61. Tottenham Hotspur: Lloris, Dier, Rose/Davies dk72, Capoue, Kaboul, Vertonghen, Lamela, Bentaleb/Dembele dk59, Adebayor, Eriksen/ Townsend dk59 na Chadli.

HII NDIYO 'FIRST ELEVEN' YA PHIRI SIMBA SC, HAKUNA OKWI, MKUDE WALA KIONGERA...NA BADO KUNA WAKALI WENGINE WA KIKOSI CHA PILI WANATISHA

Hiki ndicho kikosi cha kwanza cha Simba SC, ambacho kocha Patrick Phiri amekuwa akikitanguliza dakika 45 za kwanza katika mechi zake visiwani Zanzibar. Na hiki ndicho kikosi kilichomaliza kipindi cha kwanza kinaongoza 4-0 dhidi ya KMKM jana katika ushindi wa 5-0. Kutoka kulia waliosimama ni Joram Mgeveke, Miraj Adam, Ivo Mapunda, Joseph Owino, Amri Kiemba, na Haroun Chanongo. Waliochuchumaa kutoka kulia ni Ramadhani Singano 'Messi', Pierre Kwizera, Shaaban Kisiga, Amisi Tambwe na Issa Rashid. Wachezaji watatu wa kiwango cha juu, Emmanuel Okwi, Paul Kiongerea na Jonas Mkude hawapo hapa. Na kuna wachezaji wa kikosi cha pili kama Said Ndemla, Elias Maguri, Twaha Ibrahim 'Messi' wanafanya vizuri. Hii inamaanisha Simba SC ipo vizuri kuelekea msimu ujao.

HII NDIYO 'FIRST ELEVEN' YA PHIRI SIMBA SC, HAKUNA OKWI, MKUDE WALA KIONGERA...NA BADO KUNA WAKALI WENGINE WA KIKOSI CHA PILI WANATISHA

Hiki ndicho kikosi cha kwanza cha Simba SC, ambacho kocha Patrick Phiri amekuwa akikitanguliza dakika 45 za kwanza katika mechi zake visiwani Zanzibar. Na hiki ndicho kikosi kilichomaliza kipindi cha kwanza kinaongoza 4-0 dhidi ya KMKM jana katika ushindi wa 5-0. Kutoka kulia waliosimama ni Joram Mgeveke, Miraj Adam, Ivo Mapunda, Joseph Owino, Amri Kiemba, na Haroun Chanongo. Waliochuchumaa kutoka kulia ni Ramadhani Singano 'Messi', Pierre Kwizera, Shaaban Kisiga, Amisi Tambwe na Issa Rashid. Wachezaji watatu wa kiwango cha juu, Emmanuel Okwi, Paul Kiongerea na Jonas Mkude hawapo hapa. Na kuna wachezaji wa kikosi cha pili kama Said Ndemla, Elias Maguri, Twaha Ibrahim 'Messi' wanafanya vizuri. Hii inamaanisha Simba SC ipo vizuri kuelekea msimu ujao.

HAYA NDO MAPYA YALIYOBUKA OLD TRAFORD KUHUSU ROJO

Mlinzi Marcos Rojo aliyesajiliwa Manchester United kutoka Sporting Lisbon ya Ureno anakabiliwa na shauri la jinai kwao Argentina, na ndilo linamzuia kuanza kuchezea timu yake mpya. Hadi Jumapili hii asubuhi alikuwa hajapatiwa visa ya kumwezesha kufanya kazi nchini, kutokana na madai kwamba ana kesi ya jinai ya kupigana na jirani nchini Argentina tangu 2010 ambayo bado ipo kwenye majalada ya polisi. Rojo (24) alikamilisha usajili kwa dau la pauni milioni 16 wiki mbili zilizopita, lakini upelelezi wa vitendo vyake vya jinai unasababisha zuio la yeye kupewa visa, walau kwa muda huu, japokuwa Kocha Mkuu wa Man U, Louis van Gaal anasema ana uhakika mchezaji huyo atakuwa tayari kwa mechi dhidi ya Queen Park Rangers (QPR) Septemba 14. Imeelezwa, hata hivyo, kwamba Chama cha Soka (FA) cha England kimeshamalizana na suala la mtu huyo wa tatu na kimetoa hati ya kumwezesha kucheza, lakini kinachosubiriwa sasa ni visa, kwani aliyoingia nayo ni ya utalii. Hivi sasa Rojo yupo Madrid, Hispania kwa ajili ya kusubiri kuhojiwa na watumishi wa Ubalozi wa Uingereza ambao watatathmini kwa kina ugomvi aliosababisha wakati huo, na wakiona inafaa watampatia visa ya kufanya kazi nchini Uingereza. Fernando Burlando ambaye ni mwanasheria wa Rojo, amedai kwamba mchezaji huyo aliyekuwa kwenye Timu ya Taifa ya Argentina ameshaonekana na polisi kuwa na kesi, hivyo anasubiriwa kupelekwa mahakamani, lakini akasema watalimaliza suala hilo. Amedai hata akitiwa hatiani, anaweza kuwekwa chini ya uangalizi na kupewa adhabu ya kufanya kazi za jamii, ambazo si lazima azifanyie nchini Argentina, hivyo ataweza tu kuingia Uingereza. Kabla ya mechi ya Jumamosi hii ya Man United dhidi ya Burnley iliyoisha kwa suluhu, Van Gaal alisema; “ni suala la muda tu. Mimi ni kocha wa klabu kubwa zaidi duniani lakini siwezi kubadili sheria.” Baada ya mechi hiyo, akasema; “naamini kwamba tutakapocheza na QPR atakuwa ameshaipata (visa).”

KIVAZI CHA LULU CHAWATESA WANAUME: JIONEE MWENYEWE HAPA

LICHA YA SKENDO, MIGOGORO KATIKA FAMILIA: FLORA MBASHA AJA NA MPYA:

Msanii wa muziki Florah Mbasha, Baada ya kufunguka mengi kuhusiana na matatizo katika ndoa yake wiki hii, ameweka wazi kuwa shughuli zake za muziki bado zinaendelea huku akiwa na albam mpya kabisa kwaajili ya wapenzi wa sanaa yake. Frorah Mbasha amesema kuwa, anamshukuru Mungu kwa kufanikisha kutoa albam mpya inayokwenda kwa jina Nipe Nguvu ya Kushinda, kazi ambayo tayari jamii imeipokea vizuri. Msanii huyu ambaye amezoeleka kufanya kazi ya muziki pamoja na mumewe Emmanuel Mbasha, amewatoa wasiwasi mashabiki kuwa licha ya mgogoro, Mumewe yupo katika kazi hii.

BAADA YA DIAMOND PLATNUMZ KUPELEKWA KWENYE SHOW SAA 10 ALFAJIRI HUKO GERMANY, DIAMOND ATOA YA MOYONI

kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany... kinachoniuma na kunisikitisha zaidi ni jins watu walivyoamua kujitolea kuja kutusupport vijana wao kwa wingi, halaf mwisho wa siku promoter anatupeleka wasanii kwenye show saa kumi alfajiri... najua ni kiasi gani mmeumia na kuwa disappointed... lakini naomba mtambue kuwa halikuwa ni kosa langu, coz mimi ni mgeni tu, na nafata maelekezo ya promoter...hivyo nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaoutaka mimi...

Beki hii ya Simba, mh!

KOCHA wa Mafunzo ya Zanzibar, Hemed Morocco, amesema kuwa kikosi cha Simba kinaendelea kuimarika hasa safu ya viungo na washambuliaji huku akidai bado kuna tatizo kubwa katika safu ya mabeki hasa beki ya pembeni. Juzi Jumatano Mafunzo ilicheza na Simba katika Uwanja wa Amaan ambapo iliambulia kipigo cha mabao 2-0 ila kocha huyo alidai kuwa alikuwa anakiangalia tu kikosi chake kwani bado hajaanza kazi rasmi. Morocco alisema kuwa Simba wana timu nzuri ila kocha Patrick Phiri anatakiwa kufanya marekebisho haraka hasa nafasi hiyo ili isije ikamgharimu katika mechi za Ligi Kuu Bara msimu ujao. “Ukiiangalia Simba ya sasa ni tofauti na ya msimu uliopita, nafasi ya kati na mbele wanacheza sana kwa kuelewana na wapo vizuri kuliko nafasi ya nyuma, sasa hilo ni tatizo ambalo kocha anatakiwa kulirekebisha,” alisema. “Kwa upande wa timu yangu ni vigumu kuzungumzia mapungufu yake kwani katika mechi hiyo nilikuwa naangalia tu kazi ya kuifundisha timu hiyo inaanza rasmi wiki ijayo, lakini kikubwa nampongeza Phiri kwa kuitengeneza upya Simba.” Katika mechi hiyo ya kirafiki, safu ya ushambuliaji ya Simba iliongozwa na Amissi Tambwe pamoja na Shaban Kisiga ambaye pia anacheza nafasi ya kiungo. Viungo ni Amri Kiemba, Pierre Kwizera, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Haruni Chanongo huku mabeki akiwatumia Issah Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Joram Mgeveke, William Lucian ‘Gallas’ huku golini akisimama Ivo Mapunda.credit mwanaspoti

Maximo: Wananichunguza? Wanapoteza muda wao

MWANASPOTI imewashuhudia makocha mbalimbali wa Ligi Kuu Bara kama wa Mbeya City, Juma Mwambusi, wa Simba Mzambia Patrick Phiri pamoja na Kocha Msaidizi wa JKT Ruvu, Nelson Haule wakiangalia ufundi wa Mbrazili wa Yanga, Marcio Maximo kwenye mechi yao ya kirafiki waliyocheza na Shangani wakashinda 1-0, lakini ufahamu walichoambiwa? Baada ya kuambiwa kwamba makocha wengine wameitazama Yanga kwa umakini kwenye mchezo huo, Maximo alifunguka na kusema huku akisisitiza: “Walipoteza muda wao tu, kama ni kuwafunga kupo palepale.” Alikwenda mbali na kusisitiza, mazoezi aliyoyafanya kwa wakati huo na sasa ni kuwaelekeza mbinu mbalimbali atakazotumia kwenye kipindi chote cha msimu, lakini kila mechi ataicheza kwa staili tofauti kulingana na namna wapinzani wake watakavyokuja. “Nawajua vizuri, Mwambusi, Phiri, Minziro (Fred) na wengineo ni marafiki zangu, lakini watambue kuwa hata wakiangalia na kufuatilia mbinu zangu kama kipigo kipo palepale, hawawezi kubadilisha kitu,” alisema Maximo. “Watambue kuwa hiki ninachowafundisha wachezaji wangu ni kwa ajili ya msimu mzima wa ligi, huwezi kuandaa timu kwa kungalia usoni yaani hapa karibu, natengeneza timu ya msimu mzima. “Lakini watambue mbinu nitakazotumia kucheza na Mtibwa Sugar mechi ya kwanza siyo nitakayoitumia kucheza na Mbeya City au Simba hapo baadaye ni ngumu. Hizo ni hofu zao tu, kama kipigo kipo pale pale.” Maximo hakuwahi kushuhudia mechi za Simba ikicheza Uwanja wa Amaan, lakini baadhi ya wachezaji na wasaidizi wake walihudhuria mechi hizo.credit mwanaspoti

Manji jeuri, aapa Okwi hachezi Simba

SIMBA kila kona nchini wanashangilia baada ya kumsainisha straika machachari mwenye mkataba na Yanga, Emmanuel Okwi. Lakini Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji, ameibuka na kutoa msimamo mkali kwa kusisitiza kwamba mchezaji huyo hatacheza Msimbazi. Manji aliyeonekana na uso wa furaha wakati wote wa mkutano wake na waandishi wa habari akiambatana na Makamu wake Clement Sanga, alisisitiza kwamba Yanga haiwezi kuwa chini ya mchezaji mmoja na kwamba hawajawahi kumuacha Okwi. Alisema kwamba wamemfungulia mashtaka ya kinidhamu TFF na hata katika orodha yao ya wachezaji wa kigeni waliopelekwa TFF jina la Okwi limo wakisubiri hatma ya kesi waliyoifungua. “Siku zote tumekuwa tukiwaheshimu hawa jamaa zetu, mtamkumbuka mara kadhaa nimekuwa nikiwapongeza hata wanapoifunga timu yangu, tumekuwa tukiwasajili wachezaji wengi wa Simba kama Kaseja (Juma), Yondani (Kelvin) lakini hatukuwa tunawasajili wakati wana mikataba tunasubiri mpaka mikataba yao inapomalizika,”alisema Manji. “Yanga hatuna desturi ya kulalamika waliondoka Kavumbagu (Didier) na Domayo (Frank) kwenda Azam hatukulalamika kwa kuwa utaratibu ulifuatwa na hata hili hatulalamiki kwa kuwa tunajua tunachokifanya, Yanga hatujamuacha Okwi, ni mchezaji wetu. “Inashangaza sana inawezekanaje mtu akawa na ugomvi na mkewe wakati huohuo kuna mtu mwingine anajitokeza kusikojulikana na kutangaza kufunga ndoa halali na mkeo, unaweza kujiuliza hawa watu wamekutana na kupatana wakati gani, linatutia shaka hili.” Manji alisema kwa kuwa tayari wameshafungua kesi ya kwanza ambayo kabla ya kujibiwa mchezaji husika ameongeza kosa lingine, sasa Yanga imewasilisha TFF mashtaka mengine ambayo sasa itawajumuisha Okwi, Simba na wakala wa mchezaji. Katika kesi hiyo sasa pande hizo tatu zitatakiwa kuilipa Yanga kiasi cha Dola 500,000 (Sh825mil). “Nina uwezo wa kuwanunua wachezaji wote wa Simba pamoja na kocha wao Phiri (Patrick) na kuwazuia wasicheze ligi wakae pale Gymkhana wachezee mpira na kulala, lakini nikifanya hivyo watu watalalamika Manji anaharibu mpira. “Najua kwamba mishahara ya wachezaji wangu wa Yanga ya miezi miwili pale Simba inawalipa wachezaji wao wote mwaka mzima, tunataka kuona TFF inawafungia Okwi na Simba tunatoa siku saba kujua hatma ya hilo ikishindikana hapo tutaenda Fifa na CAS (mahakama ya michezo),”alisisitiza Manji. TFF yamtambua Okwi Yanga TFF kupitia kwa Katibu wake Mkuu, Celestine Mwesigwa, amethibitisha kwamba ofisi yake haina mamlaka ya kutoa kibali chochote maalum cha kumpeleka Okwi kuichezea Simba ambapo kwa sasa bado wanamtambua mchezaji huyo kuwa ni mali ya Yanga.credit mwanaspoti

Amissi Tambwe azua balaa jipya Msimbazi

UVUMI kwamba uongozi wa Simba ulikuwa na mpango wa kumtema straika namba moja, Mrundi Amissi Tambwe, ili kumpisha Mganda Emmanuel Okwi, jana ulizua balaa kubwa baada ya baadhi ya mashabiki kutaka kuandamana Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, jijini Dar es Salaam kupinga, kabla ya uongozi kuzima mambo. Uvumi huo ulianza baada ya kudaiwa kwamba kocha Patrick Phiri amewaambia viongozi kwamba Mrundi mwingine, Pierre Kwizera na Okwi wanatosha katika safu yake ya mbele. Mapenzi ya mashabiki hao kwa Tambwe, yamejengwa na kiwango alichokionyesha straika huyo tangu alipotua klabuni hapo ambapo msimu uliopita ndiye aliyekuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara kwa kufunga mabao 19. Hadi tulipokuwa tunakwenda mitamboni jana usiku huku usajili ukiwa katika dakika za lala salama, Simba ilikuwa katika mazungumzoa na mabeki, Salum Salim Mbonde, wa Mtibwa na Juma Nyosso (huru) ili kumpata mmoja wao kuziba nafasi ya Mkenya, Donald Mosoti, ambaye ameomba kuachwa ili akacheze soka Qatar. Lakini Mwanaspoti linajua kwamba viongozi hao walikuwa wamewekeza akili zao kwa Mbonde kuliko Nyosso ambaye hata kocha Phiri anamkubali.credit mwanaspoti