Sunday, August 24, 2014

SPURS YAUA 4-0, ADEBAYOR NAYE ATUPIA NYAVUNI

Wazee wa dozi; Mshambuliaji wa Spurs, Emmanuel Adebayor akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao katika ushindi wa 4-0 dhidi ya QPR Uwanja wa White Hart Lane. Mabao mengine ya Tottenham Hotspur yamefungwa na Chadli mawili na moja Eric Dier kikosi cha Mauricio Pochettino kiking'ara leo katika Ligi Kuu ya England

DI MARIA SASA NI MOJA, MBILI, TATU, NNE.....

Muda wa mshambuliaji Angelo Di Maria kuondoa Real Madrid unaanza kuhesabika. Pamoja na kutangaza dau jipya la zaidi ya pauni milioni 70 ili Manchester United impate, lakini inaonekana Madrid imeshindwa kumzuia. Kwani leo asubuhi hakuonekana mazoezini na kitendo cha kocha Carlo Ancelotti kutomjumuisha kwenye mechi za Super Cup ya Hispania, inaonyesha kiasi gani hayuko kwenye hesabu za timu hiyo. Siku nne zilizopita, Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos walizungumza na uongozi na kuutaka ufanye juhudi kumbakiza. Lakini Muargentina huyo anaonekana kuchoshwa na kutopewa heshima yake, hivyo anaweza kuondoka ndani ya leo au kesho. Na mdadisiblog/festosaimon

DIEGO COSTA AKIVUTA MEHELA BAADA YA KUIPIGIA BAO CHELSEA JANA

Piga bao, vita mkwanja; Mshambuliaji mpya wa Chelsea Diego Costa aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 32 kutoka Atletico Madrid akitoa fedha kwa mashine za benki (ATM) muda mfupi baada ya kuifungia Chelsea katika ushindi wa 2-0 jana dhidi ya Leicester katika Ligi Kuu ya Englans. Diego amefunga mechi zote mbili za awali za Chelsea.

Mwanzo mzuri: Costa akishangilia bao lake la jana dhidi ya Leicester Uwanja wa Stamford Bridge dakika ya 62

JOSE MOURINHO AWACHARUKIA DIEGO COSTA NA WENZAKE LICHA YA KUSHINDA 2-0 DHIDI YA LEICESTER

Kibarua kizito: Diego Costa aliifungia Chelsea bao la kuongoza dhidi ya timu ngumu ya Leicester. JOSE Mourinho aliwajia juu wachezaji wake kuwa ni wavivu kufuatia kucheza vibaya kipindi cha kwanza licha ya ushindi wa mabao 2-0 waliopata jana dhidi ya Leicester. Chelsea walibanwa mbavu kipindi cha kwanza na timu mpya iliyopanda daraja ya Leicester kabla ya Mourinho kuwawashia moto wachezaji wake wakati wa mapumziko. Mabao ya Diego Costa na Eden Hazard yalitosha kuwapa ushindi The Blues katika dimba la Stamford Bridge. Vijana kazeni: Jose Mourinho aliwajia juu wachezaji wake baada ya kipindi cha kwanza kumalizika. Mourinho hakafurahishwa na mwanzo wa taratibu. Alisema: “Napenda kufanya mazoezi asubuhi, lakini wiki hii nilifanya mazoezi mchana kwasababu sio hali nzuri ya kucheza mpira, unapata uvivu”. “Kipindi cha kwanza timu ilicheza kivivu na sikupenda kabisa. “Lakini walijiboresha kipindi cha pili na kushinda, hiki ndicho kitu muhimu zaidi” “Wakati wa mapumziko tuliwakalipia kidogo. Niliwaambia kuwa jinsi tunavyocheza haitoshi kushinda mchezo na walikuwa katika hatari”. NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON

Fifa yataka kina Ronaldo wakacheze Morocco (kwenye EBOLA)

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa) limethibitisha kwamba Morocco itakuwa mwenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa Dunia kwa mwaka wa pili mfululizo licha ya kuwapo na wasiwasi wa ugonjwa wa Ebola. Maeneo ya Afrika Magharibi yamekuwa tishio kubwa kutokana na kuibuka kwa virusi hivyo vya ugonjwa wa Ebola na kuibua wasiwasi kama ni mwafaka kwa michuano hiyo kufanyika Morocco Desemba mwaka huu. Hata hivyo, Fifa imetangaza kwamba hakuna haja ya kuwa na wasiwasi na timu zitakuwa kwenye mazingira mazuri. “Afya za wachezaji, maofisa na mashabiki ni kitu kinachozingatiwa zaidi na Fifa kwenye michuano yake,” ilibainisha taarifa ya shirikisho hilo. “Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba hakuna kesi yoyote ya Ebola iliyoripotiwa Morocco, hivyo hakuna sababu ya kuzungumzia kubadili sehemu ya kufanyika kwa michuano hiyo. Kama kutakuwa na mabadiliko tutatoa taarifa.” Miongoni mwa timu zitakazoshiriki ni Real Madrid inayochezewa na masupastaa wa dunia, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, James Rodriguez na Toni Kroos.

Kigogo Simba akwama kumuiba Okwi Jangwani

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Emmanuel Okwi, huenda akaiingiza hasara klabu hiyo na inaweza kulazimika kuvunja mkataba wake kama hatajiunga nayo mpaka usajili utakapofungwa Agosti 27 huku ikielezwa kuwa kuna ujanja ulifanyika wa kughushi barua ya timu iliyoelezwa kuwa ana mpango wa kujiunga nayo. Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinadai kuwa Okwi ni mchezaji anayewasumbua na amechukua fedha nyingi, lakini katika uchunguzi uliofanywa umebainisha kuna mmoja wa wanazi na kiongozi wa Yanga alishirikiana na kigogo wa Simba kutaka kumrubuni Okwi kwa kughushi barua kwamba kuna timu inamtaka. Habari zinasema kwamba viongozi wa Yanga walifuatilia kwa umakini juu ya madai ya kuwapo kwa timu inayomtaka na kubaini kuwa barua iliyotumwa Yanga haikutoka katika klabu hiyo ambayo hata hivyo haitajwi wazi. Yanga ilimsajili Okwi kwa Sh116milioni na inamlipa mshahara wa Sh6milioni kwa mwezi. “Tulibaini kuna ujanja ulifanyika kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Yanga akishirikiana na mtu wa Simba kutengeneza uongo kwani klabu waliyosema inamtaka haina taarifa zozote, walitaka Okwi aachiwe ili ajiunge na Simba, hivyo bado tunaangalia jinsi ya kumchukulia hatua kiongozi huyo,” alidokeza kigogo wa Yanga. “Hapa kuna mawili, Yanga kuingia hasara kwa kuvunja mkataba na Okwi au Okwi kuendelea kuwepo katika timu, ila napo itategemea na kocha atakavyoamua kwani hataki mchezaji ambaye hana utayari wa kucheza, Okwi alisema atarudi ila hatujui ni lini.” Kwa upande wa Simba, ilielezwa kwamba suala la Okwi lilitinga katika vikao vya Kamati ya Usajili na kuleta mtafaruku mkubwa kwani wajumbe walio wengi hawakukubaliana na Okwi kurudi ingawa kigogo mmoja akawa anashinikiza na hakuungwa mkono.Credit mwanaspoti

KWA MZIGO WA PAUNDI MILIONI 60 ANGEL DI MARIA ANATUA OLD TRAFFORD

Fundi: Angel Di Maria aliichezea Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid katika mechi ya Super Cup MANCHESTER United wanakaribia kukamilisha usajili ghali wa Muargentina, Angel Di Maria kwa paundi milioni 60. Uhamisho huo ukikamilika utavunja rekodi ya klabu hiyo katika usajili. United wamekuwa wakifuatilia dili la nyota huyo wa Real Madrid kwa muda mrefu na inafahamika kuwa wametoa ofa ya mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki. kwa sasa inafahamika kuwa Di Maria imewaambia United kuwa atakuja Old Trafford na sasa klabu hiyo ipo katika mazungumzo ya kukubaliana ada ya uhamisho na Real madrid. Kiwango cha juu: Di Maria anatarajia kujiunga na Manchester United kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 60 na mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki. Kifaa cha ukweli: Gary Neville anaamini kuwa Di Maria ndio aina ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa na Manchester United. Na mdadisiblog/festosaimon

Ingia hapa kusoma habari zngine>>>> BONYA HAPA 

KISA NI CHA KWELI SIO HADITHI PITIA

Habari wana wadau…!!! Huu ni mkasa wa kweli kabisa na nipo njia panda mpaka sahivi sijui cha kufanya. Nipo kwenye mahusiano na mtoto mkali kweli wa kichaga na tunapendana sana, tumekuwa na mipango na future nzuri tu. Tumevumiliana kwenye shida na raha japo yeye bado anasoma na yupo mwaka wa mwisho. Yeye anakaa Arusha ila anasoma hapa Dar kwenye chuo kimoja. Sasa chuo kilipofungwa si akaenda likizo kwao na likizo hiyo ikaambata na field ya muda mrefu akaniacha hapa dar…!! Bwana weeeh kama ilivyo kawaida kiasili wanaume wengi ila sio wote tamaa ikaja nilikutana na demu mmoja nilikua nakaa nae kitaa na alikua jirani yangu kipindi iko nakaa home kwa wazazi nayeye pia alikua ameshahama kwao anajitegemea so wazazi wake na wangu wanafahamiana vizuri wana urafiki wa kawaida tu. Basi dem sikumtongoza ila tulibadilishana namba za simu tukawa tunawasiliana dem nikilmkaribisha getho anakuja. Alinipa historia ya maisha yake baada ya kupotezana kwa miaka mingi alikua na mtoto mmoja wa kike ila alikua hajaolewa bwana ake baada ya kumpa mimba na mtoto akazaliwa akazuga zuga kama kawaida akakimbia na kumuacha ila hela ya matumizi ya mtoto wake anapeleka kama kawaida kila mwezi. Tukawa marafiki anakuja getho na mm naenda kwake mara moja moja… sikutaka kumtongoza nilitaka siku akija getho nipige tu coz sometime tulikuwa tuna kunywa whisky, wine akiwa anakuja getho. Kuna siku nikalazimisha nikaishia kula mate…..!! siku zilivyokwenda nikamuomba game hapo sijamtongoza wala kumwambia nakupenda akawa staki nataka nikaona anazingua ngoja niachane nae nikawa nampotezea sasa ila kila siku lazima apige simu na kutuma sms sometime najibu ila sometime napotezea….!! Kuna siku akakasirika kwann siimjibu sms zake wala kupokea simu yake nikamwambia nipo tite sana na kazi akasema atafuta namba yangu mimi nikamwambia asifute ila anivumilie tu. Basi bwana siku, miezi ikapita nimeshaanza hata kumsahau ilikua ijumaaa mida ya saa 12 jioni mchepuko ukapiga simu upo wapi nikamwambia nipo getho akanambia napitia hapo nakuja.!! moyoni niksema leo lazima nikumalize ikishindikana leo basi naaachana kabisa na wewe. Nikaenda kuoga fast nikaandaa kondom za kutosha na nikapika chakula changu pale nikijiandaaa kumgegeda uyu kiumbe. Niliposhiba vizuri mtoto akaja siku hiyo hata sikupata tabu nilimshughulikia vya kutosha na alifurahi basi ikawa ndo mchezo wetu na tukakubaliana tukapime na tulivyopima tukajikuta tukawa fresh yani ikawa kama dozi kumbuka sijawahi kumwambia nakupenda. Basi kuna siku akaniuliza hivi unanichezea au unanipenda nikamjibu kwanza nina mpenzi yupo nje ya dar anarudi mwezi wa tisa ukae ukijua hilo nikamwambia tutaendelea hivi hivi akija itakua basi maana nay eye bwana ake wa zamani alikua anamsumbua so nikahisi pia watarudiana tu. Muda ukazidi kwenda nikawa nakula mzigo navyotaka safari hii nikawa naenda kwakwe pale kwangu nikamwambia haiwezekani kuja tena maana kuna mtu anafahamiana na mtoto wa kichaga so ataharibu mambo. Ilileta utata ila akaelewa kwa utata sana na vitisho juu so nikawa naenda tu kwakwe kula mzigo na kusepa..!! Basi mambo yakawa mambo Yule mchepuko akanambia ana mimba tukaenda kupima kweli alikua ana mimba ya mwezi mmoja akawa anataka kutoa mm nikamwambia asitoe nimeukubali yeye akasema sawa hataitoa hii mimba iwapo tu nikubali niende kwa wazazi wake nikajitambulishe moyoni nikasema labda ardhi ipasuke ndo naweza kwenda.. Nikamwambia si unakumbuka lakini nina mtu inawezekana kweli mm kufanya hivyo nikamwambia lea mimba itakua siri baada ya mwaka mmoja kila kitu kitajulikana na kitakuwa wazi kwa kila mtu na mm nitakupa ushirikiano wa kutosha kabisa.. Basi akakataaa akanitishia kutoa nikambembeleza wapi mwsiho wa siku nikamwambia uamuzi ni wako sasa ila siwezi muacha mchaga wangu ila nipo tayari kumkubali mtoto yeye akasema kama staki kwenda kwao anatoa nikamjibu utakua uamuzi wako sio wangu… sasa mchaga wangu anakaribia kuja na mchepuko umenambia umekubali mawazo yangu kuwa atafanya siri kwa mwaka mmoja ila sasa simwamini nahisi atakuja kuniharibia makusudi.. naomba ushauri hapo wadau nifanyaje

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA WIKIENDI HII ZIPO HAPA

Mshambuliaji wa England Danny Welbeck, 23, ameambiwa anaweza kuondoka Manchester United, wakati Louis van Gaal akiendelea kukisuka kikosi chake. Tottenham wameonesha nia ya kumtaka Welbeck (Times), mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o, 33, amefanyiwa vipimo vya afya Liverpool na atasaini mkataba wa mwaka mmoja Anfield (Daily Mirror), meneja wa Sunderland Gus Poyet hajakata tamaa kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Fabio Borini, 23, na anataka kuchukua wachezaji wengine wawili kwa mkopo (Daily Express), Barcelona walitoa dau la pauni milioni 48 kumtaka winga wa Real Madrid Angel Di Maria, 26, lakini ombi hilo lilikataliwa mara moja na rais wa Real Florentino Perez (sport.es), kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Pogba, 21, amefuta matumaini yoyote ya kurejea Old Trafford baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitano Juventus (Daily Star), Liverpool wamemuambia Mario Balotelli kuwa atapoteza pauni milioni 2 kwa mwaka iwapo ataonesha utovu wa nidhamu, baada ya pia kukubali kupunguza mshahara wake kutoka AC Milan (Sun), AC Milan wanatazama kati ya wachezaji sita kuziba pengo la Balotelli, akiwemo Javier Hernandez, 26, wa Man U, Roberto Soldado, 29, wa Spurs na Fernando Torres, 30, wa Chelsea (Gazetta dello Sport), Arsenal wanakaribia kumsajili beki wa Olympiakos Kostas Manolas, 23, kuziba pengo la Thomas Vermaelen aliyekwenda Barcelona (Goal), kipa wa Stoke City Asmir Begovic, 27, hatoondoka kabla ya dirisha la usajili kufungwa licha ya Liverpool, Manchester City, Arsenal na Real Madrid kuonesha dalili za kumtaka (Daily Mirror), AC Milan wanamtaka kiungo wa Chelsea Marco van Ginkel kwa mkopo (Inside Futbol), boss wa Sunderland Gus Poyet anamtaka Danny Welbeck wa Man U kwa mkopo (Sunderland Echo), Fredy Guarin anayesakwa na Man U anajiandaa kujiunga na Zenit St Petersburg baada ya Andre Villas Boaz kumshawishi mchezaji huyo kutoka Colombia kuhamia Urusi, ingawa lazima kwanza wafuzu kucheza Champions League (Gazetta dello Sport), Napoli wanafikiria kumchukua Marouanne Fellaini licha ya kumsajili Jonathan de Guzman (Corriere dello Sports), mshambuliaji wa Arsenal Lukas Podolski anajiandaa kurejea Ujerumani na kujiunga na Wolfsburg. Galatasaray na Besitkas wanamtaka mchezaji huyo, lakini anaonekana kwenda Bundesliga (Metro). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Zimesalia siku tisa kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Cheers!!