Sunday, December 21, 2014

REAL MADRID MABINGWA WA DUNIA, WABEBA KOMBE AFRIKA

Unaweza kusema kweli huu ni mwaka wa Real Madrid, kwani wamefanikiwa kuitwanga San Lorenzo kwa mabao 2-0 na kubeba ubingwa wa dunia. Madrid wametupia mabao hayo mawili kupitia kwa Sergio Ramos na Gareth Balena kubeba Kombe hilo katika ardhi ya bara maarufu la Afrika. Mechi hiyo ya fainali ya Kombe la Dunia kwa klabu, imepigwa mjini Marakech, Morocco. Cristiano Ronaldo hakuweza kufunga katika mechi hiyo ambayo Madrid imeshinda mara 21 mfululizo. Kwa...

Wednesday, November 19, 2014

Njia 5 za kumrudisha mpenzi wako baada ya kuzinguana

Katika uhusiano kunaweza kutokea ugomvi ambao ni wa kawaida na ambao hauhitaji nguvu kubwa kuumaliza lakini upo ule ambao ukitokea ni lazima nguvu ya ziada itumike ili kuweza kurudi katika mazingira ya amani na furaha. Kutokana na hilo, leo nimeona nizungumzie mbinu tano zinazoweza kukusaidia katika kumrudisha mpenzi wako ambaye mmezinguana lakini bado unampenda. Kumbuka wapo ambao wanagombana na inakuwa ndiyo mwisho wa uhusiano kutokana na ukweli...

HIKI NDO KITU KIKUBWA ALICHOKIFANYA ROONEY DHIDI YA SCOTLAND

ENGLAND imewalaza wenyeji Scotland mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa usiku huu. Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 32 na Wayne Rooney aliyefunga mabao mawili dakika za 47 na 85, wakati bao pekee la wenyeji lilifungwa na Andrew Robertson dakika ya 83. Kwa kufunga mabao hayo mawili, Rooney amekuwa mchezaji wa tatu kufunga mabao mengi katika historia ya timu ya taifa ya England kutokana na kufikisha...

JB kuja na filamu ya soka la Bongo

Muigizaji mahari wa filamu, Jacob Stephan aka JB, amesema yupo mbioni kuandaa filamu kuhusu soka la Tanzania. JB ambaye ni shabiki mkubwa Simba alisema hayo kwenye kipindi cha Kili Chart Show cha EATV baada shabiki mmoja kumuuliza kama ana mpango wa kufanya filamu ya aina hiyo. “Kwa sababu wengi wameguswa nitafanya tena filamu nyingine ya mpira, ambayo nitazungumzia moja kwa moja, mpira wa kitanzania, wazo lako nitalifanyiwa kazi na Jerusalem film,”...

Baada ya Mabasi ya Mwendokasi, Kivuko cha Mv. Dar, hii ni nyingine kuhusu usafiri Dar.

Baada ya Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi, Treni, Kivuko cha Mv. Dar es Salaam, leo kuna taarifa nyingine nzuri ambayo inahusu jitihada za Serikali kumaliza tatizo sugu la foleni katikati ya jiji la Dar es Salaam. Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha TBC1 , Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli amesema; “… Tuliwatuma wataalamu hawa, na bahati nzuri Chief Executive wa TANROADs hivi karibuni na wataalamu wenzake walienda South Korea.. Serikali ya South Korea...

Wednesday, November 12, 2014

Nuh mziwanda afunguka kuhusu kupewa kichapo na mpenzi wake kila anapokosea

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amefunguka kuwa watu wanaomsema vibaya kuhusu yeye kupewa kichapo na mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wanakosea kwani anaamini kufanywa hivyo ni mahaba. Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Mziwanda alisema kuna taarifa zimeenea kuwa huwa anapigwa na Shilole pindi anapokosea lakini ukweli si kupigwa ‘live’ bali ni kupigwa kimahaba. ‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake ‘Nuh Mziwanda’. “Jamani...

Saturday, November 01, 2014

Hiki ndicho kilichotokea ligi kuu England leo, matokeo ya michezo yote yapo hapa

Haya ndiyo matokeo ya ligi hiyo kwa leo;- Newcastle1 – 0 Liverpool FT Arsenal 3 – 0 Burnley FT Chelsea 2 – 1 QPR FT Everton 0 – 0 SwanseaFT Hull 0 – 1 Southampton FT Leicester 0 – 1 West Brom FT Stoke 2 – 2 West Ham ...

DE GEA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MAN UNITED KWA ASILIMIA 70

MASHABIKI wa Manchester United wamemchagua kipa David de Gea kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa klabu hiyo, baada ya Mspanyola huyo kupata asilimia 70 ya jura zilizopigwa kwenye mtandao. Licha ya kushindwa kuzuia nyavu zake kutikiswa katika mchezo wowote mwezi huo, De Gea alikuwa katika kiwango kizuri wakati United ikiifunga Everton kabla ya kutoa sare na West Brom ugenini na baadaye na vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea nyumbani. Mlinda mango...

ARSENAL YAUA 3-0 ENGLAND, SANCHEZ MBILI PEKE YAKE

ARSENAL imeng’ara katika Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burnley Uwanja wa Emirates, London. Hadi mapumziko hakuna bao lililokuwa limepatikana na iliwachukia hadi robo ya mwisho ya mchezo, The Gunners kuanza kuhesabu mabao yao. Alexis Sanchez alifunga bao la kwanza dakika ya 70, kabla ya Callum Chambers kuongeza la pili dakika ya 72 na Sanchez tena kuwainua vitini mashabiki wa Arsenal dakika ya 90. Kikosi cha Arsenal kilikuwa;...

RONALDO AFUNGA REAL MADRID IKISHINDA 4-0 LA LIGA NA KUPANDA KILELENI

REAL Madird imeichapa Granada mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania, maarufu La Liga jioni ya leo Uwanja wa Nuevo Los Carmenes. Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo aliifungia Real Madrid bao la kwanza dakika ya pili, kabla ya James Rodriguez kufunga la pili kipindi cha kwanza, Karim Benzema kufunga la tatu dakika ya 54 na James Rodriguez kukamilisha ushindi huo dakika za mwishoni. Ushindi huo, unaifanya Real ipae kileleni mwa La...