Tuesday, September 02, 2014

Alichosema Cristiano Ronaldo baada ya Falcao kuhamia Man United

Usiku wa jana klabu ya Manchester United ilikamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao kwa mkopo. Falcao ambaye alikuwa akiwindwa na vilabu vya Arsenal na Man City amejiunga na Man U akitokea klabu ya Monaco ambayo alijiunga nayo akitokea Atletico Madrid. Usajili wa mchezaji umezungumzia na watu wengi mmoja wao ni mchezaji bora wa ulaya na dunia – Cristiano Ronaldo. Akiongea jijini Madrid Ronaldo alisema: ‘Falcao ni mchezaji mzuri sana, nadhani Manchester United wamefanya jambo zuri kumsajili. Sidhani kabisa kama ni mchezaji asiyewafaa, ni mchezaji wa daraja la dunia na hivyo naamini huu usajili mzuri.”

NDEGE YAANGUKA NA KUUA ABIRIA WOTE MKOANI MARA: TAZAMA PICHA HAPA

Ndege iliyopotea mapema jana ikitokea Mwanza kuelekea Magadi nchini Kenya, imepatikana huko eneo la Serengeti Mara, na abiria wote watatu wamekufa.

New AUDIO | Zachaa ft Diamond Platnumz & Godzilla - Mtoto wa Mama | Download hapa

>>>>>>>>>>>====> BOFYA HAPA KUDOWNLOAD NGOMA HII ∞<========[[[[[>>

PERUZI KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI YA LEO JUMANNE HAPA

PEREZ AMPA CHICHARITO JEZI NAMBA 14 REAL MADRID

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez akimkabidhi jezi mshambuliaji mpya, Javier Hernandez 'Chicharito' aliyetua kwa mkopo kutoka Manchester United leo.

HATIMAYE SUNDERLAND YA SAJIL KIFAA HIKI CHA LIVERPOOL

Beki Sebastian Coates akiwa na skafu na jezi ya Sunderland baada ya kukamilisha uhamisho wa mkopo kutoka Liverpool.

FIRST ELEVEN NA MFUMO WA MAN UNITED BAADA YA KUMNASA RADAMEL FALCAO

Hivi ndivyo kikosi cha kwanza cha Manchester United kinavyotarajiwa kuwa baada ya kusajiliwa kwa Radamel Falcao kutoka Monaco kwa mkopo. Na mfumo utakuwa kama unavyoonekana hapo.

 BONYA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI KIRAHISI PUNDE ZITUFIKIAPO 

HATIMAYE DANNY WELBECK AONDOKA MAN UNITED AJIUNGA NA TIMU HII YA ENGLAND HAPO HAPO

Mshambuliaji wa kimataifa wa England na Manchester United Danny Welbeck amefuata mkumbo wa kundi la wachezaji walioihama Man united wiki hii. Baada ya Shinji Kagawa, leo hii imethibitishwa rasmi Danny Welbeck amejiunha na klabu ya Arsenal. Welbeck ambaye alijiunga na United tangu alipokuwa na miaka 7, amejiunga na Arsenal kwa ada ya uhamisho wa £16m na akisaini mkataba wa miaka minne. Welbeck ameshaichezea Man united mechi 142 huku akifunga jumla ya mabao 29.

 BONYA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI KIRAHISI PUNDE ZITUFIKIAPO 

Radamel Falcao ajiunga rasmi na Man United – soma alichosema hapa

Siku ya mwisho ya usajili barani ulaya imefungwa kwa staili ya aina yake na klabu ya Manchester United baada ya kufanikiwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao. United ambao leo hii imewauza washambuliaji wake wawili Chicharito na Danny Welbeck – imethibitisha kumsajili Falcao kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa mkopo huku wakiwa na option ya kumnunua moja kwa moja msimu ujao. Falcao anakuwa mchezaji wa sita kujiunga na Man United wakati wa dirisha hili la usajili, baada ya Luke Shaw, Herrera, Blind, Di Maria, na Rojo. Kocha Louis Van Gaal amesema mchezaji wa aina ya Falcao anakupokuwa na uwezekano wa kumpata basi hiyo sio nafasi ya kuipoteza. Falcao nae alisema: “Nina furaha kujiunga na Manchester United kwa mkopo. Manchester United ni klabu kubwa zaidi duniani na ina kila sababu ya kurudi kuwa juu tena. Nipo tayari kufanya kazi na Louis van Gaal na kuisadia timu kupata mafanikio katika kipindi nitakachokuwepo kwenye klabu.”

 BONYA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI KIRAHISI PUNDE ZITUFIKIAPO 

BAADA YA FALCAO HUYU NDO MCHEZAJI MWINGINE ALIYEKAMILISHA USAJILI WAKE MAN UNITED HAPO JANA

KLABU ya Manchester United imemsajili Daley Blind kwa dau la Pauni Milioni 14 katika jitihada za kocha Louis van Gaal kutatua tatizo la safu ya ulinzi Old Trafford. Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uholanzi mara moja amwatumia salamu mashabiki wa timu hiyo kwa kusema; "Ni heshima kusajiliwa na United. Siwezi kusubiri kufanya kazi na klabu dunia,". Inamaanisha Van Gaal ametumia zaidi ya Pauni Milioni 150 kwa usajili wa kipindi hiki - ambacho ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kutumiwa na klabu hiyo kwa miaka mitano iliyopita, huku Radamel Falcao naye akiwa mbioni kukamilisha uhamisho wa mkopo

 BONYA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI KIRAHISI PUNDE ZITUFIKIAPO 

Monday, September 01, 2014

INSTA PHOTO:HII NDIO PICHA KALI KUSHINDA ZOTE ZA MASTAA WAKIKE WIKI HII HUKO INSTAGRAM

LUIS SUAREZ LEO AREJEA LIVERPOOL NA HIKI NDICHO ALICHOFANYA

MSHAMBULIAJI Luis Suarez amerejea kwenye viwanja vya mazoezi vya Liverpool katika siku ya leo ya mwisho ya usajili... lakini nyota huyo aliyehamia Barcelona kwa Pauni Milioni 75 alikwenda kuchukua mizigo yake tu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 aliwasili akiwa na zawadi ndogo kwa Steven Gerrard - jezi ya Barca yenye nina lake- na Nahodha huyo wa Liverpool ameposti picha hiyo kwenye akaunti yake ya Instagram. Iliambatanishwa na ujumbe usemao: "Amekuja na zawadi kusema kwaheri kwa mtu muhimu asubuhi hii, namtakia mafanikio makubwa mchezaji,".

KIFAA KINGINE CHA CHELSEA CHAENDA AC MILAN KWA MKOPO

KINDA wa Chelsea, Marco van Ginkel amekamilisha uhamisho wa mkopo kwenda AC Milan, akifuata nyayo za Fernando Torres. Kiungo huyo wa Uholanzi, Van Ginkel sehemu kubwa ya msimu wake wa kwanza Stamford Bridge alikuwa anasumbuliwa na majeruhi na hivyo kocha Jose Mourinho ameamua kumtoa akapate uzoefu. Kuondoka kwa mchezaji huyo kunapunguza idadi ya wachezaji wa kigeni ili waweze kuendana na kanuni za mashindano ya Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

HATIMAYE CHICHARITO AONDOKA MAN UNITED NA HII NDO TIMU ALIYOTUA

Mshambuliaji wa Manchester United, Javier Hernandez 'Chicharito' yuko Madrid kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na klabu ya Real Madrid ya Hispania. Dirisha la usajili linafungwa

HUYU NDO MCHEZAJI ANAYETARAJIWA KUKAMILISHA USAJILI WAKE LEO HII MAN UNITED

KLABU ya Manchester United imeshinda mbio za kuwania saini ya mshambuliaji Radamel Falcao kutoka Monaco kwa mkopo wa mwaka mmoja. Mpachika mabao huyo ataigharimu klabu hiyo ya Old Trafford Pauni Milioni 12 kwenda kuungana na Angel di Maria, Daley Blind, Luke Shaw, Ander Herrera na Marcos Rojo katika orodha ya wachezaji wapya kwenye kikosi cha Louis van Gaal. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 28 tayari ameafiki kulipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki na anatarajiwa kutua Manchester wakati wowote kwa ndege binafasi kukamilisha taratibu.

Okwi apewa masharti magumu Simba

STRAIKA aliyesaini mkataba wa miezi sita na Simba, Emmanuel Okwi, amepewa masharti magumu ambayo asipoyatekeleza yatamgharimu. Viongozi wa Kamati ya Usajili ya Simba wameamua kumshupalia mchezaji huyo kutokana na rekodi zake za usumbufu wa mara kwa mara ikiwamo kwenda kwao na kuchelewa kurudi kambini. Akizungumza na Mwanaspoti Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zacharia Hans Poppe, amesema wanaelewa tabia za Okwi na wamekaa naye na kumpa masharti kwamba anatakiwa kubadilika kwa vile nafasi waliyompa ndiyo ya mwisho vinginevyo hawataweza kumvumilia. Bosi huyo aliyemtambulisha Okwi mwishoni mwa wiki iliyopita, alisema wamemsisitiza Okwi kujituma na kuimarisha kiwango chake kwa muda huu ili arudi kwenye fomu aliyokuwa nayo siku za nyuma kwani Simba ni timu kubwa na haitetemekei umaarufu wa mchezaji. Alisema Simba waliyoisajili sasa inaweza kufanya makubwa bila kumtegemea Okwi na ndiyo maana wamempa mkataba ambao utamruhusu kuondoka kama akipata timu popote. “Tunatambua hilo la tabia yake, kila kitu kipo wazi tumemweleza kwamba tunamkaribisha katika timu yetu, lakini anatakiwa kuangalia maisha yake yalivyokuwa kila timu aliyokwenda na sasa hii nafasi tuliyompa ni kama nafasi ya mwisho kwake kutakiwa kujirekebisha,” alisema Hans Poppe. “Hatukuwa tunamuhitaji sana Okwi katika timu yetu lakini kwa kuwa alikuja kutuomba tukalazimika kumkubalia, sasa tumemweleza kwamba hatuna mchezaji anayejiona ni muhimu zaidi kuliko wengine. Simba ya sasa kila mchezaji ni muhimu. “Hata yeye mwenyewe ameliona hilo juzi katika mechi yetu na amekiri kwamba akizembea anaweza kuishia benchi kutokana na uwezo wa wachezaji wetu wa sasa. “Amejionea mwenyewe kwamba tunaweza kufanya makubwa bila yeye, sasa hilo lipo mikononi mwake.” Simba juzi Jumamosi usiku iliwachapa KMKM ya Zanzibar mabao 5-0 katika mchezo wa kirafiki. Mafowadi wa Simba wamewapiku wa Yanga kwenye ufungaji wa magoli kwenye michezo ya kirafiki visiwani Zanzibar baada ya timu zote kucheza michezo mitatu mitatu huku Simba ikishinda kwa mzabao wakati Yanga ikiambulia matano. Kwa upande wa Simba, mchezo wa kwanza ulikuwa ni dhidi ya Kilimani City ambapo Simba ilishinda mabao 2-1, wafungaji walikuwa Shabani Kisiga pamoja na Haroun Chanongo.

MDA HUU WAFANYA BIASHARA WA KARIAKOO WAFANYA MGOMO MZITO KUPINGA MASHINE ZA EFD

Picha hali Ilivyosasa kariakoo ambapo Wafanyabiashara wamefunga Maduka Yao ikidaiwa Kupinga matumizi ya mashine ya EFD..Hii ndo hali ilivyo asubuhi hii wafanyabiashara wa soko la kariakoo leo wamefunga maduka yao.

POMBE SIO CHAI JAMAA BIA MBILI TU KAANZA KUVUA NGUO NA KUWEKA MAPOZI YA KIMISI WATU WAMPIGE PICHA

Pombe usipoweza kuicontrol basi matokeo yake ita Control wewe ! Huyu Jamaa Alinawa na Kamera za Udaku Specially Katika Baa Moja Maarufu Mitaa ya Sinza , Inasemekana Alikuwa na Wenzake wanakunywa Baada ya Kupata Bia Mbili tu zikampanda Kichwani na Kuanza kuweka Mapozi ya Ajabu Ajabu na Mwisho Kuvua nguo na kuweka Mapozi ya Kimiss Watu Wampige Picha, Wenzake kuona Hivyo Wakamkimbia na Kumwacha Mchizi akiabika Kiaina..

BILA RONALDO, REAL MADRID YAPIGWA 4-2 LA LIGA

REAL Mdrid jana imefumuliwa mabao 4-2 na Real Sociedad katika mchezo w La LIga Uwanja wa San Sebastian. Kocha wa Real, Carlo Ancelotti alimkosa Cristiano Ronaldo, ambaye alimpumzisha hivyo kuwategemea Gareth Bale, James Rodriguez na wenzake. Sergio Ramos aliifungia Real bao la kwanza dakika ya sita, kabla ya Bale kufunga la pili dakika ya 11, lakini wenyeji wakatoka nyuma na kushinda 4-2 wakimtungua Iker Casillas. Mabao ya Inigo Martinez dakika ya 36, Carlos Vela aliyetokea benchi dakika ya 76 na David Zurutuza mawili dakika za 41 na 65 yalitosha kuirdisha Real mikono mitupu mjini Madrid. Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Carvajal/Arbeloa dk77, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric/Khedira dk74, Kroos, Isco, Bale, Benzema na Rodriguez. Real Sociedad: Zubikarai, Zaldua, Elustondo, I Martinez, De La Bella, Bergara, Granero, Prieto/Gonzalez dk83, Zurutuza, Castro/ Canales dk59 na Agirretxe/Vela dk59.

IKIWA YAMEBAKI MASAA DIRISHA LA USAJIL KUFUNGWA HIZI NI TETESI ZA USAJILI ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA

Arsenal huenda wanakaribia kumsajili Alessio Cerci, 27, kutoka Torino baada ya mchezaji huyo kuachwa katika kikosi kitakachocheza na Inter Milan Jumapili (Daily Star), Arsenal wanakaribia kumsajili kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin, 24, baada ya kukubali kutoa pauni milioni 24 (CaughtOffSide), Manchester United huenda ikashuhudia wachezaji 11, ama wakiondoka, au kuingia Old Trafford kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu (Daily Star), Real Madrid wapo tayari kuwajaribu tena Manchester City kumtaka Alvaro Negredo, 29 (Mirror), Louis van Gaal alimshawishi Robin van Persie kuahirisha upasuaji wa goti kabla ya Kombe la Dunia, lakini sasa huenda akamkosa mshambuliaji huyo wakati fulani msimu huu (Daily Mirror), Juventus wanaamini kukamilisha uhamisho wa Radamel Falcao. Real sasa wanamtaka Javier Hernandez (Gazetta dello Sport), Arsenal wameacha kumfuatilia Loic Remy wa QPR ambaye anajiandaa kujiunga na Chelsea (BBC).