Monday, September 01, 2014
|
REAL Mdrid jana imefumuliwa mabao 4-2 na
Real Sociedad katika mchezo w La LIga Uwanja
wa San Sebastian.
Kocha wa Real, Carlo Ancelotti alimkosa
Cristiano Ronaldo, ambaye alimpumzisha
hivyo kuwategemea Gareth Bale, James
Rodriguez na wenzake.
Sergio Ramos aliifungia Real bao la kwanza
dakika ya sita, kabla ya Bale kufunga la pili
dakika ya 11, lakini wenyeji wakatoka nyuma
na kushinda 4-2 wakimtungua Iker Casillas.
Mabao ya Inigo Martinez dakika ya 36, Carlos
Vela aliyetokea benchi dakika ya 76 na David
Zurutuza mawili dakika za 41 na 65 yalitosha
kuirdisha Real mikono mitupu mjini Madrid.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas,
Carvajal/Arbeloa dk77, Pepe, Ramos, Marcelo,
Modric/Khedira dk74, Kroos, Isco, Bale,
Benzema na Rodriguez.
Real Sociedad: Zubikarai, Zaldua, Elustondo, I
Martinez, De La Bella, Bergara, Granero,
Prieto/Gonzalez dk83, Zurutuza, Castro/
Canales dk59 na Agirretxe/Vela dk59. |
0 comments:
Post a Comment