Thursday, August 28, 2014

SIMBA YAMRUDISHIA OKWI JEZI NAMBA 25, KESHO ANAPAA KWENDA ZANZIBAR

Baada ya kumpokea kwa mikono miwili, Simba imeamua kumrudishia Emmanuel Okwi jezi yake namba 25. Kabla ya kuondoka kwenda Etoile du Sahel alipouzwa 'bure' na Simba chini ya Ismail Aden Rage, Okwi alikuwa akitumia jezi hiyo. Yanga pia walimpa jezi hiyo, lakini leo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amethibitisha kuwa Simba imempa Okwi namna 25. Baada ya kupokea namba hiyo, Okwi kesho anapaa Zanzibar kuungana na wenzake ambao wako kambini kujiandaa na Ligi Kuu Bara.

Habari zingine BOFYA HAPA 


Posted via Blogaway

SIMBA YAMRUDISHIA OKWI JEZI NAMBA 25, KESHO ANAPAA KWENDA ZANZIBAR

Baada ya kumpokea kwa mikono miwili, Simba imeamua kumrudishia Emmanuel Okwi jezi yake namba 25. Kabla ya kuondoka kwenda Etoile du Sahel alipouzwa 'bure' na Simba chini ya Ismail Aden Rage, Okwi alikuwa akitumia jezi hiyo. Yanga pia walimpa jezi hiyo, lakini leo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amethibitisha kuwa Simba imempa Okwi namna 25. Baada ya kupokea namba hiyo, Okwi kesho anapaa Zanzibar kuungana na wenzake ambao wako kambini kujiandaa na Ligi Kuu Bara.

Habari zingine BOFYA HAPA 


Posted via Blogaway

TFF YAIBEBA YANGA KWA ‘ JAJA’

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam, Shirikisho la soka nchini, TFF limesogeza mbele muda wa usajili kwa klabu za ligi kuu na ligi daraja la kwanza kwa masaa 48 zaidi, Siku mbili kwa wachezaji wa ndani na wiki moja zaidi kwa usajili wa wachezaji wa kigeni kutoka nje ya nchini. Uamuzi huo umefikiwa baada ya klabu zote 14 za ligi kuu na 15 za ligi daraja la kwanza kushindwa kukamilisha taratibu za uhamisho wa Kieloktroniki. Ni timu moja tu iliyoweza kukamilisha usaajili wake siku ya jana ambayo ilikuwa ni ya mwisho baada ya mara mbili kuongezwa kwa muda. Yanga SC wameshindwa kupata hati ya uhamisho wa kimataifa ( ITC) ya mshambulizi, Geilson Santos ‘ Jaja’ na kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo kutoka Brazil akaondolewa kat ika timu hiyo. Katikati ya mwaka 2010 timu hiyo ilishindwa kukamilisha taratibu za kumuhamisha mshambulizi raia wa Ghana, Keneth Asamoah aliyekuwa akichezea klabu ya FK Jagodina ya Serbia. Jaja anaweza kutemwa na kuwapisha Waganda, Hamis Kizza na Emmanuel Okwi kuungana na wachezaji wengine wa kimataifa, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Andry Coutinho. Jina la mchezaji halipo katika orodha ya wachezaji wa Yanga na hakuna maombi yoyote ambayo uongozi wa Yanga umewasilisha kwa shirikisho la soka nchini, TFF hadi kufikia siku ya jana. Kama mshambulizi huyo atakwama kusajiliwa kama ilivyokuwa kwa Asamoah huku akiwa na mkataba wa miaka miwili uongozi hautakwepa lawama hivyo wanatakiwa kufanya kila wawezalo na si kujiaminisha kupata msaada wa muda mrefu kutoka kwa Okwi, na Kizza. Afadhali kwa Kizza yeye ni mchezaji wa Yanga hasa ila Okwi ataendelea kuwasumbua Yanga. Uongozi wa Yanga unasema kuwa kumekuwa na tatizo la mawasiliano kati yao na Shirikisho la soka la Brazil, CBF, ila hawajafanya jitihada za kupeleka maombi hayo rasmi kwa TFF ambao watafanya mawasiliano na wenzao wa Brazil ili kuhakikisha mchezaji huyo anasajiliwa na kukamilisha taratibu zote. Itakuwa ni sawa na kukosa umakini kwa viongozi wa Yanga kwa kuwa wamekuwa wakifahamu, Jaja ni mchezaji wao mpya tangu mwezi uliopita. Mfumo wa TMS umekuwa ukiwasumbua viongozi wa klabu za Tanzania lakini maombi ya uhamisho wa wachezaji yanayofanywa kutumia mfumo huo hufanyika haraka. ‘ SaSA Yanga wamepata muda zaidi wa kufikiria kwa umakini ni mchezaji gani wa kigeni anayetakiwa kuachwa kati ya washambuliaji hao watatu. Kulikuwa na uwezekano mkubwa wa Jaja kuachwa, lakini matumaini ya Mbrazil huyo kucheza Tanzania yamerejea baada ya muda zaidi wa usajili kuongezwa.

Posted via Blogaway

KWA MARA YA KWANZA RONALDO AFUNGUKA KUHUSIANA NA URAFIKI WAKE NA MESSI

Kwa mara ya kwanza mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunguka kuhusiana na uhusiano wake na Lionel Messi na kusema anamheshimu hasa juhudi zake za kutaka mafanikio kama mchezaji pamoja na klabu yake ya Barcelona.

SWALI. Baada ya miaka mitano sasa na Real Madrid, umechoka kulinganishwa na Messi au umejifunza jambo?
JIBU. Ni sehemu ya kazi tu kama vile ambavyo kwenye mashindano ya langalanga (Formula 1), watu wanafananisha kati ya Ferrari na Mercedes. Haya yamekuwa maisha yangu hapa Madrid, lakini najua mambo yanabadilika na hata nilipokwenda Manchester kulikuwa na mengine tofauti.
SWALI. Kumekuwa na taarifa kwamba uhusiano wako wewe na Messi nje ya mpira umekuwa si mzuri?
JIBU. Si kweli, sisi ni marafiki, ni marafiki kazini. Binafsi sina rafiki nje ya mpira, pia sina urafiki na Messi nje ya mpira. Anajitahidi kufanya makubwa katika klabu yake na timu ya taifa, sawa ninavyofanya mimi. Tunachezea timu zenye upinzani mkubwa na huenda ushindani huo unafanya watu wayakuze hayo mambo.
SWALI. Unafikiri wewe na Messi, siku moja mtakutana, mkae na kuanza kujadili haya yaliyotokea huku mkiangua vicheko kwa furaha?


JIBU. Nafikiri inawezekana, soka ni mchezo wa furaha, soka ni kitu kikubwa na unaweza kuufananisha na saa. Ndiyo maana nashauri kuwaangalia wapinzani kwa jicho la mafanikio na kukubali wanachofanya kwa vile ni kitu kizuri.


Posted via Blogaway

USAJILI LIGI KUU BARA WASOGEZWA MBELE TENA, SABABU YENYEWE NI ‘KICHEKESHO KWELI KWELI’

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM DIRISHA la usajili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa wachezaji wazalendo limesogezwa mbele kwa Saa 48 kuanzia jana, kutokana na timu kushindwa kukamilisha usajili katika muda husika jana. Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, sababu za kusogeza mbele ni klabu zote za Ligi Kuu kushindwa kukamilisha usajili jana. “Nadhani wameshindwa kuutumia huu mfumo wetu mpya wa elektroniki, sasa tumewapa Saa 48 zaidi warekebishe, zikiisha hizo, hapo hakuna nafasi tena, tunasonga mbele,”amesema Mwesigwa. Amesema kwamba hadi muda wa kufunga usajili jana Saa 6:00 usiku, ni timu moja tu, Kimondo FC ya Daraja la Kwanza ndiyo iliyokuwa imefanikiwa kukamilisha usajili wake katika mfumo huo. “Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Kimondo kwa kumudu kuutumia mfumo huu na kuwasilisha usajili wao ndani ya muda,”amesema. Aidha, Mwesigwa amesema kwamba dirisha la usajili kwa wachezaji wa kigeni litafungwa Septemba 6, mwaka huu. “Hili dirisha la wachezaji wa kigeni likifungwa, hakuna nyongeza ya muda tena, kwa kuwa hili lipo katika mfumo wa kimataifa chini ya FIFA, likifungwa, limefungwa dunia nzima, hivyo nawasihi viongozi wa klabu wahakikishe hawafanyi makoasa,”amesema.

Posted via Blogaway

Mtoto wa miaka 9 alivyomuua Mwalimu akimfundisha kutumia bunduki.

Pale ambapo kwanza unaweza kushtushwa na umri mdogo wa mtoto mwenyewe aliekua anafundishwa kufyetua risasi kwenye bunduki, hii imetokea Arizona nchini Marekani ambapo mtoto wa miaka 9 ndio kichwa cha habari kwenye mafunzo ya kutumia submachine gun iliyotengenezwa Israel. Mtoto huyu wa kike anaetokea New York alikua kwenye mapumziko na matembezi kama mtalii kwenye mji wa Arizona ambako pia ndio alichukua time yake ya ziada kujifunza kutumia bunduki lakini kwa bahati mbaya risasi ikafyetuka na kumjeruhi mwalimu wake aitwae Charles Vacca mwenye umri wa miaka 39 ambae alifariki baadae hospitalini. Wakati tukio linatokea mtoto huyu alikua na wazazi wake ambapo tovuti ya bullets and burgers imesema watoto kati ya miaka 8 na 17 wanaweza kufyetua risasi kama iwapo tu watakua chini ya uangalizi wa Mzazi au Mwalimu. Hii sio mara ya kwanza kwa tukio kama hili, ilishawahi kutokea mwaka 2008 ambapo mtoto wa miaka 8 alijiua kwa bahati mbaya kwa risasi kwenye onyesho la bunduki hukohuko Marekani.

Posted via Blogaway

Namna utapeli wa kutumia majina ya watu unavyotumika,msikilize Godzila feki akimtapeli mtu.

Mara chache zinapotoka stori za mtu kutaperiwa na mtu akidhani labda ni star fulani alikua akiwasiliana nae kiasi hadi cha kumuamini na kumtumia pesa lakini anapotuma pesa anashangaa kuona mtu huyo anavyobadilika. Watu wa namna hii wanapopata wanachokitaka huwa wanazima simu au hawapokei kabisa,sasa kwenye meza ya Soudy Brown kuna msanii mchanga kataperiwa na Godzilla ‘feki’ kwa kumtaka amtumie kiasi fulani cha pesa kisha wafanye colabo. Bonyeza play kusikiliza.

Source millardayo


Posted via Blogaway

Umeisoma ripoti ya leo kuhusu chai na chakula kwenye bunge la katiba? Nishiida!!

Gazeti la Mtanzania August 28 2014 ndio limeripoti hii stori kuhusu Bunge la Katiba linaloendelea Dodoma, kikubwa ni gharama mbalimbali zinazotumiwa na Wajumbe. Wameandika bunge la katiba lateketeza mamilioni ya fedha ambapo kikombe cha chai na biskuti au karanga kinalipiwa shilingi elfu 10 kila siku kwa kila Mjumbe mmoja licha ya kwamba kila Mjumbe anapokea posho ya siku ambayo ni laki mbili na elfu 30. Kwenye sentensi ya pili wameandika, chakula cha mchana kila Mjumbe analipiwa elfu 16 kwa siku ambapo kwa siku hiyohiyo iendayo kwa Mungu, ni shilingi milioni 8 hulipwa kama gharama za ukumbi wa kufanyia mikutano

Hungana na familia ya kihabari kwa ku BONYA HAPA 


Posted via Blogaway

PICHAZ: K LYINN NI MREMBO WA KUZALIWA …TAZAMA PICHA HIZI!!

Q-Jay kusikika tena kwenye bongo fleva baada ya ukimya mrefu toka aokoke

Baada ya miaka kadhaa tangu mwimbaji wa R&B Joseph Kelvin Mapunda aka Q-Jay wa Wakali Kwanza kutangaza kuacha game ya bongo fleva, anatarajiwa kusikika tena kwenye muziki huo katika wimbo mpya. Q-Jay ni miongoni mwa wasanii watakaosikika kwenye wimbo mpya wa Dj Aaron unaotarajiwa kutoka Ijumaa (Agosti 29). Dj Aaron amewashirikisha Banana Zorro, Barnaba na Q- Jay katika wimbo huo uitwao ‘Peace One Day’, ambao ni wa kuhamasisha amani. Miaka kadhaa iliyopita Q-Jay aliyewahi kufanya vizuri na nyimbo kama ‘Sifai’, aliamua kuachana na muziki wa kidunia baada ya kuokoka na kutangaza kuwa atakuwa akifanya muziki wa gospel.

Ungana na familia ya habari kwa ku BOFYA HAPA 


Posted via Blogaway