Thursday, August 28, 2014

SIMBA YAMRUDISHIA OKWI JEZI NAMBA 25, KESHO ANAPAA KWENDA ZANZIBAR

Baada ya kumpokea kwa mikono miwili, Simba imeamua kumrudishia Emmanuel Okwi jezi yake namba 25. Kabla ya kuondoka kwenda Etoile du Sahel alipouzwa 'bure' na Simba chini ya Ismail Aden Rage, Okwi alikuwa akitumia jezi hiyo. Yanga pia walimpa jezi hiyo, lakini leo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amethibitisha kuwa Simba imempa Okwi namna 25. Baada ya kupokea namba hiyo, Okwi kesho anapaa Zanzibar kuungana na wenzake ambao wako kambini kujiandaa na Ligi Kuu Bara.

Habari zingine BOFYA HAPA 


Posted via Blogaway

0 comments:

Post a Comment