Thursday, August 28, 2014
 |
| Na Baraka
Mbolembole,
Dar es Salaam,
Shirikisho la
soka nchini,
TFF limesogeza
mbele muda
wa usajili kwa
klabu za ligi
kuu na ligi
daraja la
kwanza kwa
masaa 48 zaidi,
Siku mbili kwa
wachezaji wa
ndani na wiki
moja zaidi kwa
usajili wa
wachezaji wa
kigeni kutoka
nje ya nchini.
Uamuzi huo
umefikiwa
baada ya klabu
zote 14 za ligi
kuu na 15 za
ligi daraja la
kwanza
kushindwa
kukamilisha
taratibu za
uhamisho wa
Kieloktroniki.
Ni timu moja
tu iliyoweza
kukamilisha
usaajili wake
siku ya jana
ambayo ilikuwa
ni ya mwisho
baada ya mara
mbili
kuongezwa kwa
muda.
Yanga SC
wameshindwa
kupata hati ya
uhamisho wa
kimataifa ( ITC)
ya
mshambulizi,
Geilson Santos
‘ Jaja’ na kuna
uwezekano
mkubwa wa
mchezaji huyo
kutoka Brazil
akaondolewa
kat
ika timu hiyo.
Katikati ya
mwaka 2010
timu hiyo
ilishindwa
kukamilisha
taratibu za
kumuhamisha
mshambulizi
raia wa Ghana,
Keneth
Asamoah
aliyekuwa
akichezea klabu
ya FK Jagodina
ya Serbia.
Jaja anaweza
kutemwa na
kuwapisha
Waganda,
Hamis Kizza na
Emmanuel
Okwi kuungana
na wachezaji
wengine wa
kimataifa,
Haruna
Niyonzima,
Mbuyu Twite
na Andry
Coutinho. Jina
la mchezaji
halipo katika
orodha ya
wachezaji wa
Yanga na
hakuna
maombi yoyote
ambayo
uongozi wa
Yanga
umewasilisha
kwa shirikisho
la soka nchini,
TFF hadi
kufikia siku ya
jana. Kama
mshambulizi
huyo atakwama
kusajiliwa kama
ilivyokuwa kwa
Asamoah huku
akiwa na
mkataba wa
miaka miwili
uongozi
hautakwepa
lawama hivyo
wanatakiwa
kufanya kila
wawezalo na si
kujiaminisha
kupata msaada
wa muda
mrefu kutoka
kwa Okwi, na
Kizza.
Afadhali kwa
Kizza yeye ni
mchezaji wa
Yanga hasa ila
Okwi
ataendelea
kuwasumbua
Yanga.
Uongozi wa
Yanga unasema
kuwa
kumekuwa na
tatizo la
mawasiliano
kati yao na
Shirikisho la
soka la Brazil,
CBF, ila
hawajafanya
jitihada za
kupeleka
maombi hayo
rasmi kwa TFF
ambao
watafanya
mawasiliano na
wenzao wa
Brazil ili
kuhakikisha
mchezaji huyo
anasajiliwa na
kukamilisha
taratibu zote.
Itakuwa ni
sawa na kukosa
umakini kwa
viongozi wa
Yanga kwa
kuwa
wamekuwa
wakifahamu,
Jaja ni mchezaji
wao mpya
tangu mwezi
uliopita.
Mfumo wa TMS
umekuwa
ukiwasumbua
viongozi wa
klabu za
Tanzania lakini
maombi ya
uhamisho wa
wachezaji
yanayofanywa
kutumia
mfumo huo
hufanyika
haraka.
‘
SaSA Yanga
wamepata
muda zaidi wa
kufikiria kwa
umakini ni
mchezaji gani
wa kigeni
anayetakiwa
kuachwa kati
ya
washambuliaji
hao watatu.
Kulikuwa na
uwezekano
mkubwa wa
Jaja kuachwa,
lakini
matumaini ya
Mbrazil huyo
kucheza
Tanzania
yamerejea
baada ya muda
zaidi wa usajili
kuongezwa. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment