Thursday, August 28, 2014
 |
| Pale ambapo kwanza unaweza kushtushwa na
umri mdogo wa mtoto mwenyewe aliekua
anafundishwa kufyetua risasi kwenye bunduki,
hii imetokea Arizona nchini Marekani ambapo
mtoto wa miaka 9 ndio kichwa cha habari
kwenye mafunzo ya kutumia submachine gun
iliyotengenezwa Israel.
Mtoto huyu wa kike anaetokea New York
alikua kwenye mapumziko na matembezi kama
mtalii kwenye mji wa Arizona ambako pia ndio
alichukua time yake ya ziada kujifunza
kutumia bunduki lakini kwa bahati mbaya
risasi ikafyetuka na kumjeruhi mwalimu wake
aitwae Charles Vacca mwenye umri wa miaka
39 ambae alifariki baadae hospitalini.
Wakati tukio linatokea mtoto huyu alikua na
wazazi wake ambapo tovuti ya bullets and
burgers imesema watoto kati ya miaka 8 na
17 wanaweza kufyetua risasi kama iwapo tu
watakua chini ya uangalizi wa Mzazi au
Mwalimu.
Hii sio mara ya kwanza kwa tukio kama hili,
ilishawahi kutokea mwaka 2008 ambapo
mtoto wa miaka 8 alijiua kwa bahati mbaya
kwa risasi kwenye onyesho la bunduki
hukohuko Marekani. |

Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment