Thursday, August 28, 2014
 |
Baada ya miaka kadhaa tangu mwimbaji wa
R&B Joseph Kelvin Mapunda aka Q-Jay wa
Wakali Kwanza kutangaza kuacha game ya
bongo fleva, anatarajiwa kusikika tena kwenye
muziki huo katika wimbo mpya.
Q-Jay ni miongoni mwa wasanii watakaosikika
kwenye wimbo mpya wa Dj Aaron unaotarajiwa
kutoka Ijumaa (Agosti 29). Dj Aaron
amewashirikisha Banana Zorro, Barnaba na Q-
Jay katika wimbo huo uitwao ‘Peace One Day’,
ambao ni wa kuhamasisha amani.
Miaka kadhaa iliyopita Q-Jay aliyewahi kufanya
vizuri na nyimbo kama ‘Sifai’, aliamua
kuachana na muziki wa kidunia baada ya
kuokoka na kutangaza kuwa atakuwa akifanya
muziki wa gospel. |
Ungana na familia ya habari kwa ku BOFYA HAPA
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment