Thursday, August 28, 2014
 |
| Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
DIRISHA la usajili la Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kwa wachezaji wazalendo
limesogezwa mbele kwa Saa 48 kuanzia jana,
kutokana na timu kushindwa kukamilisha
usajili katika muda husika jana.
Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Selestine Mwesigwa ameiambia BIN ZUBEIRY
leo kwamba, sababu za kusogeza mbele ni
klabu zote za Ligi Kuu kushindwa kukamilisha
usajili jana.
“Nadhani wameshindwa kuutumia huu mfumo
wetu mpya wa elektroniki, sasa tumewapa Saa
48 zaidi warekebishe, zikiisha hizo, hapo
hakuna nafasi tena, tunasonga
mbele,”amesema Mwesigwa.
Amesema kwamba hadi muda wa kufunga
usajili jana Saa 6:00 usiku, ni timu moja tu,
Kimondo FC ya Daraja la Kwanza ndiyo
iliyokuwa imefanikiwa kukamilisha usajili wake
katika mfumo huo. “Napenda kuchukua fursa
hii kuwapongeza Kimondo kwa kumudu
kuutumia mfumo huu na kuwasilisha usajili
wao ndani ya muda,”amesema.
Aidha, Mwesigwa amesema kwamba dirisha la
usajili kwa wachezaji wa kigeni litafungwa
Septemba 6, mwaka huu. “Hili dirisha la
wachezaji wa kigeni likifungwa, hakuna
nyongeza ya muda tena, kwa kuwa hili lipo
katika mfumo wa kimataifa chini ya FIFA,
likifungwa, limefungwa dunia nzima, hivyo
nawasihi viongozi wa klabu wahakikishe
hawafanyi makoasa,”amesema. |
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment