Wednesday, August 27, 2014

Mascherano ajifunga kitanzi kizito Barcelona

Beki kisiki Javier Mascherano ameongeza mkataba wake wa kuichezea Barcelona. Mascherano raia wa Argentina, sasa ataichezea Barcelona hadi mwaka 2018 na amesema ni furaha kubwa kwake. Mkataba huo umesainiwa leo na kila upande umeonyesha kuwa na furaha kuhusiana na mkataba huo mpya.

Pata habari nyingi za kimichezo kwa kuingia >>>>>>>>>>>>>> ingia hapa <<<<<<<<<<

BARUA YA DI MARIA YAWAACHA NA MAJONZI WACHEZAJI, MASHABIKI WA REAL MADRID

Kiungo mshambuliaji mpya wa Manchester United, Angel Di Maria ameandika barua iliyowasikitisha wachezaji na mashabiki wa Real Madrid. Di Maria ambaye ametua Man United kwa dau la pauni milioni 60 ambalo ni rekodi England, amesema hakupanga kuiacha timu hiyo ya Hispania. Mashabiki waliochangia kwenye mtandao wa Twitter wameelezwa kusikitishwa na barua hiyo huku wakiamini siku moja, Di Maria atarejea tena katika klabu yao. Amesema wakati anakwenda kwenye Kombe la dunia baada ya kutwaa ubingwa wa Ulaya ‘La Decima’ akiwa na Madrid, alitarajia kurudi na kuendelea na kazi yake. “Hata hivyo kuna mambo yalijitokeza, yakiwemo ya mshahara wangu na sasa natarajia kuyapata Manchester United, moja ya klabu kubwa duniani na nina imani nitaweka historia pale,” alieleza katika sehemu ya barua hiyo. Di Maria ameeleza atakavyowakumbuka wachezaji wengi wa Madrid na maisha yao kwa ujumla. Tayari Muargentina huyo amemalizana na Man United na baadhi ya wachezaji wa Madrid kama Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos, hawakutaka aondoke.

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA UPATE HABARI ZA KIMICHEZO KIRAHISI KABISAA 

Official: Everton yamsaini Samuel Eto’o – aizungumzia Liverpool

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya FC Barcelona na Chelsea Samuel Eto’o amekamilisha usajili wa kujiunga na Klabu ya Everton. Eto’o ambaye alikuwa akikaribia kujiunga na liverpool amejiunga na Everton na kusaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili. Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Cameroon ameripotiwa kusononeshwa na uhamisho wake kwenda Liverpool kufeli wakati akiwa tayari ameshafanya mpka vipimo vya afya. Eto’o anatarajiwa kuanza kuichezea Everton wikiendi hii kwa mchezo dhidi ya Chelsea ambayo aliitumikia msimu uliopita.

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA ILI UPATE HABARI ZA KIMICHEZO KIRAHISI ZAID 

Uhusiano mpya unaosemekana kutoka kwa Kajala na Quick Rocker

Kama ikiwa ni kweli inaweza ikawa ni uhusiano mwingine amabayo inahusu sanaa kutoka kiwanda cha Bongo Movie na Bongo Fleva na kuwa kwenye mastar wa Tanzania waliyo kwenye uhusiano. Kwa Tanzania ukimtoa Wema Sepetu na Diamond watu wengine walio kwenye uhusiano na kutangaza kabisa ni pamoja na Nuh Mziwanda na Shilole ingawa pia zilishawahi kutoka stori za Msami wa THT na Irene Uwoya kuwa wapenzi. Soudy Brown kapiga stori na meneja wa Kajala ambaye alikua nae Kajala pamoja na Quick Rocker hata wiki iliyopita Tanga,ambaye nae kazungumza kinachoendelea katikati yao hao watu wawili. Kikubwa alichozungumza meneja wa Kajala ni juu ya kazi mpya ya filamu ambayo inategemewa kutoka siku si nyingi ambayo inamhusisha Kajala na Quick Rocker,filamu hiyo inaitwa Mbwa Mwitu.

Source millardayo BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA FAMILIA YA HABARI ILI UPATE HABARI KIRAHISI PUNDE ZITUFIKIAPO: 

CAPITAL ONE: MAN U YAPIGWA KIPIGO CHA MBWA MWIZI NA KITIMU CHA MCHANGANI,GIGGS AMWAGA CHOZI

Wachezaji wa MK Dons wakishangilia bao lao la kwanza
Analia: Kocha Msaidizi Ryan Giggs akiwa ameshika kichwa akilia kwa uchungu mwishoni mwa mchezo huo, huku kocha Louis van Gaal akiwa haamini macho yake
Wachezaji wa United wakiwa hoi baada ya kipigo

KOCHA Louis van Gaal ameendelea kuogelea katika bwawa la maji moto Manchester United, baada ya usiku huu kfungwa na Mk Dons ya Daraja la Kwanza mabao 4-0 katika michuano ya Kombe la Ligi, maarufu Capital One. Mabao yaliyomtia machungu Van Gaal leo yamefungwa na Will Grigg dakika ya 25 na 63 na Benik Afobe anayecheza kwa mkopo kutoka Arsenal dakika ya 70 na 83. Kocha Msaidizi Ryan Giggs alionekana kufuta machozi baada ya bao la tatu, akiwa kwenye benchi na bosi wake, van Gaal. Kikosi cha MK Dons: Martin, Baldock, Kay, McFadzean, Lewington, Carruthers, Potter, Reeves, Alli, Bowditch, Grigg. Subs: Green, Spence, Randall, McLoughlin, Powell, Hitchcock, Afobe. Man Utd: De Gea, Vermijl, Evans, Michael Keane, James, Janko, Anderson, Kagawa, Powell, Welbeck, Hernandez.

Tuesday, August 26, 2014

UNAWEZA KUZIELEZEAJE PICHA PICHA HIZI!!! UKIWA KAMA MTU MWENYE AKILI ZAKO TIMAMAMU!!

VAN GAAL MENO THELATHINI NA NJE, YOTE MBILI AKIWA NA WAKALA WA DI MARIA LEO

DILI la Angel di Maria kutua Manchester United linakaribia kabisa kutimia baada ya wakala wake, Jorge Mendes kupigwa picha akiwa na kocha wa Mashetani hao Wekundu, Louis van Gaal. Van Gaal alikuwa akitabasamu na Mendes wakati wawili hao wakiwa kwenye gari kuelekea viwanja vya mazoezi vya United leo wakitazamiwa kukamilisha dili la Di Maria na klabu hiyo.

DUH POZI GANI HILI?!! NANI AMETISHA ZAIDI…..UNAWEZA HATA KUOA?HUMU HUMU

LA LIGA:MATOKEO NA WAFUNGAJI WA MECHI KATI YA REALMADRID vs CORDOBA UWANJA WA BERNABEU

REAL Madrid jana imeuanza vyema msimu mpya wa La Liga kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cordoba iliyopanda daraja Uwanja wa Bernabeu. Shukurani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Mfaransa Karim Benzema dakika ya 30 na Mwanasoka Bora wa Dunia, Mreno Cristiano Ronaldo dakika ya 90. Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Arbeloa/Carvajal dk73, Ramos, Pepe, Marcelo, Kroos, Modric, Bale, James/Isco dk72, Ronaldo na Benzema/Khedira dk76. Cordoba: Carlos, Gunino, Inigo, Pantic, Crespo, Rossi, Garai, Pinillos/Cartabia dk46, Ryder/Fidel dk62, Lopez Silva na Havenaar/ Xisco dk67.

TAZAMA PICHA ZA KILICHOJIRI KATIKA PARTY ILIYOANDALIWA NA DIVA WA CLOUDS FM PALE MAISHA CLUB

Juzi ndani ya Club Maisha dar es salaam,kulikua na Party kubwa iliyoandaliwa na Mtangazaji wa Kituo cha Clouds Fm Ala za
Roho, Party hii ilihudhuriwa na wajanja wengi wa Town na burudani ilitolewa na Rapper Chidi Benz ambaye kwa muda
mrefu hajaonekana kwenye Majukwaa na sasa hivi anai promote Ngoma yake mpya
Mpaka Kuchwee aliyo washirikisha
Diamond na Ambwene Yesaya (A.Y) Chidi alipokelewa na vizuri na mashabiki waliohudhuria usiku huo, wengine walioperform ni Bob Junior Sharobaro mwenye nyota ya chips Mayai, Kassim Mganga kutoka Manza Bay Tanga, Shilolole
Kiuno pamoja na Mpenzi wake Nuh
Mziwanda wao ndio walifunga kazi kabisa kwa kula denda on stage, Godzilla pia aliperform pamoja na Wadananda, Party hii
iliisha mida ya saa kumi na moja alfajiri.