Wednesday, August 27, 2014
 |
Kiungo mshambuliaji mpya wa
Manchester United, Angel Di
Maria ameandika barua
iliyowasikitisha wachezaji
na mashabiki wa Real
Madrid.
Di Maria ambaye ametua Man
United kwa dau la pauni
milioni 60 ambalo ni rekodi
England, amesema hakupanga
kuiacha timu hiyo ya
Hispania.
Mashabiki waliochangia
kwenye mtandao wa Twitter
wameelezwa kusikitishwa na
barua hiyo huku wakiamini
siku moja, Di Maria
atarejea tena katika klabu
yao.
Amesema wakati anakwenda
kwenye Kombe la dunia baada
ya kutwaa ubingwa wa Ulaya
‘La Decima’ akiwa na
Madrid, alitarajia kurudi
na kuendelea na kazi yake.
“Hata hivyo kuna mambo
yalijitokeza, yakiwemo ya
mshahara wangu na sasa
natarajia kuyapata
Manchester United, moja ya
klabu kubwa duniani na nina
imani nitaweka historia
pale,” alieleza katika
sehemu ya barua hiyo.
Di Maria ameeleza
atakavyowakumbuka wachezaji
wengi wa Madrid na maisha
yao kwa ujumla.
Tayari Muargentina huyo
amemalizana na Man United
na baadhi ya wachezaji wa
Madrid kama Cristiano
Ronaldo na Sergio Ramos,
hawakutaka aondoke. |
KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA UPATE HABARI ZA KIMICHEZO KIRAHISI KABISAA
0 comments:
Post a Comment